Nov 28, 2013

Kitale: nimejifunza mengi kwenye kifo cha Sharo Milionea, nimeacha ujumbe kwa mama yangu nikifa yasijirudie kwangu

Kitale: nimejifunza mengi kwenye kifo cha Sharo Milionea, nimeacha ujumbe kwa mama yangu nikifa yasijirudie kwangu

Muigizaji na mwimbaji nchini Kitale yuko Tanga alipoenda kuhudhuria Dua ya kumuombea marehemu Sharo Milionea ikiwa ni mwaka mmoja tangu afariki dunia kwa ajali mbaya ya gari.

Kitale ambaye ndiye msanii pekee aliyefika Tanga siku ya jana amesema kuwa amejifunza mambo mengi katika msiba wa rafiki yake Sharo Milionea, ikiwa ni pamoja na misiba ya wasanii wengine waliotangulia mbele ya haki, Kanumba na Sajuki.

Akiongea kwa njia ya simu na Edson Mkisi katika kipindi cha Hatua Tatu cha 100.5 Times Fm, Kitale amesema kutokana na funzo alilopata ameampa ujumbe mama yake ili kwamba pindi atakapotangulia mbele ya haki mambo hayo yasijirudie kwake.

“Nimejifunza vitu vingi na nimejua marafiki walio wema na marafiki wasio wema. Ina maana kwamba kuna marafiki wanafiki na marafiki wasio wanafiki. Amesema Kitale.

“Kuna vitu vingi nimejifunza baada ya kuondoka marehemu Steven Kanumba, nimejifunza baada ya kifo cha Sharo Milionea, na nimejifunza baada ya kifo cha Sajuki. Nimejifunza vitu vingi sana sana sana.” Amesisitiza.

 “Ina maana hata mimi kama ntatangulia kuna mambo ambayo nimeshamweleza mama yangu na nimeshaieleza familia yangu, nafikiri hakitakuja kutokea kama kilichotokea kwa wenzangu. Nimejifunza vitu vingi hasa ukiwa msanii...” Kitale ameiambia Hatua Tatu.

Hata hivyo Kitale alikataa kueleza ujumbe huo na kudai kuwa ni siri kati yake na familia yake kwa kuwa hafahamu nani atatangulia kati yake na wazazi wake.

Kitale amewashauri wasanii kumkumbuka Mungu wakati wanapoendelea na shughuli zao na ndio sababu watu wengi wanaamini kuwa asilimia kubwa ya wasanii ni ‘Freemason’, na kwamba hiyo inatokana na kitendo cha wasanii hao kumsahamu Mungu wao.

Siku kama ya leo mwaka uliopita (November 27,2012) ndio siku ambayo marehemu Sharo Milionea alizikwa huko Tanga.

Apumzike kwa Amani.

0 Weka maoni yako hapa:

Post a Comment

COMMENT HAPA