Mar 8, 2012

Tunawatakia sikuu njema kina mama wote duniani

Blog yenu pendwa leo inaungana na Watanzania waote katika kuazimisha siku ya wanawake duniani pia inatumia nafasi hii kuwakumbusha wanawake kujituma kwa bidii katika kufikia malengo yao ili kuondokana na hali ya kuwa tegemezi katika jamii mfano wa kuingwa ni kwa wanawake wenye mafanikio katika sehemu zao kama mama  ASHA ROSE MINGILO  naibu katibu mkuu umoja wa mataifa na waziri wa ardhi na makazi mama ANNA TIBAIJUKA kwa jinsi wanavyojituma katika kazi zao   pia tunatoa wito kwa serikali kutilia mkazo vipaumbele  vya wanawake na kuondoa aina zote za unyanyasaji wa kijinsi dhidi yao.
Mama wajawazito wapewe huduma safi katika vituo vya afya na hospital zote na hili lisiwe kwa kusema tu bali kwa kulifuatilia na kuhakikisha kweli huduma hizo zinatolewa kama ilivyopangwa 
pia kuondoa haina zote za ubaguzi dhidi ya wanawake makazini na kupinga rushwa ya ngono na kuwe na usawa katika  utoaji wa ajira na wanawake wapewe kipaumbele katika nyanja zinazo husiana na malezi ya familia.kwani kwa kufanya hivyo jamii yetu itakuwa na maadili mema
 

0 Weka maoni yako hapa:

Post a Comment

COMMENT HAPA