
Kikosi cha Young Africans Sports Club kilichoanza leo dhidi ya Waw Salaam
Mabingwa
watetezi wa kombe la Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (KAGAME)
timu ya Young Africans Sports Club imeichapa bila huruma timu ya Wau
Salaam ya Sudan mabao 7- 1 katika mchezo wa kundi wa C uliofanyika
katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Young Africans ilianza mchezo kwa kasisi na kucheza pasi za kuonana,
kwa dakika kumi 10 za kwanza huku ikifanya mashabulizi ya kushitukiza na
katika dakika ya 12 mshambuliaji Said Bahanunzi aliipatia Young
Africans bao la kwanza kwa kichwa kufuatia kumalizia kazi nzuri
iliyofanywa na kiungo Haruna Niyonzima.
Dakika ya 17 ya mchezo
mshambuliaji Said Bahanunzi aliipatia Young Africans bao la pili, mara
baada ya kumalizia kazi nzuri iliyofanywa na Hamis Kiiza na mfungaji
kufunga bila ajizi akiwa ndani ya eneo la penati.
Huku ikicheza
soka safi nala kuvutia, Young Africans iliendelea kulishambulia lango la
Wau Salaam na dakika moja baadae dakika ya 18, Hamis Kiiza aliipatia
Young Africans bao la tatu.
Ikicheza mbele ya viongozi wake wapya
na mwenyekiti mpya wa Young Africans Yusuf Manji , Hamis Kiiza Diego
aliipatia Young Africans bao la nne dakika ya 25, na dakika tano baadae
dakika ya 30 kiiza tena aliipatia Young Africans bao tano.
Hamis
Kiiza aliendelea kuwa mwiba kwa wasudan hao, kwani katika ya 35 ya
mchezo aliipatia tena Young Africans bao la sita akimalizia krosi safi
ya Haruna Niyonzima aliyeonekana kuisumbua Waw Salaam sehemu ya kiungo
Mpaka mpira unakwenda mapumziko, Young Africans ilikuwa mbele kwa mabao 6- 0.
Kipindi
cha pilik kilianza kwa Young Africans kufanya mabadiliko ambapo
ilimpumzisha Kelvin Yondani na nafasi yake kuchukuliwa na Juma Seif
Kijiko, Rashid Gumbo akachukua nafasi ya Haruna Niyonzima, na Idrisa
Rashid alichukua nafasi ya Stephano Mwasika.
Mabadiliko hayo
yaliipa uhai timu ya Wau Salaam kwani ilianza kulishambulia lango la
Young Africans na kutawala kidogo eneo la kiungo, huku washambuliaji wa
Young Africans Kiiza, Bahanunzi na Nizar Khalfan wakikosa mabao ya wazi
kutokana na kutokua makini.
Nizar Khalfan aliipatia Young Africans bao la saba katika dakika ya 75 kufuati kumalizia krosi safi iliyopigwa na Idrisa Rashid.
Huku
watazamaji wakianza kutoka uwanjani wakijua Young Africans imeshinda
mbao 7-0, Wau Salaam wailipata bao la kufutia machozidakika ya 92 ya
mchezo, kufuatia kutokua makini kwa walinzi wa Young Africans.
Mpaka dakika 90 za mchezo zinamalizika Young Africans iliibuka na ushindi wa mabao 7-1 dhidi ya Wau Salaam ya Sudan.
Young Africans iliwakilishwa na:
1.Berko, 2.Taita, 3.Oscar, 4.Cannavaro, 5.Yondan/Kijiko, 6.Chuji, 7.Nizar, 8.Niyonzima, 9.Bahanunzi, 10.Kiiza, 11.Mwasika/Idrisa
0 Weka maoni yako hapa:
Post a Comment
COMMENT HAPA