YANGA YAJIANDAA KUIKABILI RUVU SHOOTING
KIKOSI CHA YANGA
Young Africans imeendelea na mazoezi leo katika uwanja wa shule ya
sekondari Loyola-Mabibo kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom siku
ya jumaosi dhidi ya maafande wa Ruvu Shooting katika uwanja wa Taifa
jijini Dar es salaam.
Mchezo wa jumamosi ni muhimu kwa timu ya Young Africans kupata
ushindi ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kutetea ubingwa wake na
kupunguza tofauti ya pointi dhidi ya timu inayoongoza kwa tofauti ya
pointi 5.
Kocha Mkuu wa Yanga mholanzi Ernie Brandts ameendelea
kuyafanyia marekebisho makosa yaliyojitokeza katika michezo iliyopita
kwa lengo la kuhakikisha vijana wake wanakua makini na kuzitumia vizuri
nafasi wanazozipata.
Ikiwa imecheza mitano ikishinda mchezo mmoja,
sare michezo mitatu na kufungwa mchezo mmoja, Young Africans
imefanikiwa kukusanya pointii 6 na kufunga mabao 10 na kufungwa mabao 7.
Kikosi
kinatarajiwa kuingia kambini kesho katika hosteli za klabu kujiandaa na
mchezo huo wa jumamosi dhidi ya maafande wa Ruvu Shooting.
0 Weka maoni yako hapa:
Post a Comment
COMMENT HAPA