Nov 6, 2013

Exclusive: Hermy B aeleza sababu zilizopelekea Angel kuondolewa TPF6

Exclusive: Hermy B aeleza sababu zilizopelekea Angel kuondolewa TPF6

Jaji wa shindano la Tusker Project Fame 6 ambaye pia ni producer/sound engineer wa B’Hitz Music Group, Hermy B ameelezea sababu anazoamini zimepelekea kuondolewa kwa mshiriki wa Tanzania, Angella Karashani katika shindano hilo, hali iliyowavuruga akili na kuwaachia maswali mengi watazamaji hasa wa Tanzania walioamini kuwa Angel alipaswa kuwa mshindi ama kufika mbali zaidi.

Hermy B aliongea na tovuti hii exclusively na kutoa ushauri wake kwa Angel ambaye hivi sasa amerudi nyumbani Tanzania, pia kuhusu malalamiko ya baadhi ya watazamaji kuwa hakuwachagulia nyimbo nzuri washiriki wa shindano hilo wiki hii na kwamba ndio sababu ya wao kutoimba vizuri.

“Kitu cha kwanza..ndio, niliwapa watanzania matumaini, lakini matumaini ambayo niliwapa sikuwapa kwamba Angel akifanya vizuri atatoka, hapana. Angel alitakiwa afanye part yake yeye na Watanzania wangempigia kura,” amesema Hermy.

“Cha kusikitisha zaidi, mimi nilipata nafasi ya kufanya kazi na Angel wakati wa wiki yangu kama music director ambapo niliandaa show nzima ya wiki iliyopita, na nilifanya kazi na Angel. Surprisingly, Angel ana uwezo wa kuimba lakini alipokuwa kule ndani ya nyumba, Angel alikuwa mvivu..simpondi, au either alikuwa hajiamini, na mimi nafikiri sio uvivu lakini labda alikuwa hajiamini au alikuwa hajui uwezo wa sauti yake na uwezo wa kipaji chake.

Nilivyokuwa nafanya kazi mimi na Erick Wainaina, ilifikia point tulifukuza kila mtu ndani ya hall ya rehearsal tukabaki mimi, Wainaina na yeye, na aliweza kutoa sauti. Tulipofanya rehearsal mchana alitoa sauti."

Je! Hermy B anadhani Angel alitendewa haki kwa kuondolewa katika
mashindano hayo Jumamosi hii?

“Ile siwezi kusema kwamba ameonewa, ile kila mtu ameona kwamba Angel hakuimba vizuri, kama unatazama TV uliona kwamba hakuwa anafanya vizuri, kwa hiyo lile lilikuwa tatizo upande wake yeye, haikuwa tatizo upande wa judges na haikuwa ni tatizo upande wa watu wengine, yeye ndiye alikuwa ana shida. Kwa hiyo sio kwamba Angel ameonewa, Angel ametoka kwa haki kabisa, na haki ni kwa sababu hakuweza kutimiza wajibu ambao alitumwa mle ndani.”

Anaizungumziaje kauli ya Peter Msechu aliyewahi kuwa mshiriki wa TPF, kuwa
washiriki wa Tanzania mwaka huu hawajitumi sana na hawana njaa?

“Kwa upande wa Angel naweza kusema kwamba huenda Angel alikuwa hana njaa,
lakini kwa upande wa aliyebaki Hisia ana njaa. Hisia wimbo ambao nimempatia ni wimbo wa Adam Levine, ulikuwa unaitwa Payphone.

Ni wimbo mgumu kwa sababu ule wimbo, Adam ameuimba kwenye B flat, ambayo ni sauti ya juu sana na Hisia hakuweza, mpaka Hisia ameweza kuuimba tuliushusha mpaka kwenye G na Hisia ameweza kuperform ule wimbo.

Hisia ana njaa, kwa hiyo sidhani kama mawazo ya Peter Msechu yako sawa lakini kila mtu ana haki ya kufikiria kile anachotaka kufikiria kutokana na anavyoliona shindano jinsi lilivyo.”

Ni ipi nafasi ya Hisia kwa sasa katika shindano hilo ukilinganisha na washiriki wengine, Watanzania tuendelee kuwa na matumaini kuwa atashinda?

“Hilo ni tatizo letu jingine watanzania, tunakosaga matumaini hata kama bado tuna nafasi ya kushinda, Hisia ana uwezo wa kushinda. Kama Hisia nilimpa wimbo mgumu na akauimba vizuri, Hisia anauwezo wa kushinda, ni sisi tumsapoti.”

Kwa upande wa ushauri anaompa Angel katika career yake baada ya kuondolewa katika mashindano hao, Hermy amesema:

Angel anahitaji tu ku-recover kutoka kwenye makosa yake kama ameweza kugundua kwamba alikuwa ana makosa,anahitaji kuyatambua makosa yake na kuendelea mbele aachane nayo.

Asiwe mvivu, asi-holdback kitu alichonacho, asifiche alichonacho, nafikiri huku duniani atakuwa na uwezo wa kufanikiwa. Angel sio kwamba hajui kuimba, anajua kuimba sana yaani, sana..ni msanii mzuri. Kwa hiyo huku duniani ajifunze kupitia makosa yake. Arudi a-correct na afanye anachofanya. Na najua kwa sababu Angel anafahamu producers tofauti aangalie na opportunities zimekaa wapi na ziko vipi, asipoteze opportunity kama alivyopoteza,kwa sababu Angel ana uwezo wa kuimba.”

Kuhusu maoni ya watu kuwa wiki hii akiwa kama Music Director hakuwachagulia washiriki nyimbo nzuri, Hermy amesema:

Sidhani kama watu waliimba vibaya, nadhani kitu cha kwanza watu wanatakiwa wafahamu kuwa lile ni shindano, unapochagua nyimbo, humchagulii mtu wimbo
ambao anauimba bafuni kwake, hapana. Lile shindano ni kuonesha kipaji cha mtu, kwamba mtu anaweza kubadilika akaimba chochote kile.

Sidhani kama watu wameimba vibaya, nadhani wote wameimba vizuri, kwa sababu wamefanya kile ambacho wamejaribu kufanya, na kiukweli majaji walipata shida. Ukiangalia watu walioingia kwenye probation ni wawili tu ndio walikuwa wana haki ya kuingia kwenye probation.
wengine labda kwa sababu ambazo majaji wenyewe wanaweza kuwa wanazijua. Labda mkiwauliza wenyewe wanaweza wakawaambia.

Lakini watu wameimba vizuri, na ile imeonesha kwamba wale vijana wana vipaji, kwamba ukimpatia mtu wimbo wa reggae anauwezo wa kuiproject sauti yake  akaimba wimbo bila shida.”

chanzo na http://www.timesfm.co.tz

0 Weka maoni yako hapa:

Post a Comment

COMMENT HAPA