Na ANDREW CHALE, ARUSHA
WAAFRIKA wametakiwa kukataa utumwa na kuiga neno la ‘WOOD’, kwenye soko la filamu hasa
baada ya nchi nyingi kukopi jina la
‘HOLLYWOOD’ ambalo ni eneo lililopata umaarufu mkubwa kwenye soko la filamu
Duniani kwa kuwa na wasanii nyota na studio za kisasa, za masuala ya filamu.
Akielezea
mapema leo kwenye semina ya waandishi wa habari za
Sanaa kuhusu Filamu za Afrika, Mkurugenzi wa Tamasha la Filamu za
Kiafrika la Arusha (Arusha African Film Festival –AAFF 2013)
na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Arcadia, kilichopo
Pensylvania, Marekani , Mr. Akpor Otebele, alisema Waafrika waache
dhana ya kuendelea
kutumia jina hilo ambalo nchi nyingi wamekuwa wakitumia viunganishi vya
neon hilo la ‘Wood’ bila kujua maana hasa la kuendelea kulitumia.
Hii aina maana, ni la kuliacha na Nigeria kule waigizaji
wengi wanatafakari maana ya hili neon lakini jibu hakuna, lakini bado
wanaendelea kulitumia” alisema.
Akitolea mfano wa baadhi ya nchi zinazotumia jina hilo
kutoka Hollywood, ni pamoja na : Bongowood/ Swahiliwood (Tan zania), Nollywood
(Nigeria), Riverwood (Kenya), Ghollywood (Ghana), SierraWood (Sieralion)na
Congowood (Kongo) na mengine mengi.
Akpor Otebele
aliongeza kuwa, kuendelea kutumia viunganishi hivyo ni kuwanufaisha watu wa
Magharibi na kuupamba Mji wa Hollywood
unaoishi mastaa na studio maalufu huko Lose Angels nchini Marekani,
ambapo kwa dhana hii inafanya Waafrika kuwa watu wasiojua wanachokifanya.
…”Swahiliwood, its means, Swahili ubao? Is that sure? So why to use ‘Wood’?? in Swahili mean ‘UBAO’?? Alisema Akpor
Otebele.
Na kuongeza kuwa nchi
nyingi za Afrika zinatumia neno
'Wood' kinyume na maana yake
huku wengine wakipokea misaada bila kujijua kuwa wanarubuniwa ujinga. "Kwa
nini wanahitaji Bongowood. Mimi ninavyojua wood ni mbao, kwa nini wasiseme, swahili
movie?" alihoji.
Otebele aliwataka wanahabari kuwaelemisha wadau wa filamu kuwa, Hollywood
si jina la kutungwa bali la mji uliotokea kuwa maarufu kutokana na kusheheni
vitendea kazi bora na vya kisasa na kwenye makazi ya wasanii nyota mbali mbali, ni wakati wa
kulipinga.
Mbali na hilo, Otebele
aliwataka wasanii na waongoza filamu Afrika na kwingineko
kuzingatia filam,u za kiushindani
ilikufia malengo yao.
Hii ni kwa kuwataka
kuzingatia filamu zenye ubora, maarifa na zitoazo mafunzo mbele ya jamii
inayotuzunguka kila siku.
Katika
semina hiyo inayofanyika jini hapa, katika hoteli ya kisasa na
kitalii ya Silver Palm Hotel, ambapo mada mbali mbali zitawasilishwa
kuhusu tasnia ya filamu barani Afrika huku watoa mafunzo wengine wakiwemo Mtaalamu wa
filamu wa chuo kikuu Mlimani, ambaye pia ni mtayarishaji wa filamu ya ‘CHUNGU’,
Shule na Mtendaji Mkuu wa ZIFF, Prof. Martin Mhando.
Semina
hiyo ilianza mapema leo inatarajia kuendelea hadi Desemba Mosi, huku
ikiandaliwa na Waandaji wa Tamasha la
Kimataifa la Filamu za Nchi za Majahazi (Zanzibar International Films
Festival –ZIFF) kwa udhamini wa Mfuko wa kusaidia Vyombo vya
habari nchini (Tanzania Media Fund-TMF) ambapo
waandishi mbali mbali wanapatiwa mafunzo juu ya uandishi wa habari za
Sanaa hapa nchini kwenye vyombo vyao vya habari na mitandao ya kijamii zikiwemo
blogs.
Pia
semina hii inaendana na tamasha kubwa la filamu la AAFF 2013,
lililoanza Novemba 25 hadi Desemba Mosi, kwenye kumbi mbali mbali za
Alliance Francaise, Via Via , Mount Meru Hotel, Mango Tree & New
Arusha Hotel, ambapo kiingilio ni BURE/FREE ENTRY.
0 Weka maoni yako hapa:
Post a Comment
COMMENT HAPA