Naibu spika J. Ndugai ametoa amri Mbowe atolewe nje baada ya Mbowe
kuomba muongozo ila Job Ndugai akamuamuru akae chini na asiongee
chochote ndipo Mbowe akakataa kukaa mpaka asikilizwe anachotaka kusema.
Wabunge wa upinzani wamegoma Mbowe kutolewa nje na kinachoendelea ni kupigana kati ya askari na wabunge wa CHADEMA.
Vurugu kubwa zilizotokea Bungeni muda
huu ambapo askari wa Bunge walikuwa wakivutana na Wabunge wa kambi ya
upinzani waliokuwa wakipinga amri ya Naibu Spika ya kumtoa nje kiongozi
wa kambi ya upinzania Bungeni, Mhe. Freeman Mbowe.
Vurugu kubwa zimetokea Bungeni hivi
sasa mara baada ya Naibu Spika kutoa amri ya kutolewa nje kwa kiongozi
wa kambi ya upinzania Bungeni Freeman Mbowe ambapo wabunge wa kambi ya
upinzani hawakukubaliana na amri hiyo.
Chanzo cha kutolewa kwa amri hiyo ni
kutokana na Mbunge wa Hai Freeman Mbowe kusimama na kuanza kuzungumza
pasipo kupewa ruhusa ili apinge uamuzi wa kura zilizopigwa na Wabunge
ambapo Bunge lilipiga kura ya kuuondoa mjadala wa mswada wa katiba au
ubaki ambapo wabunge 56 walisema mjadala huo uondolewe na Wabunge 159
walisema mjadala huo uendelee kwani ulishapita kwenye hatua mbalimbali.
Mara baada ya zoezi la upigaji kura
kuisha Naibu Spika Job Ndugai aliendelea na utaratibu wa Bunge ambapo
alimsimamisha Mhe. Mrema achangie mjadala na wakati huo huo Mhe. Mbowe
naye alisimama kupinga uamuzi wa Naibu Spika na ndipo alipotoa amri kwa
askari wa Bungeni wamtoe nje ya ukumbi wa Bunge na walifanikiwa kumtoa
nje mara baada ya mvutano mkali kati ya Wabunge wa kambi ya upinzania
dhidi ya polisi.
BONDE FC NI MABINGWA WAPYA WA BEIRA YOUTH CUP 2012
-
Timu ya Bonde fc jana iliibuka kuwa mabingwa wapya wa BEIRA YOUTH CUP
2012 ubingwa huo umepatikana baada ya kuibuka na ushindi wa gili 5-4 dhidi
ya New B...
12 years ago