OKWI APIGWA STOP YANGA
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limesimamisha usajili wa
Emmanuel Okwi katika timu ya Yanga wakati likisubiri ufafanuzi kutoka
Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) kutokana na kuwepo na
kesi tatu zinazomhusu Okwi, moja ikiwa imefunguliwa na Simba kuidai
Etoile du Sahel malipo baada ya kumuuza mchezaji huyo,kesi ya pili ikiwa
ni ya Okwi aliyoishtaki timu hiyo kutokana na kutolipwa mshahara wakati
kesi ya tatu ikiwa imefunguliwa na Etoile ikimshtaki Okwi kwa utoro.
TFF imeusimamisha usajili huo wakati ikiwa imewasiliana na FIFA kutaka
kujua iwapo mchezaji huyo anaweza kucheza Ligi nchini Tanzania wakati
Etoile du Sahel ikiwa imefungua kesi katika shirikisho hilo la kimataifa
ikidai Okwi bado ni mchezaji wake.
0 Weka maoni yako hapa:
Post a Comment
COMMENT HAPA