Katibu wa Baraza la Wazee wa klabu ya Yanga SC Mzee Ibrahim Akilimali akiongea na waandishi wa habari leo makao makuu ya klabu
Baraza la Wazee wa Klabu ya Young Africans leo wamefanya mkutano na
waandishi wa habari makao makuu ya klabu na kuwakemea wanachama
wanaosema ya kwamba watapeleka baarua TFF kwa ajili ya kuushitaki
uongozi kuwa wamevunja Katiba kwa kuongeza muda wa mwaka mmoja kuwa
madarakani.
Akiongea na waandishi wa habari makao makuu ya klabu, Katibu wa
Baraza la Wazee Bw Ibrahim Akilimali amesema kwa niaba ya Baraza la
Wazee wanasema wanachama wanaopinga maamuzi ya mkutano mkuu uliokuwa na
wanachama zaidi ya 1500 basi wafuate taratibu za kuwasilisha malalamiko
yao ni si kufanya vinginevyo.
Mwenyekiti wetu Yusuf Manji
alishasema tangu mapema ya kwamba yeye hatagombea tena na siku ya
mkutano aliyasema hayo awali, lakini Mjumbe wa Baraza wa Wadhamini mzee
Jabir Katundu aliwasilisha hoja ya kumuomba aendelee na uongozi, ndipo
wanachama walipopata nafasi ya kujadili chini ya Mama Karume na kwa
pamoja kuafiki Mwenyekiti aendelee japo kwa miaka minane "alisema
Akilamali.
Aidha Akilimali alisema Manji hakuafikiana na suala
hilo na ndipo alipoomba japo aongezewe muda wa mwaka mmoja kabla ya
kuelekea kwenye mikikimikiki ya Uchaguzi ili aweze kukamilisha baadhi ya
mambo kama ya usajili, ujio wa kocha mkuu mpya Marcio Maximo na ujenzi
wa Uwanja.
Naye mwenyekiti wa Baraza la Vijana Bw Bakili Makele
amesema wao kama vijana pia wanashangazwa hao baadhi ya wanachama ambao
wanataka kuirudisha Yanga nyuma, mara hii wameshasahau shuruba
tulizopitia mpaka kufikia muafaka, sisi kama vijana tunasema hatuamini
kama hao wanaosema hawakubaliani na maamuizi ya mkutano ni watu
wanaoitakia mema klabu yetu.
"Mwenyekiti
Bw Yusuf Manji hajayapenda madaraka na wala haitaji kuendelea kuiongoza
Yanga, bali kwa maombi yetu sisi wanachama pamoja na Baraza la
Wadhamini alikubali kuiongoza japo kwa mwaka mmoja kabla ya kuelekea
kwenye mkutano mkuu wa Uchaguzi ambapo atakayejiona ana uwezo wa
kuongoza Yanga basi atapata fursa hiyo ya kujinadi na si kupiga kelele
sasa hivi kweye vyombo vya habari" alisema Bakili.
BONDE FC NI MABINGWA WAPYA WA BEIRA YOUTH CUP 2012
-
Timu ya Bonde fc jana iliibuka kuwa mabingwa wapya wa BEIRA YOUTH CUP 2012
ubingwa huo umepatikana baada ya kuibuka na ushindi wa gili 5-4 dhidi ya
New Bo...
11 years ago
0 Weka maoni yako hapa:
Post a Comment
COMMENT HAPA