|
|
|
kikosi cha timu ya Taifa |
Kocha
Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen amesema ili kuitoa Msumbiji ‘Mambas’
kwenye michuano ya Afrika ni lazima timu yake ishinde mechi ya marudiano
itakayochezwa Juni 17 mwaka huu jijini Maputo.
Mechi
ya marudiano kusaka tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Mataifa ya
Afrika (AFCON)
zitakazofanyika mwakani nchini Afrika Kusini itachezwa
kwenye Uwanja wa Taifa ulioko Zampeto nje kidogo ya Jiji la Maputo
kuanzia saa 9 mchana kwa saa za huko.
Kim
amewaambia Waandishi wa Habari leo (Juni 13 mwaka huu) kuwa maandalizi
ya kikosi chake yanakwenda vizuri ingawa ana wachezaji watatu ambao ni
majeruhi; kipa Mwadini Ali, na mabeki Nassoro Masoud Cholo na Waziri
Salum.
Amesema
wachezaji hao hawatakuwemo kwenye msafara wa timu hiyo utakaoondoka
Juni 15 mwaka huu saa 11 alfajiri kwa ndege ya Kenya Airways kupitia
Nairobi.
Kocha
huyo amesema baada ya mechi tatu maendeleo kiuchezaji kwa timu yake
inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager ni mazuri ingawa bado
anafanyia kazi kwa nguvu safu ya ushambuliaji. Mechi iliyopita Taifa
Stars iliifunga Gambia 2-1 huku mabao yote yakifungwa na mabeki.
Iwapo
Taifa Stars itaitoa Msumbiji katika raundi ya mwisho itapangiwa moja
kati ya timu 16 zilizocheza Fainali za AFCON zilizofanyika Januari mwaka
huu katika nchi za Gabon na Equatorial Guinea. Katika mechi ya kwanza
dhidi ya Msumbiji iliyochezwa Dar es Salaam, Februari 29 mwaka huu timu
hizo zilitoka sare ya bao 1-1.
Taifa
Stars ambayo msafara wake utakuwa na wachezaji 20 itaagwa kesho (Juni
14 mwaka huu) saa 6 mchana kambini kwao- hoteli ya Accommondia (Tansoma)
jijini Dar es Salaam. Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA)
kwa ajili ya kujenga afya kupitia mpira wa miguu.
|
0 Weka maoni yako hapa:
Post a Comment
COMMENT HAPA