AZAM TV KUONYESHA LIGI YA VODACOM LIVE
Azam TV imefanikiwa kupata haki ya kuonyesha michezo ya ligi kuu
Tanzania Bara moja kwa moja (live) inayo tazamiwa kuanza agosti 24 mwaka
huu.
Kwa
mujibu wa taarifa toka global publisher Azam TV itaonyesha michezo
isiopungua 60 Moja kwa moja (live) huku michezo 180 ikirushwa baada ya
kurikodiwa.
Taarifa
hizo zinaeleza kuwa Azam TV inayomilikiwa na kampuni ya Said Salim
Bakharesa wamiliki wa Azam FC inayoshiriki ligi kuu ya Tanzania Bara,
wameweka mezani kiasi cha Tsh bilioni 6.5 kwa shirikisho la soka
Tanzania (TFF) kwa ajili ya kupata haki hiyo ya Matangazo.
0 Weka maoni yako hapa:
Post a Comment
COMMENT HAPA