Kasisi mmoja mashuhuri wa kanisa moja nchini Kenya alizimia na kufariki
dunia katika hali ya kutatanisha akiwa ndani ya nyumba ya mwanamke
ambaye sie mke wake.
Mwanamke amesema kuwa kasisi alikuwa nyumbani kwake kwa maombi
Tukio hili lilishuhudiwa katika mtaa wa Buruburu mjini Nairobi Kenya.
Mwili wa kasisi huyo kwa jina Geoffrey Maingi wa kanisa la Redeemed
Gospel church mjini Nairobi, ulipatikana ndani ya chumba cha mwanamke
huyo,baada ya kufarikini kutokana na sababu ambazo hazijulikani mnamo
siku ya Jumanne.
Polisi walisema kuwa kasisi Maingi mwenye umri
wa miaka 70, aliingia katika nyumba ya muumini mmoja wa kanisa lake kwa
kile ambacho muumini huyo mwanamke alisema ilikuwa maombi maalum wakati
alipofariki.
Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 40 ambaye
alitalakiana na mumewe mwaka jana kutokana na ugomvui wa kinyumbani,
aliambia polisi kuwa Maingi alikuwa amemtembelea kwa maombi kabla ya
kuzirai na kufariki.
Kadhalika alisema kuwa kasisi huyo amekuwa akija
nyumbani kwake kwa maombi,kwani mbali na kuwa kiongozi wake wa kanisa
pia ni rafiki yake wa karibu.
Alihojiwa na kuachiliwa ingawa uchunguzi ungali unaendelea.
Kifo cha mzee huyo kilivutia hisia kutoka kwa
majirani waliokuwa wanadai kuwa kasisi huyo alifariki kutokana na
kutumia tembe za kuongeza nguvu mwili.
BONDE FC NI MABINGWA WAPYA WA BEIRA YOUTH CUP 2012
-
Timu ya Bonde fc jana iliibuka kuwa mabingwa wapya wa BEIRA YOUTH CUP
2012 ubingwa huo umepatikana baada ya kuibuka na ushindi wa gili 5-4 dhidi
ya New B...
12 years ago
0 Weka maoni yako hapa:
Post a Comment
COMMENT HAPA