Nov 8, 2013

Wasanii wa filamu wadaiwa kukwepa mwaliko bungeni leo kwenye hoja kuhusu marekebisho kwenye sheria ya Filamu

Wasanii wa filamu wadaiwa kukwepa mwaliko bungeni leo kwenye hoja kuhusu marekebisho kwenye sheria ya Filamu

Waigizaji wa filamu nchini leo wanadaiwa kukwepa mwaliko bungeni walikotakiwa kwenda muswada wa marekebisho kwenye sheria ya Filamu na Michezo ya Kuigiza (1976).

Kupitia Twitter muigizaji mrembo, Yobnesh Yussuph maarufu kama Batuli, amesema amefuatilia mjadala huo kupitia TV lakini amesikitishwa kubaini kuwa wapo wasanii walioalikwa lakini hawakwenda bungeni.
“Yes nimefuatilia bunge ila cha kusikitisha ni wasanii waliopewa mwaliko halafu hawajaudhuria,” aliandika Batulli.

“Nalaani sana kitendo cha walioalikwa kutokufika bungeni kwenye hoja nyeti kama hii nikiwajua sitawanyamazia,” aliongeza.

Naye Lulu alijibu: Hatujichukulii serious ndo mana hatuchukuliwi serious pia..unaachaje kuhudhuria mwaliko unaokuhusu halafu umealikwa? Ndo tatizo la kutokuwa na umoja, haya tutaendelea kulia tu.”

CHANZO  NA  http://www.timesfm.co.tz/

0 Weka maoni yako hapa:

Post a Comment

COMMENT HAPA