Apr 24, 2013

Yondani azungumzia kuhusu kuondoka Yanga SC


 
 Kevin Yondani

 
BEKI kisiki wa kati wa Yanga, Kelvin Yondani, amesema kuwa kwa hivi hafikirii na hana mpango wa kuihama klabu hiyo yenye maskani yake mitaa ya Jangwani na Twiga jijini Dar es Salaam.

Nyota huyo alijiunga na klabu hiyo kwenye msimu huu wa Ligi Kuu Tanzania Bara akitokea Simba na kuiwezesha Yanga kutwaa Ubingwa wa Kombe la Kagame 2012.Akizungumza na Championi Jumatano, Yondani alisema bado ni mchezaji halali mwenye mkataba na Yanga, hivyo malengo yake hivi sasa ni kuhakikisha anaisaidia timu hiyo katika kutwaa ubingwa wa ligi na kwenye mashindano mbalimbali ya kimataifa na kitaifa.


Yondani alisema, anafurahi kuwepo kwenye timu bora na ambayo msimu ujao itashiriki michuano ya kimataifa.


“Kiukweli hivi sasa sifikirii kuihama Yanga na hakuna mpango wowote wa kuondoka, ninachoangalia ni jinsi gani nitaiwezesha timu yangu kuchukua ubingwa wa ligi.“Tofauti na ubingwa, pia ni katika mashindano ya kimataifa tutakayoshiriki hapo baadaye na kikubwa nataka kucheza kwa kujitoa kwa nguvu zote ili tushinde mechi inayofuata kwa ajili ya kujihakikishia ubingwa,” alisema Yondani.

Siku aliyokuwa anasaini mkataba na Yanga 

chanzo na http://www.globalpublishers.info

0 Weka maoni yako hapa:

Post a Comment

COMMENT HAPA