Vyanzo: Sakata la Diamond kuvaa sare za jeshi, Babu Tale ashikiliwa na polisi, Kamanda wa polisi azungumza
Kufuatia tukio la Diamond Platinumz kuonekana akiperform na sare
zinazoaminika kuwa za jeshi la Wananchi (JWTZ), imeelezwa kuwa jeshi la
Polisi limemshikilia meneja wa Diamond, Babu Tale na inaelezwa kuwa
alilala selo.
Kwa mujibu wa chanzo chetu kilichokuwa katika eneo la kituo cha
polisi cha Osterbay, Dar es Salaam jana (October 21), Babu Tale
alifikishwa katika kituo hicho ambapo maafisa kadhaa wa jeshi na polisi
walionekana katika eneo hilo.
Chanzo hicho kimeeleza kuwa Uongozi wa Diamond ulipewa muda wa
kujieleza kabla ya saa mbili asubuhi, October 21 lakini haukufanya hivyo
na ndipo hatua hiyo ikachukuliwa.
Haijafahamika bado kwa nini jeshi la Polisi lilimshikilia Babu Tale
peke yake bila Diamond lakini vyanzo vimeeleza kuwa mwanamuziki huyo
yuko safarini.
Hadi habari hii inaenda hewani, namba ya simu ya Babu Tale ilikuwa haipatikani.
Tovuti ya Times Fm imeongea na kamanda wa polisi wa mkoa wa kipolisi
wa Kinondoni, Dar es Salaam, Camillus Wambura ambaye amesema bado
hajawasiliana na kituo cha Osterbay kuhusu suala hilo na hajapata
taarifa kwa kuwa kesi hiyo inachunguzwa na iko chini ya mkuu wa
upelelezi wa Mkoa.
“Mimi ninachojua kuwa suala hilo liko chini ya uchunguzi. Habari ya
kushikiliwa watu na nini bado sijafahamu. Najua tu suala hilo liko
chini ya uchunguzi na linafanyiwa uchunguzi. Hiyo ni kesi ambayo iko
chini ya mkuu wa upelelezi wa Wilaya, chini ya mkuu wa upelelezi wa
Mkoa. Kwa hiyo sijapokea taarifa ya uchunguzi huo ulipofika.” Ameiambia
tovuti ya Times Fm.
Akijibu kuhusu taarifa za uongozi wa Diamond na Diamond kupewa muda wa kujieleza, Kamanda Wambura alijibu:
“Uchunguzi unafanywa huko. Kwa sasa hivi sina taarifa hiyo nina mambo
mengi sana. Kwa hiyo kwa sasa hivi uchunguzi unafanywa chini ya Mkuu wa
Upelelezi wa Mkoa. Kwa hiyo sijapata nafasi ya kujua wamefikia wapi
katika uchunguzi wa suala hilo,”ameongeza kamanda Wambura.
Mapema wiki hii, jeshi la wananchi Tanzania lilitoa taarifa kwa vyombo vya habari likipiga marufuku raia kuvaa sare za jeshi.
chanzo na http://timesfm.co.tz
0 Weka maoni yako hapa:
Post a Comment
COMMENT HAPA