LIPUMBA AKUTANA NA NAIBU WAZIRI MKUU WA DENMARK NA KUJADILI UCHUMI
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
TAREHE 06/11/2013
PROF LIPUMBA AKUTANA NA NAIBU WAZIRI MKUU WA DENMARK: WAJADILI MATATIZO YA UCHUMI
.
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF Prof.Ibrahim Lipumba akutana na
Naibu waziri mkuu wa Dernmark Bi. Margrethe Vestager kujadili mambo
mbalimbali ikiwemo uchumi katika kikao kilichofanyika katika mji wa
Copenhagen nchini Denmark.
Katika mazungumzo hayo walijdaili
matatizo ya uchumi yanayokabila nchi za Ulaya hasa ukanda wa Euro
vinavyoathiri nchi za Afrika ikiwemo Tanzania na hatua za kuchukua.
Mambo mengine yaliyogubiga mzungumzo hayo ni pamoja na tatizo la ajira
kwa vijana ulimwenguni, Misaada ya Maendeleo kwa nchi maskini na ujenzi
wa uhusiano mzuri kati ya CUF na chama cha Radikale Venstre.
Bi. Margrethe Vestager ambaye ni kiongozi wa Chama cha Radikale Venstre
pia ni Naibu Waziri Mkuu katika Seikali ya Mseto ya Denmark
inayojumlisha vyama vitatu vya Social Democrats, Radicale Venstre na
Socialist People Party.
Majadiliano hayo yalifanyika wakati wa
ziara ya ujumbe wa CUF Denmark kwa mwaliko wa chama cha Radicale
Venstre.Ujumbe wa CUF ulijumuisha viongozi mbalimbali wa chama pamoja na
wanachama uliofanyika kuanzia terhe 26Oktoba 2013 mpaka 3 Novemba 2013.
Imetolewa na
Abdual Kambaya
Naibu Mkurugenzi wa Haki za binadamu ,sheria na Habari CUF
0 Weka maoni yako hapa:
Post a Comment
COMMENT HAPA