Mchenguaji anayewakilisha ngome ya Miraba Minne, Nash MC ameachia wimbo wake mpya alioupa jina la ‘Naandika’.
Wimbo umetayarishwa katika studio za Kali Nation na Jeysan Keyz.
Mdundo wa wimbo huu ulikuwa wa Wasalu Muhammad Jaco aka Lupe Fiasco na
mtayarishaji aliyeuandaa ni Needlz aliyeandaa midundo ya mastaa kibao
akiwemo 50 Cent, The Game, Bruno Mars, Ludacris na wengine.
“Naandika kuhusu mitaa kwa hisani ya watu wa maskani, unaandika
mapenzi hiyo ni kwa hisani ya radio flani. Kwa hisani ya promo mnarudi
utumwani, haujui siri yeyote unaandika kwa hisani ya kusikika hewani.” Anarap Nash Mc kwenye wimbo huu.
chanzo na timefc
0 Weka maoni yako hapa:
Post a Comment
COMMENT HAPA