May 24, 2013

TAPELI MAARUFU JIJINI DAR LANASWA JIJINI


Kijana anayedaiwa kuwa tapeli akiwa mikononi mwa raia.
 Mtego huo ulifyatuka Jumanne ya Mei 21, mwaka huu ambapo kijana mmoja (jina halikupatikana) alinaswa na kupewa ‘henyahenya’ ya aina yake huku akinusurika kuchomwa moto.
Bila kujua kuna mtego, kijana huyo aliingia kwa mbwembwe katika Ukumbi wa Mango Garden, Kinondoni jijini Dar na kukaa katika moja ya viti kisha kuita mhudumu na kuchomoa noti ya shilingi ‘buku’ kumi, akaagiza misosi.
Akiwa amemeza tonge moja tu, aligeuka akatazama mlangoni, akamuona jamaa mmoja akimfuata kwa mwendo wa kasi na katika hali ya taharuki, ndipo akakurupuka akitaka kutoka nduki.

 
..Jamaa akiendelea kuhenyeshwa na wananchi.

ILIKUWAJE?
Majira ya saa 9:00 alasiri, ghafla kijana huyo aliibua tafrani alipokurupuka mbio kutoka nje ya ukumbi huo.
Nyuma ya kijana huyo, jamaa aliyekuwa amedaiwa kutapeliwa na mtu huyo alianza kumkimbiza akipiga kelele za mwizi ndipo baadhi ya raia nao wakaanza kumfukuzia
  
Baada ya kichapo jamaa alivishwa tairi tayari kupigwa kiberiti.

ATIWA MIKONONI
Raia hao walitimua mbio wakimfukuza kijana huyo na  walipofika maeneo ya Vijana, Kinondoni, kwa bahati mbaya alijikwaa na kuanguka ndipo akatiwa mikononi.
Yule jamaa ambaye alikuwa anamwitia mwizi, alikuja mbio na kuwaambia watu kuwa huyo ni tapeli ambaye alimtapeli shilingi laki tatu na nusu baada ya kumsomesha kuwa yeye ni mwajiri wa kampuni moja.
Aliyetapeliwa alidai kuwa katika utapeli huo, kijana huyo huwa anashirikiana na mzee mmoja ambaye huwa anavaa nguo nadhifu huku akiwa anatembea na  ‘briefcase’ mkononi.
 
Baadhi ya picha alizokutwa nazo tapeli huyo.

                                                       ‘ASACHIWA’
Jamaa huyo ‘aliposachiwa’ alikutwa na vitu kibao vya kitapeli yakiwemo makaratasi yaliyokatwa na kufungwa kwa noti bandia za shilingi elfu kumi zinazoonekana kama burungutu la fedha kumbe hakuna chochote ni ‘bosheni’.

Pia alikutwa na vitambulisho kibao vya watu vikiwemo vya kupigia kura, leseni na picha za ‘passport size’ za watu mbalimbali.
Katika makabrasha yake kulikutwa barua mbalimbali za serikali za mitaa za jijini Dar.
Alipoulizwa kuwa vitu hivyo vya watu na nyaraka za serikali ni vya nini au alivipataje, jamaa huyo alijitetea kuwa ana mtu anayeshirikiana naye katika michongo hiyo.


 

Baadhi ya vitambulisho alivyokutwa navyo tapeli huyo.


CHANZO NA     http://www.globalpublishers.info

0 Weka maoni yako hapa:

Post a Comment

COMMENT HAPA