Mtatiro: Operesheni ya kusaka wahamiaji haramu imejaa unyamaa
1. Mtangazaji nguli na mmiliki wa kituo cha redio FADECO ya Karagwe
Ndugu. Sekiku amenyang’ anywa pasi yake ya kusafiriwa na kuwekwa katika
kifungo cha ndani ya nyumba yake, haruhusiwi kutoka.( redio yake imekuwa
na msimamo imara katika kutetea maslahi ya wananchi kuliko kuwabeba
watawala- nadhani sasa analipiziwa kisasi)
2. Diwani wa CUF huko Tunduru amevamiwa na wanajeshi hao wakidai ana
pembe za ndovu, wakasachi nyumba nzima bila kupata chochote kibaya,
badala ya kumwachia wamempiga usiku kucha na kumshikilia kwenye kambi
maalum siku 2, kisha ati ndo wamemfikisha mahakamani.
3. Kijana mmoja huko Ulanga ameuawa kinyama na askari hao, mwenzie
amepigwa sana na melazwa St Francis Ifakara, huyu alopigwa eti kosa lake
ni kumiliki nyumba ya kifahari na gari aina ya Noah, askari wamempiga
akizimia mara tatu. Wanamlazimisha akiri ati amejenga nyumba yake kwa
biashara za ujangili.
4. Katika wilaya za Kondoa, Kilwa na Kilindi, wananchi wanavamiwa na
wanajeshi na askari wanyamapori na polisi, wanapigwa mno, wengi
hawaelewi kwa nini oparesheni hii ya kinyama inafanyika.
Haya na mengi yanafanyika kuhu serikali ikiwa kimya kabisa, inaona ni
matendo ya kawaida sana. Hakuna anayechukua hatua kutokomeza vitendo
hivi. Haiwezekani miaka 50 baada ya uhuru majeshi ambayo yanalipwa kodi
za masikini yanatumiwa kuwapiga, kuwatweza, kuwadhalilisha nakuwaumiza
raia wasio na hatia.
Watanzania waliichagua serikali ya CCM wakitaka maendeleo, si
kuvunjiwa haki na utu namna hii. Nchi yetu imepoteza kabisa misingi ya
utu na haki. Kama viongozi walioko serikalini wamekaa kimya haya
yakiendelea, raia wa kawaida wafanye nini?
Binafsi huwa naguswa sana na matukio ya uvunjwaji wa haki za
binadamu. Nimewapigia wakuu wa mikoa kadhaa, wakuu wa polisi kadhaa na
hata kuongea na baadhi ya mawaziri. Kila mmoja anajidai hajui tatizo
hili au liko nje ya uwezo wake? Hivi taifa hili linakwenda mbele au
linarudi nyuma?
Natoa wito kwa wananchi wote kusimama kidete na kutumia nguvu zote
zinazohitajika kusimamisha unyama huu. Kama pana watu wanahisiwa ni
majangili waplekwe mahakamani ili haki itendeke. Kwa nini wapigwe hadi
kufa au kuachiwa ?
chanzo na
http://cuftz.com/
0 Weka maoni yako hapa:
Post a Comment
COMMENT HAPA