Nov 19, 2013

JULIUS S MTATIRO ATEMBELEA KITUO KIDOGO CHA ZIMA MOTO CHA MANISPAA YA HORSHOLM - DENMARK.

Kituo hiki kinahudumia raia 25,000 tu wa mji huu. Kina magari makubwa ya zima moto zaidi ya 10, kina helkopta kadhaa na magari madogo ya kutosha.

Hapa katika mji huu, ukipata tatizo lolote unabonyeza ALARM na wao ofisini kwao wanapata SIGNAL na wanajua exactly eneo ulilopo na watakuja ndani ya dakika 9 na wakichelewa watafika ndani ya dakika 14.

Wanatumika pia kusaidia ajali, wazee wenye umri mkubwa na wagonjwa. Mgonjwa pia hubonyeza tu ALARM na ndani ya dkk chache timu yao ya uokozi itafika.

Katika mji huu wanasema MTU HAFI BILA SABABU YA MAANA, maisha yanalindwa kuliko jambo lolote.

Kituo hiki cha zimamoto kwa ajili ya raia 25,000 tu kina vifaa na uwezo mkubwa wa kifanisi kuliko nguvu ya vituo vyote (kwa ujumla) vya zimamoto vya Tanzania ambavyo pia vinahudumia maisha ya watu milioni 42. 
Hizi picha za barabara, majengo n.k. Ni za mezani tu, wanazitumia kama MAFUNZO kwa wafanyazi wapya. 

 
 
  
 

0 Weka maoni yako hapa:

Post a Comment

COMMENT HAPA