Jan 18, 2014

Coastal Union wakanusha wachezaji wao kutakiwa Oman

 

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
  Kuna taarifa zimeanza kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu suala la wachezaji watatu wa Coastal Union, kutaka kuchukuliwa na klabu moja hapa nchini Oman.

Nikiwa msemaji wa Coastal Union, ambae nimeambatana na timu nchini hapa naweka wazi kuwa taarifa hizo hazina ukweli. Hakuna kitu kama hicho.

Nimezungumza na mwenyekiti wa Coastal Union, Hemed Hilal ‘Aurora’ ambae pia yupo hapa Oman, na ameonyesha kusikitishwa sana na taarifa hizo na mtoa taarifa aliwahi kumuuliza na alimpa majibu hayohayo kuwa hakuna kitu kama hicho.

Vilevile imedaiwa kuwa uongozi umeshaanza mazungumzo na klabu hiyo inayotaka kuwachukua wachezaji watatu, hakuna kitu kama hicho uongozi haujafanya mazungumzo yoyote na klabu nchini hapa.

Aidha ikiwa kitu kama hicho kipo si vibaya, kwani inaonyesha ni namna gani wachezaji wa Coastal Union wanacheza soka la kuaminika, lakini kuzungumza mambo kwa hisia hiyo ni kinyume na taaluma ya uandishi wa habari.

Hivyo ibaki kuwa mpaka sasa hakuna mchezaji yeyote alietakiwa na klabu, lakini ikiwa kuna klabu imeonyesha kuridhishwa na kiwango cha mchezaji yeyote klabu inaweka wazi milango yake kufanya mazungumzo kwani hiyo ni kawaida na ni bahati kwa mchezaji na klabu.

HAFIDH KIDO (Msemaji)
COASTAL UNION
MUSCAT, OMAN
+986 97695911
 

0 Weka maoni yako hapa:

Post a Comment

COMMENT HAPA