Oct 24, 2013

Hali ilivyokuwa wakati Simba ikilazimisha suluhu Tanga na Coastal Union










Coastal Union wamelazimishwa suluhu katika uwanja wa nyumbani wa Mkwakwani walipokutana na wekundu wa Msimbazi Simba.
Katika kipindi cha kwanza Simba walionekana kuelemewa kiasi golikipa wa timu hiyo Mganda Abel Dhaira alishindwa kustahamili mikiki ya Mganda mwenzake wa Coastal union, Yayo Kato ambaye alikuwa hampi nafasi. Hivyo Dhaira akasalimu amri dakika chache kabla ya kipindi cha kwanz akuisha na nafasi yake ikachukuliwa na golikipa namba mbili wa Simba Abuu Hashim.
Mpaka dakiak 45 za awali zinakwisha hakuna timu iliyoona lango la mwenzake lakini kwa namna Wagosi walivyokuwa wakishambulia kwa kasi walifurahi sana mwamuzi alipopuliza kipyenga kuashiria ni mapumziko.
Kipindi cha pili Simba walianza kwa kasi ambayo iliwatisha mashabiki wa Coastal, lakini haikudumu kwa muda mrefu mambo yakaanza kuwabadilikia.
Baada ya kuona hakuna mtu wa kutumbukiza mipira katikati, kocha wa Wagosi Joseph Lazaro, ambaye amechukua nafasi ya Hemed Moroco aliyeachia ngazi alimuingiza Uhuru Suleiman na kumtoa Danny Lyanga, halafu akamtoa Keneth Masumbuko na kumuingiza Pius Kasambale.
Mbali ya mabadiliko hayo bado uhaba wa mabao uliendelea kuiandama Coastal Union huku Simba wakiomba mchezo uishe kutokana na kuelemewa kila idara.
Katika hatua nyingine wana kidedea waliokuwa wakipiga ngoma walishikwa na bumbuwazi wasijue cha kufanya kutokana na ugumu wa mechi.
Simba ambao wametoka suluhu ya 3-3 na Simba Jumapili iliyopita hawakufurahishwa na suluhu ya leo mbali ya kuja na uongozi wote kuanzia Mwenyekiti Aden Range, Makamu Mwenyekiti Mzee Kinesi na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili Hanspope.
Kutokana na suluhu hiyo Wagosi wa Kaya wamevuna point 12, huku wakiendelea kushikilia nafasi ya 9 katika msimamo. Baada ya hapo watakabiliwa na mechi dhidi ya Mtibwa Sugar na Mgambo JKT zote zitachezwa Mkwakwani. Baada ya hapo watatoka nje kucheza na JKT Ruvu katika uwanja wa Chamazi jijini Dar es Salaam.
COASTAL UNION
23, OKTOBA 2013
TANGA, TANZANIA 

0 Weka maoni yako hapa:

Post a Comment

COMMENT HAPA