Jul 30, 2012

Ngassa kuuzwa Simba SC

Mshambuliaji wazamani wa Yanga aliyekuwa anaitumikia Azam FC amesajiliwa Simba SC kwa ajili ya msimu ujao wa ligi kuu ya Vodacom kwa uwamisho wa $50,000.

Kwa majibu wa taarifa iliyowekwa katika ukurasa wa Azam FC ndani ya Facebook inaeleza kuwa klabu hiyo imefikia uwamuzi huo baada ya Ngassa kuonesha dhamira ya kutotaka kuendelea kuitumikia klabu hiyo yenye maskani baada ya kunaswa anabusu logo ya wapinzani wa Simba."Klabu ya Azam FC inapenda kutoa taarifa rasmi kuwa baada ya baada ya mchezaji wetu Mrisho Ngasa kuonesha wazi kuwa na mapenzi na Yanga kwa kuivaa na kuipiga busu Logo ya Yanga, tuliwapa Yanga nafasi ya upedeleo ya kumnunua lakini hadi leo hakuna ofa iliyokuja toka Yanga. simba wametoa ofa na uongozi unatafakari ofa ya Simba
, Yanga.... Ngasa anauzwa $50,000 wadau wa Yanga tunajua mnampenda sana Ngasa... fikisheni ujumbe kwa uongozi wenu, " ili eleza taarifa hiyo ndani ya ukurasa wa Azam FC.


Ngassa ameitumikia Azam FC kwa misimu miwili ambapo ameweza kuwapa taji la Kombe la Mapinduzi mwaka 2012, kuwezesha Azam FC kushika nafasi ya pili katika ligi kuu ya Tanzania Bara msimu wa 2011/12 pamoja na Kagame Cup 2012 nafasi ya pili.


Ngassa amefanikiwa kuibika mfungaji bora wa ligi kuu Tanzania Bara katika msimu wake wa kwanza wa ligi kuu Tanzania kwa kuifungia Azam FC goli 16. 

0 Weka maoni yako hapa:

Post a Comment

COMMENT HAPA