Wakieleza kondakta wa basi hilo aina ya Yunton
lenye usajili wa namba T 930 BUW ambaye amevunjika miguu yote miwili
bwana Thadei Muhando na mkaguzi wa basi la Shabubu bwana Williamu
Ofyenge wamesema wakati basi lao lilikuwa liki lipita lori la mafuta
gafla waliona basi lingine liki wapita na kuwa magari matatu katika
njia moja na hatimaye dereva wao alishindwa kulimudu basi lao na
kusababisha kupinduka.
Mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa singida
daktali banuba deogratius amethibitisha kupokea majeruhi ishirini na
nane ambao wanapatiwa matibabu na mgonjwa moja ambaye alikuwa kondakta
wa basi amevunjika miguu yote miwili na wanampatia matibabu.
Kwa upande wake dereva wa roli la mafuta aina ya
benzi lenye usajili wa namba raa 496n na tela lake lenye usajili wa
namba rl 0255 ambalo lilikuwa likitokea nchi ya Rwanda bwana Hadimana
Benjamini amesema alipitwa na mabasi mawili na moja likamgonga upande
wake na hatimaye kuanguka .
Mkuu wa wilaya ya Singida mwalimu Queen Mlozi
ambaye alifika katika ajali hiyo pamoja na kuwatembelea majeruhi
amewataka madereva wote kuzingatia sheria za barabarani ilikuweza
kunusuru uhai wa watu na majeruhi.
CHANZO NA ITV
0 Weka maoni yako hapa:
Post a Comment
COMMENT HAPA