Wachezaji wa Young Africans wakiwa mazoezini leo asubuhi
Kiungo mshambuliaji wa timu ya Taifa Tanzania (Taifa Stars) Mrisho
Khalfani Ngassa ni miongoni mwa wachezaji walioanza mazoezi leo asubuhi
katika uwanja wa shule ya sekondari Loyola kwa ajili ya kujiandaa na
msimu mpya wa Ligi Kuu ya Vodacom 2013/2014 na mashindano ya kimataifa.
Yanga ambayo ilikuwa na mapumziko ya
zaidi ya wiki mbili tangu kuahirisha kushiriki mashindano ya Kagame
kufuatia serikali kuzizuia timu za tanzania kwenda kushiriki mashindano
hayo kufuatia kuwepo kwa hofu juu ya hali ya usalama katika mji wa
Darfur nchini Sudan.
Kocha
Mkuu Ernie Brandts aliyekuwa mapumzikoni nchini Uholanzi alirejea jana
na leo asubuhi ameongoza mazoezi ya asubuhi akishirikiana na kocha
msaidizi Fred Felix Minziro ambapo mazoezi yalikuwa mazuri na kuvutia
kwa wachezaji wageni.
Wachezaji
waliofanya mazoezi leo ni pamoja na kiungo mshambuliaji Mrisho Ngasa
aliesajiliwa msimu huu kama mchezaji huru akitokea tim ya Simba
alipokuwa kwa mkopo akitokea timu ya Azam FC.
Mshambuliaji
Shaban Kondo aliyejiunga na Yanga kama mchezaji huru akitokea nchini
Msumbiji amefanya mazoezi pamoja na wachezaji wengine wote wa klabu ya
Yanga ambao wataitumikia kwa ajili ya msimu mpya wa 2013/2014.
Kesho
Yanga itaendelea na mazoezi asubuhi katika uwanja wa Loyola ambapo
golikipa mpya alisejasiliwa kutokea klabu ya Azam Deogratius Munishi
'Dida' ataungana na wachezaji wengine katika mazoezi hayo ya kujiandaa
na msimu mpya wa 2013/2014.
Wachezaji waliofanya mazoezi leo ni:
Ally
Mustapha 'Barthez', Juma Abdul, Mbuyu Twite, Oscar Joshua, David
Luhende, Nadir Haroub 'Cannavaro', Salum Telela, Didier Kavumbagu,
Jerson Tegete, Abdallah Mnguli, Nizar Khalfani, Frank Domayo, Mrisho
Ngasa, Shaban Kondo.
Yanga
itaendelea na mazoezi na siku ya ijumaa itasafiri kuelekea kanda ya
ziwa kwa ajil ya kulitembeza kombe la Ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom
pamoja na kucheza michezo kadhaa ya kirafiki.
NB: Yanga haijatangaza usajili wake wa wachezaji wa msimu mpya wa 2013/2014.
Mrisho Ngasa (katikati) akiwa mazoezini leo asubuhi katika uwanja wa shule ya sekondari Loyola
CHANZO NA http://youngafricans.co.tz
0 Weka maoni yako hapa:
Post a Comment
COMMENT HAPA