Hassan Saleh Dilunga - mchezaji mpya wa Young Africans
Young Africans Sports Club almaraafu kama Yanga imefanikiwa
kumsaninisha mkataba wa miaka mitatu kiungo Hassan Saleh Dilunga kutoka
timu ya Ruvu Shooting ambapo mchezaji huyo ataanza kuitumikia timu yake
mpya katika mzunguko wa pili wa Ligi Kuu.
Usajili wa kiungo Hassan Dilunga unakua ni usajili wa pili kwa klabu
ya Young Africans katika kipindi cha dirisha dogo baada ya mwishoni mwa
wiki kukamilisha kumsajili mlinda mlango Juma Kaseja.
Mwenyekiti
wa kamati ya usajili wa klabu ya Young Africans Abdallah Bin Kleb
amesema usajili wa kiungo huyo ni utekelezaji wa maagizo ya kocha mkuu
Ernie Brandts aliyoyaacha pamoja na benchi lake la ufundi kwa ajili ya
kuboresha kikosi.
"Kocha aliacha
mapendekezo ya usajili tuyafanyie kazi la kwanza lilikuwa ni kuhakikisha
tunampata Juma Kaseja kwa ajili ya kuongeza nguvu katika nafasi ya
walinda mlango ambalo tulilikamilisha mwishoni mwa wiki na sasa
tumelimaliza la kiungo Hassan Dilunga" alisema Bin Kleb
Kikubwa
tunaendelea kuhakikisha kuwa maagizo yote yaliyopo katika ripoti ya
benchi la ufundi tunyafanyia kazi na kuyatekeleza ili kujiweka katika
mazingira mazuri ya kuboresha kikosi chetu kwa ajili ya mzunguko wa pili
wa Ligi Kuu na michuano ya Klabu Bingwa Afrika.
0 Weka maoni yako hapa:
Post a Comment
COMMENT HAPA