Oct 22, 2012

Matokeo ya jana na msimamo wake Ligi Kuu Tanzania

Jana timu ya Simba ya Dar es salaam ilishindwa kufurukuta mbele ya Mgambo ya Tanga baada ya kulazimishwa droo ya bila kufungana.
Kwa matokeo hayo inakuwa ni mechi ya tatu mfululuzo kwa Simba kutoa droo na ni droo ya nne kwa timu hiyo msimu huu. 
Hali hii inawafanya mashabiki wake waanze kuwa na hofu dhidi ya timu yao kama itaweza kutetea ubingwa wake japo ndio inayoongoza ligi kwa sasa.
Nayo timu ya Prison jana iliibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Toto Afrika ya mjini Mwanza katika mchezo uliochezwa katika uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya.
Hali haikuwa nzuri pia kwa JKT Ruvu baada ya kushindwa kuutumia vyema uwanja wake wa nyumbani dhidi ya ndugu zao wa JKT Oljoro baada ya kulazimishwa droo ya goli 1-1.
Kwa matokeo hayo Simba inaendelea kubaki kileleni ikiwa na tofauti ya pointi 19 dhidi ya 17 za Azam ambayo inafuatia ila ikiwa na tofauti ya mechi mbili mkononi na Yanga yenye pointi 14 nyuma ya Azam ila imefungana na Oljoro.
  
Mgambo 0–0 Simba
Prison 1–0 Toto
Jkt Ruvu 1–1 Oljoro

0 Weka maoni yako hapa:

Post a Comment

COMMENT HAPA