Sep 30, 2013

Kenya yaishangaa Marekani

                 

Kitendo hicho kilipokelewa kwa hisia tofauti na Serikali ya Kenya kwa kudai kwamba hatua hiyo iliyochukuliwa na Marekani  sio sahihi.   

Baada ya magaidi kuvamia kituo cha biashara cha Westgate nchini Kenya wiki iliyopita  ,Marekani imetoa onyo kwa raia wake kuacha kusafiri kuelekea nchini humo.
Kitendo hicho kilipokelewa kwa hisia tofauti na Serikali ya Kenya kwa kudai kwamba hatua hiyo iliyochukuliwa na Marekani  sio sahihi.
Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Kenya ililaani vikali hatua ya Marekani ya kuwaonya raia wake kufanya safari nchini Kenya.
Taarifa hiyo iliitaja hatua hiyo kuwa, haina umuhimu na pia ilitolewa katika wakati ambao sio mwafaka.
Ripoti hiyo iliongeza kuwa, shambulizi la Westgate jijini Nairobi, ni tatizo la ulimwengu mzima hasa kwa kuzingatia kuwa, hata Marekani yenyewe imekwishaathiriwa na vitendo kama hivyo vya kigaidi.

chanzo na mwananchi.co.tz

0 Weka maoni yako hapa:

Post a Comment

COMMENT HAPA