Aug 2, 2012

Mkataba wa Kocha Stewart Hall na Azam Wavunjwa


Klabu ya Azam FC inapenda kutoa taarifa kuwa mkataba wake na kocha Stewart John Hall kutoka nchini uingereza ulisitishwa rasmi jana Tarehe 31/07/2012 kwa makubaliano ya pande zote mbili.

Klabu ya Azam FC inajivunia mafanikio ya kocha Stewart Hall, na inampongeza kwa kazi nzuri aliyoifanya katika muda wote aliofanya kazi kama kocha mkuu na mkurugenzi wa ufundi.
 
Chini ya Stewart Hall, Azam FC ilifanikiwa kutwaa ubingwa wa Mapinduzi Cup, Kushika nafasi ya pili katika ligi kuu, Mashindano ya Urafiki na Kombe la kagame. Haya ni mafaniko ambayo hayajawahi kufikiwa na makocha wote waliotangulia na ni mafaniko ya kihistoria katika klabu ya Azam FC.
 
Azam FC inamtakia kocha Stewart Hall kila la heri, na inatarajia kuwa ipo siku katika siku za usoni kocha Stewart atarudi tena kufanya kazi na Azam FC.

Stewart Hall anaacha changamoto kubwa sana kwa mrithi wake ambaye atatangazwa hapo baadaye lakini kizuri ni kuwa, mrithi wa Stewart Hall atakuwa ni mwalimu anayefuata mfumo ule ule wa uchezaji ulioachwa na 

Stewart Hall kwani hiyo ndiyo (Playing Philosophy ya Azam FC)
Kwa sasa timu itakuwa chini ya Vivek Nagul na Kally Ongala
Imetolewa na Utawala
Azam FC

Wachezaji 21 Wateuliwa Kikosi Cha TAIFA STARS

Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen leo (Agosti 1 mwaka huu) ametangaza kikosi cha wachezaji 21 kwa ajili ya mechi ya kirafiki itakayochezwa ugenini Agosti 15 mwaka huu.

Wachezaji walioitwa Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager wanatakiwa kuripoti kambi kwenye hoteli ya Tansoma, Dar es Salaam, Agosti 8 mwaka huu saa 1 jioni tayari kwa mazoezi yatakayoanza siku inayofuata.

Makipa walioitwa kwenye kikosi hicho ni Deogratias Munishi (Azam), nahodha Juma Kaseja (Simba) na Mwadini Ali (Azam). Mabeki ni nahodha msaidizi Aggrey Morris (Azam), Erasto Nyoni (Azam), Kelvin Yondani (Yanga) na Shomari Kapombe (Simba).

Viungo ni Athuman Idd (Yanga), Frank Domayo (Yanga), Haruna Moshi (Simba), Mrisho Ngassa (Azam), Mwinyi Kazimoto (Simba), Ramadhan Chombo (Azam), Ramadhan Singano (Simba), Salum Abubakar (Azam) na Shabani Nditi (Mtibwa Sugar).
 
Wachezaji wanaounda safu ya ushambuliaji ni John Bocco (Azam), Mbwana Samata (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC), Said Bahanuzi (Yanga), Simon Msuva (Yanga) na Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC).

Jul 30, 2012

Ngassa kuuzwa Simba SC

Mshambuliaji wazamani wa Yanga aliyekuwa anaitumikia Azam FC amesajiliwa Simba SC kwa ajili ya msimu ujao wa ligi kuu ya Vodacom kwa uwamisho wa $50,000.

Kwa majibu wa taarifa iliyowekwa katika ukurasa wa Azam FC ndani ya Facebook inaeleza kuwa klabu hiyo imefikia uwamuzi huo baada ya Ngassa kuonesha dhamira ya kutotaka kuendelea kuitumikia klabu hiyo yenye maskani baada ya kunaswa anabusu logo ya wapinzani wa Simba.



"Klabu ya Azam FC inapenda kutoa taarifa rasmi kuwa baada ya baada ya mchezaji wetu Mrisho Ngasa kuonesha wazi kuwa na mapenzi na Yanga kwa kuivaa na kuipiga busu Logo ya Yanga, tuliwapa Yanga nafasi ya upedeleo ya kumnunua lakini hadi leo hakuna ofa iliyokuja toka Yanga. simba wametoa ofa na uongozi unatafakari ofa ya Simba
, Yanga.... Ngasa anauzwa $50,000 wadau wa Yanga tunajua mnampenda sana Ngasa... fikisheni ujumbe kwa uongozi wenu, " ili eleza taarifa hiyo ndani ya ukurasa wa Azam FC.


Ngassa ameitumikia Azam FC kwa misimu miwili ambapo ameweza kuwapa taji la Kombe la Mapinduzi mwaka 2012, kuwezesha Azam FC kushika nafasi ya pili katika ligi kuu ya Tanzania Bara msimu wa 2011/12 pamoja na Kagame Cup 2012 nafasi ya pili.


Ngassa amefanikiwa kuibika mfungaji bora wa ligi kuu Tanzania Bara katika msimu wake wa kwanza wa ligi kuu Tanzania kwa kuifungia Azam FC goli 16. 

Jul 27, 2012

YANGA YAICHAPA APR 1 -0, KUCHEZA NA AZAM FAINALI



Kikosi chaYoung Africans kilichocheza Nusu Fainali dhidi ya APR na kuibuka na ushindi wa bao 1-0






















Mabingwa watetezi wa kombe la klabu Bingwa Afrika Mashariki na kati, timu ya Young Africans Sports Club imefanikiwa kukata tiketi ya kucheza fainali ya mashindano hayo siku ya jumamosi, baada ya kuichapa APR kutoka Rwanda kwa bao 1- 0, katika mchezo mkali wa nusu fainali uliofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Mchezo huo ambao ulianza majira ya saa 10 kamili jioni, ulikuwa ni mkali na wa kuvutia muda wote wa mchezo, kitu kilichopelekea kumalizika kwa dakika 90 timu zote zikiwa sare ya kutofungana bao, hali iliyopelekea kunongezwa dakika 30 za muda wa ziada.

APR amabo waliingia uwanjani kwa nia ya kulipiza kisasi kwa Young Africans kufuatia kufungwa mabao 2-0 katika mchezo wa awali hatua ya makundi, waliuanza mchezo kwa kasi na kufanya mashambulizi ya kushitukiza, lakini umahiri wa mlinda mlango Ally Mustapha 'Barthez' ulikuwa kikwazo kwako.

Dakika ya 26 ya mchezo, Young Africans ilipata pigo baada ya mlinzi wake wa upande wa kulia Juma Abdul kukanyagwa vibaya mguuni na mchezaji wa APR Tuyizere Donatien hali iliyopelekea mchezaji huyo kutolewa nje na nafasi yake kuchukuliwa na Shamte Ally.

Kuona hivyo APR waliamua kupitia upande wa kulia wa Young Africans ambapo dakika ya 26 na dakika ya 38 Godfrey Taita na Shamte Ally walionyeshwa kadi za njano mwamuzi, kwa kuwachezea vibaya wachezaji wa APR.

Mpaka mpira unakwenda mapumziko, timu zote zilikuwa hazijafunagana zaidi ya kushambuliana kwa zamu. mwamuzi wa mchezo huo pia alishindwa kuumudu mchezo kwani alishinbdwa kuonyesha kadi kwa wachezaji wa APR kitu kilichofanya mashabiki kupiga kelele nyingi na kumzomea. 

Kipindi cha pili cha mchezo, Young Africans iilionekana kubadilika sana, kwani iliweza kumiliki vizuri mpira na sehemu ya kiungo, hali iliyowapelekea wachezaji wa APR wengi kurudi kukabia nyuma ya mstari wa katikakati.

Said Bahanunzi alikosa bao la wazi dakika ya 66, akishindwa kumalizia kazi nzuri iliyofanywa na Hamis Kiiza na Bahnunzi kushindwa kumchambua mlinda mlango wa APR Jean Claude Ndoli aliyepangua shuti lake na kuwa kona.

Young Africans iliendelea kukitawala kipindi cha pili, dakika ya 86 ilifanya mabadiliko ya kumtoa Shamte Ally na kumuingiza Rashid Gumbo ambaye aliongeza uhai katika nafasi ya kiungo.

Mpaka dakika 90 za mchezo zinamalizika timu zote zilikuwa sare ya kutofungana, Young Africans 0 - 0 APR.

Mwamuzi aliongeza dakika 30 za nyongeza, ambapo timu zote zilainza kusaka bao la mapema ili kuweza kuwasogeza hatua ya fainali, Mbuyu Twite alimchezea vibaya Rashid Gumbo lakini katika haliya kushangaza mwamuzi hakumpa kadi yoyote hali iliyopelekea wachezaji wa Young Africans kuja juu,

Hamis Kiiza'Diego' wa kwanza kulia akishangilia bao alilofunga katika mchezo dhidi ya APR, anayefuatia ni Godfrey Taita, Haruna Niyonzima na Rashid Gumbo




















Hamis Kiiza 'Diego' aliipatia Young Africans bao la kwanza na la ushindi katika dakika ya 100 ya mchezo akimalizia krosi safi iliyopigwa Haruna Niyonzima na Kiiza kufunga kwa bao hilo maridadi kwa kifua.

Kuona hivyo APR walianza kucheza mchezo wa kuwakwatua wachezaji wa Young Africans, hali iliyoleta majibizano na mwamuzi ambapo dakika ya 103, mwamuzi alimuonyesha kadi nyekundu mlinzi wa kulia wa Young Africans Godfrey Taita.

Mara baada ya kuona wako pungufu , Young Africans ilirudi nyuma kujipanga na kucheza mchezo wa kushitukiza huku ikilinda bao lake hilo.

Mpaka dakika 120 za mchezo zinamalizika, Young Africans iliibuka na ushindi wa bao 1-0 , hivyo kukata tiketi ya kucheza FAINALI na Azam FC siku ya jumamosi, fainali itakayofanyika majira ya saa 10 kamili jioini Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Saa 8 mchana kutakuwa na mchezo wa kusaka mshindi wa tatu kati ya APR na AS Vita.

Young Africans : 1.Barhtez, 2.J. Abdul/Shamte/Gumbo, 3.Oscar, 4.Cannavaro, 5.Yondani, 6.Chuji, 7.Taita , 8.Niyonzima, 9.Bahanunzi, 10.Kiiza, 11.Luhende

APR: 1.Ndoli, 2.Ngabo. 3.Tuyizere, 4.Twite, 5.Bagoole, 6.Iranzi, 7.Preus, 8.Mugiranenza, 9.Karekezi, 10.Wagaluka, 11.Ndikumana.

chanzo http://www.youngafricans.co.tz 

TFF, Benki Zasaini Udhamini Wa BancABC Super 8

Benki ya ABC imesaini mkataba wa miaka mitatu na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kudhamini michuano ya BancABC Super 8 inayoshirikisha timu nane, nne kutoka Tanzania Bara na nyingine nne kutoka Zanzibar.

Hafla ya utiaji saini imefanyika leo (Julai 26 mwaka huu) kwenye ofisi za TFF, Dar es Salaam ambapo Katibu Mkuu Angetile Osiah amesaini kwa niaba ya shirikisho wakati kwa upande wa ABC, saini yake iliwekwa na Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo kwa Tanzania, Boniface Nyoni.

Mashindano hayo yataanza Agosti 4-18 mwaka huu yakichezwa katika miji ya Dar es Salaam, Arusha, Mwanza na Zanzibar ambapo timu zote shiriki zitacheza katika vituo hivyo.

Uzinduzi rasmi wa mashindano hayo utafanywa Agosti 2 mwaka huu na Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa benki ya ABC yenye makao yake makuu nchini Botswana, na ina matawi katika nchi za Msumbiji, Zambia, Tanzania, Zimbabwe.

Katika uzinduzi huo, CEO ataelezea thamani ya mkataba huo ambapo utahusisha gharama za malazi, usafiri, vifaa na uendeshaji wa mashindano hayo.

Akizungumza baada ya kutia saini, Osiah amesema hatua hiyo ni sehemu ya mikakati ya TFF kuwa na mashindano mengi yatakayosaidia kuziandaa timu kabla ya kuanza Ligi Kuu.

Naye Nyoni amesema ABC imekubali kuingia kudhamini mpira wa miguu ikiwa ni lengo la kuchangia ustawi wa mchezo huo na kutoa sehemu ya faida wanayopata kwa kupitia michezo.

Timu zitakazoshiriki mashindano hayo ni zile zilizoshika nafasi tatu za juu katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara na Ligi Kuu ya Zanzibar. Nyingine ni timu iliyoshika nafasi ya kwanza kwenye Ligi 

Daraja la Kwanza Tanzania Bara na Ligi Daraja la Kwanza ya Zanzibar ambazo nazo kwa kushika nafasi hizo zimeshaingia katika Ligi Kuu.






Jul 26, 2012

NUSU FAINALI YA KAGAME NI LEO

Mashindano ya Kombe la Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati almaarufu Kombe la Kagame 2012, yamefikia hatua ya Nusu Fainali ambapo timu nne(4) zitachuana siku ya alhamis kusaka timu timu mbili ambazo zitacheza fainali siku ya jumamosi katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.


Mabingwa watetezi wa kombe hilo klabu ya Young Africans itashuka dimbani kucheza na tim ya APR kutoka Rwanda katika nusu fainali ya pili itakayofanyika jioni majira ya saa 10:00 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.

Nusu Fainali ya kwanza itaanza majira ya saa 8:00 mchana kwa kuzikutanisha timu za Azam FC (Tanzania) na timu ya AS Vita ya (DRC), timu ya Azam imefanikiwa kuingia hatua ya nusu fainali baada ya kuitoa timu ya Simba SC ya Tanzania pia kwa jumla ya mabao 3-1.

AS Vita nayo imefanikiwa kufika hatua hiyo ya nusu fainali baada ya kuifunga timu ya Atletico FC ya nchini Burundi kwa mabao 2-1 katika mchezo uliochzwa hapo awali.

Young Africans iimefanikiwa kufika hatua ya nusu fainali baada ya kuitoa timu ya Mafunzo ya Zanzibar kwa mikwaju ya penati 5-3, kufuatia kumalizika kwa dakika 90, ztimu zote zikiwa sare ya mabao 1-1.
APR kutoka Rwanda iliifinga timu ya URA kutok Uganda mabao 2-0 katika mchezo wa robo fainali na hivyo kupata tiketi ya kucheza hatua ya nusu fainali.

Kocha mkuu wa Young Africans Tom Saintfiet akiongea na tovuti ya klabu wwww.youngafricans.co.tz alisema anajua mchezo dhidi ya APR ni mgumu, kwani mchezo wa kwanza tulishinda kwa mabao 2-0, hivyo naamini APR wataingia Uwanjani wakiwa na nia ya kusaka ushindi tu ili waweze kucheza hatua ya fainali.

Saintfiet pia alisema pamoja na kuwa na mchezo huo mgumu dhidi ya APR, anaamin vijana wake wako katika hali nzuri ya ushindi, na maandalizi yote ya mchezo yamekamilika, hivyo anaamini timu yake Young Africans itaibuka na ushindi katika mchezo huo.

                                                                                                                       kikosi cha yanga kilichoifnga mafunzo kwenye hatua ya robo fainali 

Jul 25, 2012

AZAM FC YAITOA NISHAI SIMBA

Jana timu ya Azam ilizidi kuonesha ubora wake katika michuano ya Kagame baada ya kuifunga timu ya Simba jumla ya goli 3-1 

Magoli yote ya Azam fc yalitupiwa kimiani na mshambuliaji hatari wa timu hiyo John Bocco goli la kwanza ilikuwa dk 16, 46, 76,

Goli la kufutia machozi la Simba lilifungwa na Shomari Kapombe dk 64  kwa matokeo hayo timu ya Simba itakuwa imeaga michuano hiii.

Kwa matokeo haya sasa Azam fc itkutana na Vita Club ya Congo katika mchuano wa nusu fainali 

Michuano hiyo itaendelea tena kesho kwa mechi mbili za nusu fainali 

Mechi ya kwanza ni kati ya Azam fc vs Vita Club saa 8 mchana, na mechi ya pili itakuwa kati ya bingwa mtetezi Yanga dhidi ya APR mechi zote zitachezwa katika uwanja wa taifa

    Hawa ni baadhi ya mashabiki wa simba waliofika taifa hapo jana

      hawa ni mashabikiwa wa Azam Fc wakishangilia timu yao

      Wachezaji wa Azam wakishingila moja ya magoli hapo jana 
      Kikosi cha Azam fc kilichoifunga Simba jana

Kikosi cha Simba kilichofungwa na Azam jana 

picha kwa hisani ya BIN ZUBEIRY

Jul 24, 2012

YANGA YATINGA NUSU FAINALI, YAICHAPA MAFUNZO KWA PENATI 5-3

Kikosi cha Young Africans kilichoanza katika mchezo wa Robo Fainali dhidi ya Mafunzo,na kuitoa kwa kwa mikwaju ya penati 5-3















Africans Sports Club mabingwa watetezi wa kombe la Kagame, wamefanikiwa kutinga hatua ya nusu failnali mara baada ya kuifunga timu ya Mafunzo FC kutoka Zanzibar jumla ya penati 5-3, kufuatia kwenda sare ya kufungana bao 1 -1 katika dakika 90 za mchezo.

Mchezo huo uliofanyika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam ulianza majira ya saa 10 :00jioni ukiwa ni mchezo wa pili baada ya mchezo wa kwanza uliotanguliwa kati ya APR ya Rwanda iliyoifunga URA ya Uganda jumla ya mabao 2-1.

Mchezo ulianza kwa kasi toka dakika ya kwanza ya mchezo, kwa wachezaji wa timu zote kuonyesha umahiri wa kuumiliki mpira, na timu ya Mafunzo ilionekana kukamia mchezo huo kwani wachzaji wake walijituma sana kuhakikisha wanapata bao la mapema.

Mpaka dakika 30 za mchezo timu zote zilikuwa hazijafunagna, Mafunzo ilitumia mchezo wa kujaza viungo wengi katikati na kufanikiwa kuimiliki sehemu ya kiungo, kwani katika dakika ya 34, Mafunzo ilijipatia bao lake la kwanza kupitia kwa mfungaji All Othman Mmang aliyefunag kwa kichwa krosi iliyopigwa na kiungo wa timu hiyo.

Mpaka timu zinakwenda mapumziko, Mafunzo walikuw ambele kwa bao 1- 0.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi kwa Young Africans kufanya shambulizi la kushitukiza, ambapo katika dakika ya 46, Mshambuliaji Said Bahanunzi aliipatia Young Africans bao la kusawazisha kwa kichwa akiunganisha krosi ya beki wa kulia Juma Abdul.

Kuona hivyo Mafunzo waliamka na kuanza kulishambulia lango la Young Africans lakini umahiri wa walinzi wAA Young Africans ulikuwa kikwazo kwao kushindwa kumfikia mlinda mlango Yaw Berko.

Young Africans ilifanya mabadiliko ya kuwatoa Yaw Berko aliyeumia na nafasi kuchukuliwa na Ally Mustapha 'Barthez', Jeryson Tegete aliyechuku anafasi ya Rashid Gumbo na Idrisa Rashid aliyechukua nafasi ya Stephano Mwasika, mabadiliko ambayo hayakubadili matokeo.
Wachezaji wa timu zote, Young Africans na Mafunzo wakimpepea mchezaji Juma Othman Mmanga mara baada ya kuzimia, kabla ya kupata huduma ya kwanza na kuzinduka




















Dakika ya 80, mchezo ulismama kwa dakika zipatazo 5 kufuatia mchezaji wa Mafunzo Juma Mmanga kupoteza fahamu na wachezaji wa timu zote kuvua jzei zao na kuanza kumpepea, huku wengine wakiangua vilio kabla Daktari wa Young Africans Dr.Suphian Juma kwenda kumsaidia na kumzindua kisha kutolewa nje kwa machela na kwenda kupewa matibabu zaid katika gari la wagonjwa la dharula.

Mpaka dakika 90 za mchezo zinamalizika, Young Africans 1 - 1 Mafunzo, hatua iliyopelekea kupigwa kwa mikwaju ya penati.

Waliofunga penati kwa upande wa Young Africans ni: Said Bahanunzi, Nadir Haroub Cannavaro, Hamis Kiiza na Athuman Idd Chuji

Huku Mafunzo wakipata penati 3, huku Said Musa Shaban akitoa moja nje ya lango penati yake na Young Africans kufuzu hatua ya nusu fainali kwa jumla ya penati 5-3.

Kwa matokeo hayo, Young Africans itacheza na APR ya Rwanda katika mchezo wa NUSU FAINALI. 

Young Africans; Yaw Berko/Ally Mustafa, Juma Abdul, Oscar Joshua, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Athumani Iddi ‘Chuji’, Rashid Gumbo/Jeryson Tegete, Haruna Niyonzima, Said Bahanuzi, Hamisi Kiiza, Stephano Mwasika/Idrisa Rashid

Mafunzo FC; Khalid Mahadhi Hajji, Ismail Khamis Amour/Hajji Abdi Hassan, Said Mussa Shaaban, Salum Said Shebe, Ali Othman Mmanga, Juma Othman Mmanga/Sadik Habib Rajab, Suleiman Kassim ‘Selembe’, Jaku Juma Jaku, Mohamed Abdulrahim, Wahid Ibrahim/Kheir Salum Kheir na Ally Juma Hassan.
Haruna Niyonzima, Athuman Idd Chuji, Jeryson Tegete wakishangilia ushindi, mara baada ya Chuji kufunga penati ya mwisho na ya Ushindi
HABARI KWA HISANI YA MTANDAO WA YANGA SPORTS CLUB  http://www.youngafricans.co.tz

Jul 20, 2012

Robin van Persie safarini na Arsenal

Robin van Persie  
 
  The Emirates boss heads to Malaysia tomorrow and has thought about leaving Van Persie behind.

Yet that decision would virtually guarantee the Manchester City target will be leaving the club with Arsenal ready to listen to offers of £20million.

Club skipper Van Persie, who has one year left of his deal, only returned to training on Monday.
And he is due to face a Malaysia XI on Tuesday then play a friendly against City in Beijing a week today before Hong Kong two days later.

Insiders at Manchester United have ruled out a move, leaving the path clear for Etihad boss Roberto Mancini.

JEZI MPYA ZA UGENINI ZA MANCHESTER UNITED

WHITE HERE, WHITE NOW ... Rio Ferdinand models Manchester United's new away strip  
RIO FERDINAND AKIONYESHA UZI MPYA WA MAN U WA UGENINI

HATIMAE MASHABIKI WA MAN UNITED WATAKUWA WAKITANUA NA JEZI ZAO NYUPE PINDI TIMU YAO ITAKAPO KUWA INACHEZA UGENINI

MASHABIKI WENGI WA MAN UNITED WAMEONESHA KUFURAHISHO NA JINSI JEZI ZILIVYOTENGENEZWA 

Ryan Giggs, Wayne Rooney and Rio Ferdinand  
Ryan Giggs,  Wayne Rooney and  Rio Ferdinand
 

Kevin Yondan huru kuchezea YANGA

KIKAO cha Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji, kilichofanyika Julai 17, mwaka huu, kupitia mikataba na nyaraka zote zinazohusiana na mchezaji Kevin Yondani katika kujiridhisha juu ya hadhi yake ya usajili katika mashindano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame kimemhalalisha beki huyo wa kati kuchezea Yanga.
Taarifa ya Mwenyekiti Kamati hiyo ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), imesema;


1.   Kwa mujibu wa mapitio ya nyaraka zote zilizotajwa hapo juu na kufanyiwa upembuzi yakinifu, Kamati iliridhika pasi na shaka yoyote kuwa suala zima la mchezaji Kevin Yondani ni la kiutendaji, hivyo uamuzi wa Sekretarieti ya TFF kuwasiliana na Klabu ya Simba kwa suala hilo la kiutendaji  kama Sekretarieti  ilivyofanya katika barua yake ya Julai 14 mwaka huu ulikuwa sahihi.



2.   Kamati ilibaini kuwa Mkataba wa mchezaji Kevin Yondani na Klabu ya Simba ulimalizika Mei 31 mwaka huu. Hivyo kwa taratibu za usajili mchezaji Kevin Yondani kuanzia Juni 1 mwaka huu alikuwa ni mchezaji huru.



3.   Aidha Kamati ilibaini kuwa Mkataba uliowasilishwa na Klabu ya Simba TFF ukiwa na maana ya kuongeza mkataba uliokuwepo TFF baina ya mchezaji Kevin Yondani na Klabu ya 



Simba uliwasilishwa TFF, Juni 7 mwaka huu ambapo ni kinyume cha utaratibu wa kuongeza mikataba ya wachezaji unaozitaka klabu kuwasilisha mikataba ya kuongeza muda wa mikataba ya wachezaji wao wakati mkataba halisi haujaisha muda wake. Hivyo mkataba huo kwa jicho la kisheria haupo.



4.   Hata kama kamati ingeuona mkataba huo katika jicho la sheria, bado mkataba huo una tatizo la kisheria hasa katika tarehe ambazo pande mbili husika ziliingia makubaliano hayo. 



Ukiuangalia mkataba huo unabainisha kuwa, wakati mchezaji Kevin Yondani aliingia makubaliano Desemba 23 mwaka jana, upande wa pili wa kimkataba ambao ni Klabu ya 



Simba inaonekana iliingia makubaliano hayo kupitia kwa Makamu Mwenyekiti wake Geofrey Nyange Kaburu, Desemba 23 mwaka huu.



5.   Kisheria utata huu unaweza kuondolewa na pande husika tu kwa kurekebisha dosari hiyo 
kwa maridhiano kuweka saini katika mabadiliko hayo ili kuthibitisha mabadiliko hayo. Hivyo katika jicho la kisheria mkataba huo hauwezi kutumika kumzuia mchezaji huyo kwenda katika klabu anayoipenda wakati akiwa huru.


Kutokana na maelezo yote hapo juu, Kamati imeridhia hatua iliyochukuliwa na Sekretarieti ya TFF ya kumruhusu mchezaji Kevin Yondani kuichezea timu ya Yanga katika mashindano ya Kombe la Kagame 2012,”

     
KEVIN YONDANI AKIPEWA JEZI NA SEIF

Jul 19, 2012

WANAFUNZI WA MSUMBIJI, WATEMBELEA MAKA0 MAKUU YA KLABU YA YANGA


 

















Klabu ya Yanga imepongezwa kwa juhudi mbalimbali katika kuendeleza mchezo wa mpira wa miguu hapa nchini pamoja na harakati za uhuru wa Tanzania na Msumbiji.

Wakizungumza wakati wa ziara yao  wakati walipotembelea Makao Makuu ya Klabu ya Yanga Kiongozi wa msafara huo Florinda Mauribe kutoka Chuo cha Ualimu cha Ajuda do Dusenvolinmento do Povopara O 

Povo-Escola de Professones do Futuro-Chimdio, alisema wamejisikia furaha sana kufika makao makuu ya klabu ya Yanga, kuona mazingira ya klabu na kupewa historia fupi ya timu hii kongwe katika ukanda huu wa Afrika Mashariki.

Mauribe amesema Wananchi wa Msumbiji wanathamini mchango mkubwa wa ukombozi wa nchi yao kwa Tanzania ikiwemo Yanga ambapo wananchi hao wanayo taarifa kuwa baadhi ya Wapenzi na Mashabiki wa 

Yanga walitoa mchango wa hali na mali katika kusaidia harakati za ukombozi katika nchi hiyo ya Msumbiji.
Wanafunzi hao walitembezwa katika jengo la Makao Makuu ya Klabu ya Yanga na kujionea mambo mbalimbali ikiwemo Uwanja wa Kaunda unaotarajiwa kufanyiwa matengenezo,Gym ya mazoezi,Bwawa la kuogelea na Mtandao wa Klabu ya Yanga wa www.youngafricans.co.tz.
kwa hisani ya mtanadao wa Yanga sport club

Seattle Sounders 2 Chelsea 4


Eden Hazard
UP AND RUNNING ... Eden Hazard

EDEN HAZARD and Marko Marin netted on their debuts as Roberto Di Matteo's new-look Chelsea won in Seattle.

Belgian international Hazard showed just why the Blues paid £32million to sign him from Lille with an impressive first appearance in the playmaker’s role.

Winger Marin also weighed in with a goal following his £7m move from Werder Bremen, while young striker Romelu Lukaku bagged a double.

Di Matteo is ringing the changes after relying on the Chelsea old guard to win the Champions League and FA Cup last season.

And he could not fail to be impressed by his diminutive new signings — even if some of his team’s defending in their opening pre-season game left a lot to be desired.

The Italian said: “It’s a great start for them scoring in their first official game for the club and it was also good to see them striking up such an early understanding with their new team-mates.
Marko Marin is congratulated by Yossi Benayoun
NICE START ... Marko Marin is congratulated by Yossi Benayoun

“Hazard can have a real impact in the Premier League. He has great ability and quality and we’re seeing that every day in training.

“I’m really pleased with tonight’s game. We’ve got everything we were looking for from it.

“It was a good workout with good energy, we’ve integrated some new players and we’ve also seen some of the young talent that will be the future of this club.”

Even with just two of their starting line-up from the Champions League final on show, it looked as though this clash with MLS side Seattle was going to be ridiculously easy for the Blues.
Romelu Lukaku scored twice
AT THE DOUBLE ... Romelu Lukaku scored twice

They were ahead after only three minutes when Josh McEachran’s pass allowed Lukaku to shrug off Sounders defender Jeff Parke and beat keeper Bryan Meredith inside his near post.

And they doubled their lead in the 11th minute when Hazard’s shot struck John Hurtado and deflected beyond Meredith.

But Chelsea’s lack of fitness soon started to take its toll and Fredy Montero pulled a goal back for Seattle after intercepting McEachran’s ambitious ball across his own area.

The American side could even have been level but for Henrique Hilario’s flying save from Alvaro Fernandez midway through the first half.

With the enthusiastic backing of a 53,309 crowd at the CenturyLink Field, the home team took advantage of Chelsea’s reluctance to get stuck in on a dodgy pitch to snatch a 32nd-minute equaliser.
Frank Lampard signs autographs after the game
CROWD FAVOURITE ... Frank Lampard signs autographs after the game

Once again it was Montero who caused the damage, cutting inside John Obi Mikel’s half-hearted challenge to beat Hilario with a low shot into the far corner.

The Sounders defence, though, was always liable to implode and Chelsea regained the lead in the 40th minute when Marin scored with the help of another deflection off the hapless Parke.

And they confirmed their advantage a minute before the break courtesy of Lukaku, who struck again from Marin’s through-ball.

That was the signal for Di Matteo to make seven changes at half-time, with four more after 63 minutes to give his entire squad a run.

Kevin De Bruyne, also making his Chelsea debut, should have made it 5-2 but shot wide from Frank Lampard’s pass as the goals dried up after the break.

And with John Terry, Fernando Torres , Ashley Cole and Raul Meireles all due to join the squad in the next few days, Di Matteo will believe that things are slowly falling into place.
 
Chelsea: Hilario (Blackman HT); Chalobah (Hutchinson HT), Ivanovic (Kane 63), Luiz (Cahill HT), Ferreira (Saville 63mins), Mikel (Essien HT), McEachran (Lampard HT), Benayoun (Ramires HT), Hazard (Kakuta 63), Marin (De Bruyne HT), Lukaku (Piazon 63).

MAKALA MAALUMU YA SHOMARI KAPOMBE



KAPOMBE
Yatima aliyefunika tuzo za Taswa 2011 Dar
*Alikuwa muokota mipira Jamhuri Moro
Na Andrew Chale
 
USIKU wa kuamkia Juni 15, utabaki kuwa wa kihistoria kwa kiungo chipukizi wa Simba na timu ya soka ya Tanzania , Taifa Stars, Shomari  Salum Kapombe.

Ni usiku ambao Kapombe alimwaga machozi, baada ya kutangazwa kuwa mwanasoka bora wa 2011 wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (Taswa).

Usiku huo, mbali ya Kapombe kutwaa tuzo hiyo ya jumla, pia alibeba tuzo ya mwanasoka bora chipukizi wa mwaka huo kutokana na mchango mkubwa kwa timu yake ya Simba, akiwapiku Salum Aboubakar wa Azam FC.

Ni tuzo aliyostahili kutokana na mchango wake kwa timu yake ya Simba iliyomaliza msimu huo mabingwa wa Ligi Kuu ya Bara iliyofikia tamati Mei 6.

Wengi waliokuwepo kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam na waliokuwa kifuatikia kupitia luninga, walipigwa butwaa kuona Kapombe akilia.

Kilichowashangaza wengi, ni kuona chipukizi huyo akilia katika mazingira ya furaha, akiitwa mbele kwenda kupokea tuzo yake.

Wakati wengine hicho kilikuwa kipindi cha furaha kwa Kapombe ikawa kinyume chake, akiwa kwenye wakati mgumu akirejesha hisia zake kwa wazazi wake waliotangulia mbele za haki kama ilivyo kwa aliyekuwa rafiki yake mkubwa katika klabu ya Simba, Patrick Mafisango.

Kuhusu wazazi, Kapombe alifiwa na baba yake mzazi (Salum Kapombe) wakati yeye akiwa na umri wa miaka mitatu.
Hiyo ikamfanya kwa kiasi kikubwa kulelewa na mama yake mzazi (Ester 

Shomari), hivyo kukosa mapenzi ya baba.
Zaidi ya hapo, shujaa huyu akiwa na umri wa miaka 10, mama yake naye akafariki.

Hiyo ikamfanya Kapombe alelewe na ndugu zake, akiwemo bibi yake Hilda Emilian, aliyekuwa akiishi Mafiga, Morogoro.

Hata hivyo, Kapombe akiwa na umri wa miaka 14, bibi yake huyo mzaa mama, naye akafariki.

Hiyo ikamlazimu Kapombe kulelewa na dada zake, Halima na Aisha Kapombe; wote wakiwa watoto yatima.

Baada ya Kapombe kuyatafakari magumu aliyopitia katika maisha yake akiwa yatima na mafanikio mbali ya wazazi wake, Kapombe anasema, kingine kilichomfanya alie, ni kuyakumbuka maneno ya rafiki yake Patrick Mutesa Mafisango.

Anasema, Mafisango nyota wa kimataifa wa Rwanda aliyefariki Mei 17, alikuwa mtu wake wa karibu akimtia moyo, ajitume zaidi kusaka mafanikio.

“Nilipowakumbuka wazazi wangu waliofariki, ndipo nilipojisikia huzuni kubwa, kama wangekuwa hai, wangeshuhudia nikipata tuzo,” anasema Kapombe.

Kapombe aliyetua Simba msimu uliopita akitokea timu ya Polisi Morogoro, wakati huo ikiwa Ligi Daraja la Kwanza , anasema alipomkumbuka Mafisango, alishindwa kuvumilia.

“Mafisango alikuwa mtu wangu wa karibu, alikuwa msaada mkubwa kwangu, akinipa ushauri wa kujituma zaidi, ili nifanikiwe,” anasema Kapombe.

Hata hivyo, kuna kitu yawezekana si wengi wanaokijua, kilichowafanya Mafisango na Kapombe wawe marafiki zaidi wakiwa Simba; wote ni watoto yatima.

Kapombe anasema, Mafisango alikuwa akimtia moyo akimtaka ajitume na kutokata tamaa, ili afanikiwe huku akimtolea magumu aliyokuwa amepitia hadi anatua Simba.

Ingawa ni raia wa DR Congo , alibadili uraia wake na kuwa Mrwanda ili aweze kufanikiwa katika malengo yake ya soka.

Hata ubini Mafisango, si jina la baba yake mzazi, bali mkwe wake. Alifanya hivyo kupata urahisi wa kuishi Rwanda kwenye harakati za kusaka mafanikio ya soka.
 
TUZO YA TASWA
 
 
Kutokana na mchango wake mkubwa kwa timu yake ya Simba tena akiwa chipukizi wa umri wa miaka 18, Kapombe amekuwa gumzo kubwa ndani na nje ya Simba.

Mchango wake kwa Simba, ndio ukamshawishi aliyekuwa Kocha Mkuu wa timu ya soka ya Tanzania , Taifa Stars, Jan Poulsen kumwita.

Mechi ya kwanza kwa Kapombe akiwa Stars, ilikuwa mechi ya kuwania nafasi ya kupangwa kwenye makundi ya kusaka tiketi ya fainali za Kombe la Dunia za mwaka 2014.

Stars wakianzia ugenini Novemba 11, 2011, licha ya ugeni wake kwenye kikosi hicho, Kapombe  alipangwa kikosi cha kwanza.

Katika mechi hiyo ambayo iliisha kwa Stars kushinda 2-1, Kapombe alionesha uwezo mkubwa ambao umemwezesha kuwamo hadi sasa chini ya Kocha Kim Poulsen.

Vitu vyake vya uhakika akiwa na timu yake na Simba na Stars, vyote hivyo vimemfanya awe kivutio kwa kila mpenda maendeleo ya soka.

Kwa uwezo wake dimbani na mchango wake kwa Simba na Stars, hata jina lake lilipotajwa kama chipukizi bora, hakuna aliyeshangaa.

Aidha, hata jina lake lilipotajwa kuwa mshindi wa jumla wa Tuzo ya Mwanamichezo Bora wa Chama 
cha Waandishi wa Habari za Michezo (Taswa), hakuna aliyesema hakustahili.

AMETOKEA WAPI KISOKA

Kapombe anasema, alianza kupenda soka tangu akiwa na miaka mitano, wakati huo akicheza chandimu mtaani kwao Mafiga, Morogoro.
Anasema, timu yake ya kwanza ni Santos FC, iliyokuwa ikishiriki michuano mbalimbali, akipata nafasi ya kujifunza mengi ya soka.
Kati ya michuano aliyowahi kucheza akiwa na Santos FC, ni ‘Serve Access Game’ iliyokuwa ikiandaliwa na taasisi ya kuibua vipaji ya  Morogoro Youth Academy .
 
KUOKOTA MIPIRA UWANJANI
 
Mbali ya kucheza Santos FC, pia Kapombe alikuwa kwenye timu iliyokuwa ikiundwa na vijana waokota mipira kwenye uwanja wa Jamhuri, Morogoro iliyojulikana kwa jina la ‘Jamhuri Ball Boys FC.

“Nilipitia timu nyingi katika utoto wangu, Mafiga FC, Santos, Jamhuri Ball Boys, hadi nikaonwa na kituo cha Moro Youth Academy,” anasema Kapombe.

Anasema, kote alikopitia kisoka kwenye utoto wake, ndoto yake ilikuwa ni kufika mbali kisoka, hivyo kutwaa tuzo ya Taswa, ni mwanzo kwake.

“Nikiwa Ball Boys pale uwanja wa Jamhuri, nilikuwa na shauku kubwa ya kucheza timu kubwa kama 

 Mtibwa Sugar, Simba, Yanga na nyinginezo nilizokuwa naziona Jamhuri.
“Nilijipa moyo, nikiongeza juhudi zangu katika mazoezi kutimiza ndoto hizo, kweli zimeanza kutimia,” anasema Kapombe.

Akiwa na umri wa miaka 14, wakati huo akiichezea Ball Boys, alipewa uhahodha katika michuano ya WINOME Cup na Serve Access Games.

Baada ya kung’ara, ndipo akatwaliwa na kituo Moro Youth, hivyo kupata nafasi ya kujifunza mengi zaidi.
 
WALIOCHANGIA MAFANIKIO
 
Kapombe anamtaja Kocha Yahya Belin aliyemnoa katika timu ya Jamhuri Ball Boys, akisema alikuwa akimpa mbinu nyingi na kumtaka asichague namba.

“Kocha Belin, alinipa siri kucheza namba nyingi uwanjani ili kupangwa mara nyingi, pia kuweza kuhama namba moja hadi nyingine kulingana na mazingira ya mchezo kuisaidia timu.”

Kutokana na uwezo wake mkubwa kiuchezaji, licha ya kuwa na umri wa miaka 15, alipandishwa kikosi cha vijana wa umri wa chini ya miaka 17 cha kituo hicho.

Akiwa kwenye timu hiyo, ndipo alipoteuliwa kwenye kikosi cha mkoa cha vijana wa chini ya miaka 17, kilichoshiriki michuano ya Copa Coca Cola mwaka 2008, huko nako akiwa nahodha.

Anasema, katika mashindano hayo walitolewa hatua ya robo fainali na Kigoma ambayo ilikuja kuwa mabingwa.

Kapombe anasema, baada ya michuano
hiyo, yeye na  Zahor Zeirani kutoka kikosi cha Morogoro, waliteuliwa kwenye timu ya Coca Cola Dream Team iliyokwenda Brazil .

Lakini, yeye Kapombe hakuungana na Kombaini hiyo ya Dream Team kutokana na kuwa mgonjwa, hivyo akarudi Morogoro na kujiunga na timu ya Polisi Morogoro.

Anasema, alikuwa ni kati ya nyota sita kutoka Kombaini ya Morogoro waliokuwa wametwalia na Polisi Morogoro, hivyo akapata nafasi ya kuonesha kipaji chake.

Akiwa kikosi cha pili cha Polisi Morogoro, mwaka 2009, Kapombe alishiriki michuano ya vijana wa timu za Ligi Kuu ‘Uhai Cup.

Kutokana na uwezo wake mkubwa, Kapombe alipandishwa hadi kikosi cha kwanza cha timu hiyo, kilichokuwa kikishiriki Ligi Kuu Tanzania Bara.

“Nakumbuka kulikuwa na mechi kati yetu na timu moja ya Arusha, katika mechi ile, alikuwepo Kocha Jamhuri Kihwelo ‘Julio.’

“Aliridhishwa na uwezo wangu, akanieleza ningekuwemo kwenye kikosi cha timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 23, ndipo nilijiunga na kikosi hicho,” anasema.

Akiwa na U-23, Kapombe anasema alishiriki  kwenye hatua ya kuwania nafasi ya kucheza

Michuano ya All African Games na fainali za Olimpiki, akicheza mechi dhidi ya Cameroon , Nigeria na Uganda , hivyo kuzidi kupata uzoefu.
 
ALITUA VIPI SIMBA?

Anasema, Simba walimwona katika mechi ya kimataifa dhidi ya Cameroon kwenye uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam .

Anasema, baada ya filimbi ya mwisho, alifuatwa na viongozi wa Simba wakimtaka ajiunge nayo, naye hakusita kwani ni kitu ambacho hakuwa amekitaraji katika umri wa miaka 17.

“Naikumbuka mechi baina ya U-23 dhidi ya Cameroon , mchezo uliochezwa kwenye dimba la Taifa, siku hiyo viongozi wa Simba walinifuata na kunitaka nijiunge nayo,” anasema.

“Nikamshukuru Mungu, kwangu ulikuwa mwanzo wa safari ya mafanikio kisoka, anasema Kapombe.

Anasema, baada ya kutua Simba, mechi yake ya kwanza ilikuwa dhidi ya timu kutoka Uganda kwenye Simba Day, Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, jijini Arusha.

Anasema, wakiwa njiani kurejea jijini Dar es Salaam, aliyekuwa Kocha Mkuu wa timu hiyo, Moses Basena, akatangaza nyota 18 huku akimpa jezi namba 15 ya kikosi cha kwanza.

Anasema, mbali ya kupewa jezi, Basena alimsihi kucheza kwa kujiamini na mechi kubwa kwake ilikuwa mechi ya Ngao ya Hisani dhidi ya Yanga, akiingia kutokea benchi.

Kapombe anasema, anashukuru Mungu kumjalia uwezo kisoka kwani msimu wake wa kwanza akiwa Simba, ameweza kupangwa kikosi cha kwanza katika mechi zote.
 
KUITWA TAIFA STARS
 
“Siku nilipoitwa kwenye kikosi cha Stars, nilishangaa, kwa sababu naona kama ni mapema kwangu, lakini namshukuru Mungu,” anasema.
 
HISTORIA KWA UFUPI
 
Kapombe ni mtoto wa mwisho kwenye familia ya watoto watatu wa Mzee Salum Kapombe wa mjini Morogoro, aliyezaliwa Januari 28, 1992. Alipata elimu ya msingi katika shule ya Mwele, kuanzia 2000 hadi 2006 na baadaye elimu ya sekondari ya Lupanga.

Anasema, hiyo ni shule iliyo jirani na Chuo cha Ualimu Kigurunyembe, kuanzia 2007 hadi 2010.
 
SIFA ZA ZIADA
 
Amejaliwa uwezo wa kutumia miguu yote miwili, pia amekuwa akicheza namba zaidi ya moja ikiwemo kudaka.

Kapombe amekuwa akivutiwa na Haruna Moshi ‘Boban,’ akisema ndiye amekuwa akiiga uchezaji wake kwa hapa nchini.

Kimataifa, amekuwa akivutiwa na Tom Cleverley wa timu ya Manchester Utd ya England .
 
SHUKRANI
 
Anasema, hawezi kuwasahau makocha, wazazi wake na wengine wengi wakiwemo Catherine Ntevi, Godfrey Ngatimwa na Dennis Anthony kwani wamekuwa msaada mkubwa akiwa
jijini Dar es Salaam .

Aidha, anawashukuru makocha Belin, Allan Thigo na Rajabu Kindagule wa Moro Youth, John Tamba wa Polisi Morogoro, ‘Julio’, Moses Basena wa Simba Jan Poulsen aliyemwita mara ya kwanza Stars.
 
ASICHOKISAHAU
 
Kapombe anasema, katika maisha yake hatosahu walipokuwa safarini kuelekea mjini Younde , Cameroon , mwanzoni mwa mwaka huu.

Anasema, wakiwa angani, walikumbana na hali mbaya ya hewa hadi ndege kuanza kuyumba, hali ile ilimuweka kwenye wakati mgumu.

“Kwenye hali ile, wachezaji tulikuwa kwenye wakati mgumu sana , wengi wetu tulisema pengine ndiyo ulikuwa mwisho wa uhai wetu; hata hivyo tulifika salama,” anasema Kapombe.
                    
Mwisho
 
DONDOO MUHIMU;
 
JINA KAMILI: Shomari Salum Kapombe.
KUZALIWA: Januari 28, 1992.
MAHALI: Morogoro.
TIMU YA MTAANI: Santos Fc, Mafiga Kids
UTAIFA: Tanzania
ELIMU: Kidato cha nne
Mwandishi wa makala: 0719076376/chalefamily@yahoo.com
 
Mwisho

Jul 18, 2012

BAADA YA KUSHINDA KESI TERRY ANATANUA URENO

John Terry and wife Toni    
John Terry akiwa na mke wake Toni nchini Ureno wakitanua 

John Terry   
Terry akiwa katika boti ya kifahari nnchini Ureno 

vessel  
Hii ndio boti ya kifahari ambayao Terry na mke wake walikuwa wakitanua nayo Ureno 
katika mapumziko hayo JT alikuwa akitumia SHAMPEIN za  bei mbaya  zilizonunuliwa Hollywood club zaidi ya paund £13,000

MARIO BALOTELLI ANATANUA HISPANIA

Mario Balotelli                               Mchezaji wa Man city Mario Balotelli akiwa anavaa kaputula tayari kwa kula bata

 Mario Balotelli   
Vimwana fans wa Balotelli wakiwa wanagusa mwili wake kwa shahuku ya kukutana nae


Mario Balotelli 

Balotelli akiwa bechi na vimwana huko Spain katika mapumziko yake kabla ya kuanza msimu wa ligi


YANGA YAICHAPA WAU SALAAM 7-1-



Kikosi cha Young Africans Sports Club kilichoanza leo dhidi ya Waw Salaam




















Mabingwa watetezi wa kombe la Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (KAGAME) timu ya Young Africans Sports Club imeichapa bila huruma timu ya Wau Salaam ya Sudan mabao 7- 1 katika mchezo wa kundi wa C uliofanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Young Africans ilianza mchezo kwa kasisi na kucheza pasi za kuonana, kwa dakika kumi 10 za kwanza huku ikifanya mashabulizi ya kushitukiza na katika dakika ya 12 mshambuliaji Said Bahanunzi aliipatia Young 

Africans bao la kwanza kwa kichwa kufuatia kumalizia kazi nzuri iliyofanywa na kiungo Haruna Niyonzima.
Dakika ya 17 ya mchezo mshambuliaji  Said Bahanunzi aliipatia Young Africans bao la pili, mara baada ya kumalizia kazi nzuri iliyofanywa na Hamis Kiiza na mfungaji kufunga bila ajizi akiwa ndani ya eneo la penati.

Huku ikicheza soka safi nala kuvutia, Young Africans iliendelea kulishambulia lango la Wau Salaam na dakika moja baadae dakika ya 18, Hamis Kiiza aliipatia Young Africans bao la tatu. 

Ikicheza mbele ya viongozi wake wapya na mwenyekiti mpya wa Young Africans Yusuf Manji , Hamis Kiiza Diego aliipatia Young Africans bao la nne dakika ya 25, na dakika tano baadae dakika ya 30 kiiza tena aliipatia Young Africans bao tano.

Hamis Kiiza aliendelea kuwa mwiba kwa wasudan hao, kwani katika ya 35 ya mchezo aliipatia tena Young Africans bao la sita  akimalizia krosi safi ya Haruna Niyonzima aliyeonekana kuisumbua Waw Salaam sehemu ya kiungo

Mpaka mpira unakwenda mapumziko, Young Africans ilikuwa mbele kwa mabao 6- 0.
Kipindi cha pilik kilianza kwa Young Africans kufanya mabadiliko ambapo ilimpumzisha Kelvin Yondani na nafasi yake kuchukuliwa na Juma Seif Kijiko, Rashid Gumbo akachukua nafasi ya Haruna Niyonzima, na Idrisa Rashid alichukua nafasi ya Stephano Mwasika.

Mabadiliko hayo yaliipa uhai timu ya Wau Salaam kwani ilianza kulishambulia lango la Young Africans na kutawala kidogo eneo la kiungo, huku washambuliaji wa Young Africans Kiiza, Bahanunzi na Nizar Khalfan wakikosa mabao ya wazi kutokana na kutokua makini.

Nizar Khalfan aliipatia Young Africans bao la saba katika dakika ya 75 kufuati kumalizia krosi safi iliyopigwa na Idrisa Rashid.

Huku watazamaji wakianza kutoka uwanjani wakijua Young Africans imeshinda mbao 7-0, Wau Salaam wailipata bao la kufutia machozidakika ya 92 ya mchezo, kufuatia kutokua makini kwa walinzi wa Young Africans.

Mpaka dakika 90 za mchezo zinamalizika Young Africans iliibuka na ushindi wa mabao 7-1 dhidi ya Wau Salaam ya Sudan.

Young Africans iliwakilishwa na:
1.Berko, 2.Taita, 3.Oscar, 4.Cannavaro, 5.Yondan/Kijiko, 6.Chuji, 7.Nizar, 8.Niyonzima, 9.Bahanunzi, 10.Kiiza, 11.Mwasika/Idrisa

Young Africans itacheza tena mchwezo wake wa mwisho siku ya ijumaa dhifi ya vinara wa kundi C timu ya APR

Jul 17, 2012

KUUTOKA TAIFA YANGA YAONGOZA KWA GOLI 6-0 DHID YA WAW SALAAM


      
Timu ya yanga mpaka sasa inaongoza goli 6-0 dhidi ya waw salaam ikiwa ni dk 36 magoli ya yanga yamefungwa na


Said Bahanuzi DK 13: na DK 17



  Hamis Kiiza DK 19 ,30 ,35

  Stephano Mwasika DK 25:


CRDB Yashinda Tenda Ya Tiketi Za Elektroniki

Benki ya CRDB PLC imeibuka mshindi wa tenda ya kutengeneza tiketi za elektroniki za kuingilia uwanjani iliyotangazwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

Kampuni saba zilijitokeza katika hatua ya awali ya kuonesha nia (Expression of Interest) kwa ajili ya tenda hiyo ambapo Aprili 19 mwaka huu Kamati ya Mipango na Fedha ya TFF ambayo ndiyo Bodi ya Tenda ya shirikisho ilipitia maombi hayo na kupitisha nne kati ya hizo.

Baadaye kampuni hizo nne; CRDB Bank PLC, Prime Time Promotions, Punchlines (T) Limited na SKIDATA People Access Inc. zilitakiwa kuwasilisha rasmi tenda zao zikionesha jinsi zitakavyofanya shughuli hiyo pamoja na gharama ya utengenezaji kwa tiketi moja.

Bodi ya Tenda ya TFF ilikutana Julai 13 mwaka huu kwa ajili ya kupitia tenda hizo ambapo kampuni zote nne zilifanya uwasilishaji (presentation) wa jinsi zitakavyofanya shughuli hiyo, na baadaye kuipa kazi hiyo benki ya CRDB.

Uamuzi huo wa Bodi ya Tenda uliwasilishwa mbele ya Kamati ya Utendaji ya TFF. Kamati ya Utendaji ya TFF katika kikao chake kilichofanyika Julai 14 mwaka huu iliridhia uteuzi huo wa benki ya CRDB.

Baadhi ya vigezo ambavyo Bodi ya Tenda ya TFF iliangalia na kuipa CRDB tenda ni uwezo wa kufanya kazi hiyo (capacity), hadhi yake mbele ya jamii (credibility) katika shughuli inazofanya na teknolojia ya kisasa itakayotumika kutengeneza tiketi hizo.

Uamuzi wa TFF kutangaza tenda hizo ulilenga kuimarisha udhibiti wa mapato ya milangoni na kurahisisha mtiririko mzima wa washabiki kupata tiketi na kuingia viwanjani.

Rais wa TFF, Leodegar Tenga amesema: “Hatua hii ni muhimu sana, kwani tulikuwa tukiisubiri kwa muda mrefu. Si tu itaimarisha udhibiti wa mapato, bali pia itaondoa matatizo ya tiketi na kuendelea kujenga credibility (kuaminika) ya TFF. Mafanikio haya si kwa TFF pekee bali mpira wa miguu kwa ujumla.”

CRDB imeanza mara moja mchakato wa shughuli hiyo ambapo tiketi hizo zinatarajia kuanza kutumika rasmi katika kipindi cha kati ya miezi miwili na mitatu kuanzia sasa.