CUF yaipa tano kambi ya upinzani Bungeni.
Chama
cha wananchi CUF kimesema kinaiunga mkono kambi ya upinzania Bungeni
kutokana na hatuwa walioichukua ya kukataa kujadili mswaada wa
marekebisho ya sheria ya mabadiliko ya katiba mpya ambao umesomwa kwenye
Bunge hilo mjini Dodoma kwa ajili ya kujadiliwa na wabunge ndani ya
bunge hilo hadi pale Zanzibar itakaposhirikishwa kikamilifu katika
mchako huo.
Kauli hio imesemwa
na mkurugenzi wa haki za Binadamu habari,uenezi na mawasiliano ya umma
Mh:Salim Bimani wakati alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi
huko ofisini kwake Vuga mjini Unguja.
Amesema kuwa jambo la
kusikitisha kamati maalumu ya katiba na sheria ya jamuhuri ya muungano
wa Tanzania ilifanya jitihada za kusikiliza maoni ya watu wengi sana
pamoja na asasi mbali mbali za kiraia lakini wote nikutoka upande wa
Tanzania Bara tu,kamati hio kwa makusudi ilifuta kabisa ratiba ya kuja
kukushanya maoni kwa upande wa Zanzibar ili kuwasikiliza wazanzibar nao
wanasemaje juu ya suala hili, lakini kutokana na kutoitakia mema
Zanzibar hawakufanya hivi wakati wanajua fika kuwa Zanzibar ni nchi
moja iliounda jamuhuri ya muungano wa Tanzania.
Alieza kwa
masikitiko makubwa wakati wabunge wa CUF wakitetea hoja hii ya kutaka
mswaada huu uondolewe ndani ya Bunge ambao umewasilishwa na Mbunge wa
Jimbo la Mkoani,Mkoa wa kusini Pemba Mh,Ali Khamis Seif na kuungwa mkono
kwa asilimia mia moja na chama cha CHADEMA,na NCCR Mageuzi,lakini cha
ajabu na chakushangaza wabunge wa CCM kutoka Zanzibar wakiongozwa na
Mbunge wa jimbo la Kitope Baloz Seif Ali Idi ambae ametoa barua kwa tume
hio kwa niaba ya wazanzibar kuwa wamekubaliana na mswaada huo tena bila
hata ya wazanzibar wenyewe kuulizwa juu ya suala hilo.
‘’Ni
wazi kabisa hawa jamaa hawana nia njema na nchi hii na kuna kila haja ya
kuwapinga kwa njia yoyote hile umeona wapi mtu asiekuwa na uchungu na
nchi yake kama si dalali wa nchi unadhani ninani’’alieleza Bwana Bimani.
Pamoja na hayo ametowa wito kwa wananchama wa CUF wote pamoja na
wazanzibar wanaoipenda nchi yao tena bila kubaguwana wawaunge mkono
wabunge wao pamoja na wale wote wnanoshirikiana kuitetea Zanzibar.