Nov 27, 2013

Times Q&A: Madame Rita ajibu maswali tisa muhimu kuhusu EBSS 2013


Times Q&A: Madame Rita ajibu maswali tisa muhimu kuhusu EBSS 2013 (Audio)Shindano la EBSS 2013 linaelekea ukingoni ambapo November 30, atatangazwa mshindi wa shindano hilo pale Escape 1, Dar es Salaam.

Washiriki watano waliobaki katika shindano hilo ni Emmanuel Msuya, Elizabeth Mwakijambile, Amina Chibaba, Melisa John na Maina Thadei.

Tovuti ya Times Fm imefanya mahojiano na Chief Judge wa shindano hilo, Rita Paulsen aka Madam Rita, na ameweza kujibu vizuri maswali tisa muhimu.

Watu wengi hawakutegemea Mandela angeondolewa kati ya washiriki sita, na walitegemea awe kati ya watano, ni upi mtazamo wako kwa kuzingatia kuwa ulionesha kumkubali sana?

Mandela pale alipofikia wamemshinda wenzake, lakini sio kwamba sio muimbaji mzuri. Tunahitaji mshindi mmoja, kwa hiyo ubora umezidiana na nafikiri hata watazamaji wanakubalina kwamba hapo alipokuwa amefikia wenzake ambao wamebaki wanamzidi hata ukiwaweka kwa pamoja, I’m sure.
Kwa hiyo, ndio kuna mashabiki lakini mshindi lazima awe na uwezo wa kuimba sio tu mshindi kwa sababu watu wanashabikia. Lakini sio kwamba hawezi, huwezi kuwa kama huwezi halafu ukafika top ten, Mandela amefika hadi top six.

Kuna wasichana wanne na mvulana mmoja tu kati ya washiriki walioingia fainali, je hii inaonesha kuwa wasichana wanauwezo zaidi?

Imetokea, sisi huwa tunaangalia vipaji zaidi kuliko gender, imetokea kwamba wasichana wamefanya vizuri kuliko wanaume this year. Kwa hiyo kitu ambacho kimetokea na sio kwamba imepangwa au nini…Imetokea kwamba this year wasichana wamekaza buti na wamefanya vizuri mpaka wakafikia top 4.

Kuna wakati nyie kama Majaji huwa mnatofautiana na unaonesha kukasirika, je huwa iko serious? 

yeah..Huwa inakuwa serious, yeah ni serious!

Unazungumziaje comments za Salama kwa kuwa mara nyingi amekua ‘akimchana’ mshiriki, halafu unaoneka haufarahii alichokisema na hata unabadilika emotionally?

Mimi sina tatizo nae na na-react kutokana na ninavyokuwa najisikia. Lakini Salama mimi namkubali kwa sababu analeta changamoto kwa washiriki na analeta changamoto kwenye meza ya Majaji na ndio maana yupo leo mwaka wa saba. Sina tatizo nayo kwa sababu otherwise itakuwa boring inabidi kuwepo na changamoto. Yeye anaujasiri wa kuweza kuongea anavyoongea na mimi naweza kuongea ninavyoongea.
Niseme tu kwamba kila Jaji ambaye yuko kwenye ile meza ni real, hakuna mtu anafake au whatever. Kila mtu anakuwa anaongea hisia zake zinavyomtuma. Ukizingatia hii ni reality show na kuna washiriki wanataka kusikia yeye anasema nini na hawajali mimi nasema nini, na kuna watazamaji wanataka kusikia yeye anasema nini na wala hawataki kusikia mimi nasema nini. Na hiyo ndio imeifanya EBSS kuwa EBSS…Entertainment.

Kwa kuwa washiriki wote wamekaa nyumba moja kama familia, je huwa wanagombana? Na kama ndiyo, ni njia gani inatumika kuhakikisha wanaenda sawa?

Of course wanagombana, kuna uongozi kuna sheria ambao wanakuwa wanafuatilia, kuna walimu na kuna watu wanaowakosoa. Kwa hiyo it’s a proper organized thing, kuna uongozi kabisa kwenye EBSS. Na ikitokea nisema nao natokea, kwa hiyo kuna discipline ya hali ya juu na discipliners wapo pia.

Ni mshiriki yupi ambaye wewe unaweza kumtaja kama mshiriki mwenye nidhamu/mtiifu zaidi?

Kusema ukweli wote walioshiriki mwaka huu ni watiifu na wana tabia nzuri, they are good kids nashukuru Mungu. Hatujawa na matatizo ya watu kukosa nidhamu, ni vijana wazuri na wasikivu na hakuna hata mmoja wao mwenye tatizo.

Ni mshiriki gani ‘mmoja’ aliyetoka katika shindano hilo lakini kutokana na uwezo wake ungependa sana angekuwa kati ya hawa watano?

Mandela, Mandela..! Tutaangalia pia jinsi ya kumsaidia kama muigizaji (Benchmark Production), I think ni muigizaji zaidi kuliko muimbaji.

Ni ipi picha halisi ya show ijayo ya fainali ya EBSS 2013 na maandalizi, kwa kuzingatia kuwa siku hizi watu huangalia zaidi ubora wa show?

Ni changamoto, lakini mimi naweza kuzungumza kuwa itakuwa very nice, itakua nzuri sana kutokana na..sisi tunapenda kubadilisha na kuwa na vitu vipya kila mwaka. Na mwaka huu hiyo ni changamoto kwetu, hiyo ni sehemu mpya kwetu ni venue mpya pale Escape 1, lakini itakuwa bomba kinoma.

Watu wengi wanatamani P-Funk Majani arudi kwenye meza ya Majaji, wewe kama Chief Judge unalichukuliaje?

Hili tutalifanyia kazi!

msikilize hapa
chanzo na  http://www.timesfm.co.tz

0 Weka maoni yako hapa:

Post a Comment

COMMENT HAPA