Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Chadema, John Mnyika ambaye amedai, “Waraka utakaotumika katika mashtaka yao siyo huo. Sisi tutautumia ule ambao uliwasilishwa katika Kamati Kuu ambao una mambo makubwa na mengi zaidi kuliko huo unaochapishwa sehemu mbalimbali, ikibidi tutautoa huo waraka halisi,” alisema. Picha na Maktaba
Dar na Arusha. Utata mkubwa umeibuka kuhusu
waraka halisi wa ‘Mkakati wa Mabadiliko 2013’ uliosababisha Zitto Kabwe
kuvuliwa wadhifa wake wa Naibu Katibu Mkuu wa Chadema na kikao cha
Kamati Kuu ya chama hicho kilichofanyika Novemba 20 - 22, mwaka huu.
Baada ya juzi, Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa
Chadema, John Mnyika kuwaeleza wanahabari kuwa waraka uliochapishwa
katika magazeti na mitandao ya kijamii, siyo halisi, aliyekuwa
Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba amejitokeza na
kuutetea huku akidai kwamba huo unaodaiwa na uongozi kuwa ndiyo halisi
umeghushiwa.
Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini
(Chadema), alivuliwa uongozi pamoja na aliyekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu,
Dk Kitila Mkumbo na Mwigamba kutokana na madai ya kuandaa waraka huo
ambao Chadema kimesema ulikuwa unaeleza mbinu za uasi za viongozi hao
ambazo zingetumika wakati wa uchaguzi mkuu wa ndani wa chama hicho jambo
ambalo ni kinyume na katiba, sheria na itifaki zake.
Katika tamko alilotoa jana, Mwigamba alidai kwamba
kuna njama zinazofanywa na baadhi ya viongozi wa
Chadema ili kuubadili waraka halisi wa ‘Mkakati wa Mabadiliko 2013’ kwa
lengo la kupoteza maana yake, huku akisisitiza kuwa waraka halisi hauna
tatizo lolote.
Katika madai yake, Mnyika alisema waraka huo
unaosambazwa na kuchapishwa, si ule uliowasilishwa na kujadiliwa katika
kikao cha Kamati Kuu na kuahidi kuutoa waraka halisi ambao una mambo
makubwa na mengi zaidi.
“Waraka utakaotumika katika mashtaka yao siyo huo.
Sisi tutautumia ule ambao uliwasilishwa katika Kamati Kuu ambao una
mambo makubwa na mengi zaidi kuliko huo unaochapishwa sehemu mbalimbali,
ikibidi tutautoa huo waraka halisi,” alisema.
Hata hivyo, jana Mwigamba alisema waraka halisi ni
ule ambao upo katika kompyuta mpakato (Laptop) aliyonyang’anywa na
wanachama wa Chadema, Oktoba 25, mwaka huu, katika mkutano mjini Arusha.
“Waraka uliosambazwa kwenye vyombo mbalimbali vya
habari na mitandao ya kijamii ni sahihi neno kwa neno kama nilivyousoma
katika magazeti ya jana (juzi), pamoja na nakala iliyopo katika mtandao
wa kijamii wa Jamii Forums.”
Aliongeza: “Ili kuthibitisha kwamba waraka ule
ndiyo wenyewe, nawatumieni ‘soft copy’ kutoka kwenye kompyuta yangu
kwani waraka huo uliibwa kutoka katika kompyuta hiyo ambayo
nilirudishiwa baada ya wao kuikagua na kukuta waraka huo halisi.”
Mwigamba alisema waraka wake unatofautiana kwa
kiasi kikubwa na ule ambao Chadema kinasema kuwa ndiyo halisi: “Lissu na
wenzake wana mpango wa kuuchakachua waraka huu, lakini wamekwama.”
Alisema kuandaa waraka huo siyo uhaini kama
ambavyo imekuwa ikielezwa na viongozi wa Chadema na kusisitiza kuwa ni
waraka wa kusaka ushindi katika uchaguzi halali ndani ya chama hicho
uliopangwa kufanyika Desemba mwaka huu na baadaye kusogezwa hadi Juni
mwakani.
“Wakati wa uchaguzi si ajabu kuwepo kwa wanachama wanaounga
mkono wagombea tofauti. Nimekuwa karibu na Mwenyekiti wa Chadema,
Freeman Mbowe kwa miaka mingi, najua hata yeye ana mikakati na
wanaoshiriki mkakati wake ni Lissu na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless
Lema,” alisema.
Alisema anashangazwa kwa kitendo cha Chadema
kuusambaza waraka huo, wakati ulikuwa ni mpango wa siri kati yake, Dk
Kitila pamoja na mtu mwingine anayetajwa kwa jina la M2.
“Baada ya kugundua madhara ya kusambaza ovyo
waraka huo, sasa wameamua kuukana, waraka wangu ni sahihi na unaeleza
ukweli. Binafsi nimefanya kazi ofisi ya makao makuu ya chama kama
Mhasibu Mkuu ningeweza kuanika mengi lakini sijafanya hivyo kwa masilahi
ya chama,” alisema na kuongeza:
“Tunatambua kwamba viongozi wetu wanamchukia Zitto
na tangu siku nyingi walipanga kumfukuza. Nawashauri watafute sababu
nzuri za kumfukuza uongozi na hata uanachama.
Zitto hahusiki na mkakati huu pamoja na kwamba alikuwa ndiye mhusika mkuu, alikuwa hajui lolote.”
Zitto hahusiki na mkakati huu pamoja na kwamba alikuwa ndiye mhusika mkuu, alikuwa hajui lolote.”
Jumamosi iliyopita, mama yake mzazi Zitto, Shida
Salum ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema alisema waraka huo
ulikuwa umeongezwa maneno.
“Hata ule waraka uliongezwa maneno baada ya baadhi
ya wanachama kumpora Mwigamba `laptop’ yake alipokuwa mkoani Arusha
katika kikao cha Chadema,” alisema bila kutaka kufafanua ulibadilishwa
vipi, licha ya kuwataja kwa majina waliohusika kuubadili wakiwamo
wabunge wawili wa chama hicho na viongozi wa ngazi za juu.
Sitoki Chadema
Kuhusu hatima yake ndani ya Chadema, Mwigamba
alisema hana mpango wa kuondoka hata baada ya kuvuliwa uongozi, huku
akisisitiza kuwa hakusudii kuomba radhi kutokana na kuandaa waraka huo.
Alisema hakusudii kuhama kwa kuwa ana historia ndefu na Chadema na anaamini kuwa ndicho mkombozi wa Watanzania.
“Nimekuwa kiongozi wa kata, wilaya, mkoa hadi
taifa. Nimetumia muda wangu mwingi na hata kuhatarisha maisha yangu kwa
ajili ya chama hiki, siwezi kuondoka kutokana na tofauti za kimitazamo
na viongozi wangu,” alisema.
Mwigamba, ambaye alikuwa mfanyakazi katika
Mahakama ya Kimataifa inayosikiliza Kesi za Mauaji ya Halaiki ya Rwanda
(ICTR) na baadaye kujiondoa ili ajikite kwenye siasa, alisema ana imani
yanayotokea sasa katika chama hicho yatapita salama.
kwa habari zaidi tembelea http://www.mwananchi.co.tz
kwa habari zaidi tembelea http://www.mwananchi.co.tz
0 Weka maoni yako hapa:
Post a Comment
COMMENT HAPA