Exclusive interview na Professor Jay kuhusu Mwanalizombe Studios, D'Knob na Suma G ni wasanii wa mwanzo kufanya kazi (Audio)
Mchawi wa Rhymes, Mr. Red Carpet, Professor Jay ama Joseph Haule kwa
jina la kuzaliwa amefungua rasmi studio yake binafsi inayojulikana kama
‘Mwanalizombe Studios.
Tovuti ya Times Fm imefanya interview exclusively na mkongwe huyo katika game la Bongo Flava mwenye heshima kubwa katika game.
Mwanzo kulikuwa na tetesi kwamba Duke ndiye ambaye angekuwa producer
wa Mwanalizombe Studios, lakini Professor Jay amesema kuwa producer
atakayefanya kazi katika studio hiyo anaitwa ‘Villy’, jina geni kwa
wengi lakini anauwezo mkubwa.
Fuatilia interview yote hapa:
Je, studio ya Mwanalizombe imewasaini baadhi ya wasanii kuwa label, na kama bado kuna mpango huo?
Huu ni mwanzo bado na hatuwezi kuahidi vitu vingi sana, kwa sababu
watu wa label ni lazima tuangalie talent na nini, na talent lazima
tuzitafute, talent haziko Dar es Salaam pekee. Na ndio maana katika
tangazo letu tulilolitoa tumeweka email na namba za simu kiasi kwamba
tunaweza kuangalia talent hapa na pale. Lakini so far, hakuna mtu ambaye
tumeshamsaini officially kwamba yuko Mwanalizombe.
Lakini nia na madhumuni ya kuanzisha Mwanalizombe ilikuwa ni
kuangalia pia na talent, kwa sababu tumeona talent nyingi zimekuwa
mchangani haziwezi kushine kwa sababu gharama za studio zimekuwa kubwa
na vitu vingine kama hivyo, kwa hiyo tunaaangalia jinsi gani
tutawaboost. Hatuwezi kusema kwamba tutawarekodi bure kwa sababu uwezo
hatuna wa kufanya hivyo kwa sababu kuna umeme kuna kodi na kuna bili
hatuwezi sema tutafanya free. Lakini tunataka kuangalia talents ambazo
zipo zimejificha ili ziweze kuonekana.
Kwa sababu sasa hivi tunasikia kuna wasanii wengi wanasikika lakini
wengi hawana zile talents ambazo mimi nazijua. Nimepita mikoa mingi
nimeona kuna talent za hatari lakini bado hazijapata nafasi. Kwa hiyo
bado ni mwanzo lakini nadhani huko mbele tutaweza kuwasaini watu na
tutaweza kuwa nao kwa sababu tunataka tuupeleke muziki wetu kwenye next
level.
Ni sapoti gani umepata kutoka kwa wadau wengine wa muziki kuiinua studio yako?
Cha kwanza ilikuwa, watu wakisikia Mwanalizombe...nilikuwa nawaambia
tu kwamba kuna studio nilikuwa naifanya, lakini pia nilikuwa napata
tatizo la maproducer. Kuna maproducer ambao wamenisaidia kuifanya
Mwanalizombe iwe hapo ilipo. Mtu kama Dunga alinisaidia tangu naanza
kununua vyombo, vingine nilinunua hapa na vingine nilivinunua ng’ambo
nilikuwa nikimpigia na yeye ananishauri kufanya hiki na kile. Naye
alikuwa interested kufanya kazi lakini amebanwa wana kazi zao ambazo
wanafanya.
Mwingine ni Duke ambaye alinisaidia kufanya setup, kufunga ile studio
na kufanya kila kitu. Duke naye amebanwa kuna biashara zake anazifanya
lakini pia bado anatusapoti tuko naye pale. So, nilikuwa napata tabu
kumpata producer ambaye anaweza kuendana na vyombo vyetu vya kisasa
ambaye anaweza kupiga aina zote za muziki. Hatutaki kufanya aina moja tu
ya muziki sijui Bongo Flava tu, hapana. Tunataka anakuja mtu anafanya
mchiriku anafanya, mtu anafanya gospel anafanya na vitu vingine kama
hivyo. Kwa hiyo ilikuwa ngumu hata kumpata Villy kwa sababu na yeye
alikuwa anaprogram zake sema bahati mbaya alikuwa ana studio yake hiyo
wakamuibia.
So, nadhani atatufaa pale kwa sababu anapiga kila aina ya muziki, ni
mtu ambaye yuko humble, ni mtu ambaye nadhani kila mtu ambaye atakuja
Mwanalizombe ataridhika.
Je, kuna baadhi ya kazi ambazo tayari Mwanalizombe imezifanya na umefanya na wasanii gani?
Sasa hivi ndio tumeanza kufanya kazi na akina D’Knob wanaingiza pale,
akina Suma G na watu wengi ambao wameanza kuja kufanya, ma- underground
wengi. Sipendi kuwaongelea sana kwa sababu kazi bado hazijakamilika na
watu bado wanaendelea lolote linawea kutokea sio. Kwa hiyo itakapofika
time tutasema sasa hii ni ngoma ya kwanza kutoka Mwanalizombe na vitu
kama hivyo.
Kwa sasa hivi ndio tumejipanga rasmi kuanza kutoa nyimbo kutoka Mwanalizombe.
Sababu zipi zilipelekea uanzishe studio yako binafsi, na je,
unadhani kuna gap lipi kwa upande wa studio Tanzania ambalo Mwanalizombe
italiziba?
Sababu kubwa ya kuanzisha Mwanalizombe pamoja na kwamba nataka
nisaidie artists…kwa sababu najua katika wasanii ambao geti lao
linagongwa, langu linaongoza. Kila mtu anakuwa na imani kwamba Professor
Jay anaweza kunisaidia na wengi wanakuja kuniomba hela za kwenda
kurekodi studio. So, ili niweze kupata solution ya vitu vingi kwa mpigo
nimeona kwamba nitengeneze studio, na hata gharama zao ambazo zitakuwa
ni ndogo au zitakuwaje…lakini at least studio itapunguza geti langu
kuweza kuyumbayumba na kugongwa na vitu kama hivyo.
Hiyo ni sababu ya kwanza, lakini sababu ya pili…mimi mwenyewe ni
mwanamuziki, napata tabu saa zingine na maproducer pia sometimes sipati
kazi yangu kwa wakati na vitu vingine, kwa hiyo kazi zangu pia
ntazifanya. Sisemi kazi zangu zote ntazifanya Mwanalizombe, hapana,
lakini itanirahisishia. Kuna kazi nyingine zinatakiwa ziende quick na
kuna kazi zingine zinatakiwa ziende katika wakati lakini zilikuwa
zinanisumbua na vitu vingine kama hivyo.
Na Mwanalizombe tumeita Mwanalizombe Studios kwa maana kwamba
hatutakuwa tunafanya audio tu peke yake. Tumeagiza vyombo au vifaa pia
vya video na pia tunaweza kufanya photo-shoot na vitu vingi ambavyo
leseni yetu inatuonesha hivyo. So, tunaweza tukafanya hivyo vitu kwa
wakati wowote lakini tumeanza na audio production kwa kuwa ni wakati
wake na ndio kitu ambacho kinahitajika sana kwa kipindi hiki.
Sitaki kusema kwamba nakuja kuleta ushindani ama nakuja kuwa number
one, hapana. Nakuja kufanya kufanya muziki kwa ajili ya kufanya
mapinduzi mazuri, kwa ajili ya kufanya revolution na kuwasaidia watu kwa
mafanikio ya muziki wa kizazi kipya.
Mwanalizombe Studios inapatikana wapi, na endapo mtu anataka kuwapata atumie njia gani?
Mwanalizombe Studio iko Msasani mwisho karibu na Capetown Fish Market, watu wakaribie tu, watu wenye talent zao. Na email ni mwanalizombestudios@yahoo.com na mwanalizombestudios@gmail.com. Na namba tunazozitumia studio ni 0757919192.
Usikose kusikiliza The Jump Off ya 100.5 Times Fm, leo kuanzia saa
mbili kamili usiku hadi saa nne kamili usiku. Unaweza kusikiliza Online
kupitia link hii popote pale duniani
0 Weka maoni yako hapa:
Post a Comment
COMMENT HAPA