Jun 11, 2014

Wambura ashinda rufani, aruhusiwa kugombeaKamati ya rufani ya shirikisho la mpira wa miguu nchini TFF imemrudishia Michael Richard Wambura haki ya kugombea katika uchaguzi mkuu wa klabu hiyo hapo juni 29 mwaka huu.

Akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es salaam mwenyekiti wa kamati ya rufani ya shirikisho la mpira TFF, Mutabaazi Julius Lugaziya amesema kuwa maamuzi ya kamati ya uchaguzi ya Simba yalikuwa batili kwani Wambura alisimamishwa lakini bado alikuwa anafanya shughuri zote za ndani ya klabu kama mwanachama wa kawaida.

“Kamati ya rufani ya TFF imeamua kumrudishia Michael R. Wambura haki yake ya kimsingi ya kugombea kutokana na muwekewa pingamizu alikuwa anashirikishwa na klabu katika kila mikutano ya Simba ikiwemo kulipa ada ya uanachama na pia alikuwa ni mjumbe wa kamati kuu ya utendaji” Amesema Lugaziya ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya rufani TFF.

“Kama Wambura atasimamishwa katika uchaguzi huu basi hata kamati ya uchaguzi ya Simba itakuwa ni batiri kutokana na kamati hiyo kuchaguliwa na Wambura akiwa kama mjumbe wa kamati kuu ya utendaji” Ameongezea Lugaziya.

Wambura aliamua kukata rufaa katika kamati ya rufani ya TFF akiwa na hoja 14 zinazo pinga uamuzi wa bwana Damas Ndumbaro.

0 Weka maoni yako hapa:

Post a Comment

COMMENT HAPA