Apr 29, 2014

UKAWA KUTORUDI BUNGENI ""MTATIRO"""

ANAYEDHANI TUTARUDI BUNGE LA KATIBA KWA UTARATIBU ULIOPO ACHUKUE JEMBE AKALIME;
 

Rais anasema turudi bungeni, CCM wanasema turudi pia.

Sisi tunasema kuwa hatutarudi bungeni isipokuwa tu ikiwa bunge maalum litaijadili rasimu iliyoletwa na tume ya mabadiliko ya katiba.

Kwa uhakika kabisa, hatuko tayari kujadili muundo ambao haujapendekezwa na wananchi.
Kama CCM wanaweza kuendelea kutunga katiba yao, waendelee, sisi hatutakwenda msituni kama John Komba, tutatumia njia zote za kidemokrasia kuendeleza madai ya matakwa ya wananchi. Hatutamwogopa mtu, tutasimama kidete na imara.

CCM pia wangefurahi sana kama vyama vyetu vingevurugana ili umoja wetu ukwame, tunawahakikishia kuwa safari hii wataula wa chuya, HATUVURUGANI NG'O! Tutasimama kidete kwa umoja wa hali ya juu kulinda maslahi na maoni ya wananchi.

Tuko tayari kukabiliana na machungu yote ya kidemokrasia, lakini hatutatetereka.

J. Mtatiro,
Katibu wa UKAWA.

0 Weka maoni yako hapa:

Post a Comment

COMMENT HAPA