Oct 30, 2013

Exclusive:Rado asema uhusiano mbaya ni chanzo cha baadhi ya wakongwe kupotea,hajawasiliana na Fid Q tangu alipotoa 'Usiulize'

Exclusive:Rado asema uhusiano mbaya ni chanzo cha baadhi ya wakongwe kupotea,hajawasiliana na Fid Q tangu alipotoa

Rapper Rado toka mwanza ambae kwa kipindi kirefu amekuwa nje ya game la bongo hasa ‘Main stream’ amesema kuwa mahusiano mabaya kati ya wadau wa muziki na wasanii wakongwe ni chanzo cha baadhi ya wasanii wakongwe kupotea katika game.

“Mi nachoweza kusema wazi kuwa tatizo ni kuwepo mahusiano mabaya kati ya wadau wa muziki na wasanii wakongwe, mahusiano hayo yameharibiwa zaidi kutokana na watu kufanya hii sanaa ku-base katika masilahi binafsi, kwa sababu unakuta wadau wanajua wasanii wa muda mrefu wana taarifa nyingi kwa hiyo huwezi kumpanga kila siku. Kwa sababu bahati mbaya kumekuwa hakuna hilo, mpaka uwe una mtu ndo ueleweke.” Amesema Rado aka Uso.

 “Hakuna ile misingi halisi, kwenye hip hop tunaita element. Na hii inasababisha wasanii hata wa muda mrefu washindwe kulalamika.” Ameongeza Rado.

Akizungumza kuhusu uhusiano wake kwa sasa na Fid Q ambae hawakuwa na mahusiano mazuri miaka mingi iliyopita, Rado amesema hakuwahi kuwasiliana nae tangu alipoachia ‘Usiulize’.

“Hatukuwasiliana kabisa, na hii inatokana na content zilizokuwepo, mwanzoni tulikuwa tunawasiliana zaidi kuliko baada, baada hatukuwa tena na mawasiliano kwa sababu tayari yeye ana content nyingine, na mimi nina content nyingine.” Rado anaeleza.

Rapper huyo ambae wiki hii ameachia wimbo wa pamoja akiwa na Azma unaoitwa ‘Nia Moja’, amesema kwa sasa anafanya project iliyobeba harakati alizozipa jina ‘Chemichemi na Wana’ itakayohusisha wasanii wengi zaidi nchini.

Rado ameiambia tovuti hii kuwa ana wimbo mpya atakaoanza kuusambaza soon, na kwamba anafanya kazi na studio ya One Love FX ya jijini Mwanza
.
Sikiliza ‘The Jump Off’ ya 100.5 Times fm kuanzia saa mbili usiku hadi saa nne kupa undani wa project ya ChemChem na Wana. Unaweza kusikiliza kupitia tovuti hii, http://www.timesfm.co.tz 

chanzo na http://www.timesfm.co.tz

1 Weka maoni yako hapa:

Anonymous said...

AMSHIA WANA_TUNARUDISHIANA PUMZI

Post a Comment

COMMENT HAPA