Jan 14, 2014

JOYCE KIRIA AFUNGUKA TENA DHIDI YA WASALITI WA NDOA ZAO

 
Mambo yanazidi kuwa magumu lakini Mungu atanisimamia kwa jina la Yesu....
Ndugu jamaa na marafiki wananizonga kutokana na Msimo wangu wa kuvunja Ukimya juu ya wanaume na wanawake Wasaliti.

Ivi Usaliti unakubalika? Kama unakubalika endelea kunishambulia kadiri unavyoweza.

Kama Usaliti haukubaliki basi jirekebishe na ukiwaona Wasaliti wenzako Sema nao waache.

Ndoa yenyewe inavunjika kwa sababu ya Usaliti..

Najua kuna wengine mnasoma bandiko langu mkiwa na vimada au mahawara zenu. NI MKUKI WA MOTO SANA. Ila kuanza upya siyo dhambi. Unaweza kuacha na ukakemea dhambi hiyo ya Usaliti ili kulinda Nyumba zetu...

Hata Ndoa yangu Imeanza kuwa Mashakani kutokana na Huu MSIMAMO wangu. Ni kweli nampenda sana Mume wangu Henry Kilewo, namuheshimu sana. Kama kupinga Usaliti nimeonyesha tabia mbaya ya kutokukutii kama Mume wangu basi nipo tayari kulipa gharama...

Usaliti unatuumiza sana Wanawake na huu hapa chini ni mfano mmoja mdogo tu, wa dada aliyenitumia in box akiugua juu ya Usaliti

" dada, me nina matatizo na mzaz mwenzangu,, anamwanamke nje na nahc anampenda yeye sana kuliko mimi kwa sms zao ninazoziona' na bado nampenda kiasi nalia muda wote ninapohc amenisaliti' naomba ushauli wako,,"

Wanawake wanaolia juu ya Usaliti ni wengi sanaaaa. Wanawake Wanaoteseka na wametelekezwa pamoja na watoto wao kwa sababu za Usaliti ni wengi mnoooo, Wanawake wanaopigwa na Kutukanwa, Kunyimwa huduma muhimu za Ndoa, kwa sababu ya Usaliti ni lukuki...

Wanawake wengi wanaopitia changamoto kwenye Ndoa zao, ambao tulifanikiwa kufanya nao Wanawakelive na wengi waliotufikia kwa njia ya simu na Sms chanzo cha migogoro ni Usaliti..japo wanaume nao wapo wanaonyanyaswa na wake zao kwa sababu ya Usaliti...

Bora kuachana kama mmechokana kuliko kusalitiana..

Usaliti ni Ukatili mkubwa sana dhidi ya Wanawake. Sii tu kupigwa au kujeruhiwa na Mume ndo Ukatili, Hata Kusalitiwa ni Ukatili wa kijinsia dhidi ya Wanawake/Wanaume.
Sintakaa kimya kupinga Usaliti...

NIMEAMUA KUSIMAMA, NIPO TAYARI KULIPA GHARAMA HATA KAMA NI UHAI WANGU....hii ni 2014 nimechoka kuona machozi ya Wanawake, ni wakati wa kupambana siyo kulia na kulalamika.

TUACHANE NA WASALITI, TUMSHUKURU MUNGU TUANZE UPYA...

NAIMANI WATAPUNGUZA NA MWISHO WATAACHA KABISA...

Note: Kuna wengine wanawaletea hawara zao hadi chumbani!!!! Yaani kaona kufanyia huko nje haitoshi, hadi nyumbani kwako chumbani!!!!! Woiyeeeeeeeeee Kiruuuuuuuuu....yeleuwiiiiiiiiiii

Niuweni lakini Ukweli Utasimama Daima....

Wanawake sisi ndo wadau wa kwanza wa kuondoa hii dhambi ya Usaliti...Wewe unaelala na Mume wa Mtu acha tafuta wako. Wewe unaemwacha mkeo na kwenda kumdhalilisha kwa wanawake wengine acha tulia na mkeo...

0 Weka maoni yako hapa:

Post a Comment

COMMENT HAPA