Rais wa klabu ya Barcelona, Sandro Rosell, amejiuzulu
kufuatia madai ya utumizi mbaya wa fedha wakati klabu hiyo ilipomsajili
nyota wa Brazil, Neymar mwaka uliopita.
Mapema wiki hii, gazeto moja nchini Uhispania ilinadi kuwa, klabu hiyo ilitumia Uro milioni arubaini zaidi kuliko ilivyotangazwa kumsajili mchezaji huyo kutoka Brazil.
Ripoti zinasema kuwa babake Neymar na mawakala wengine waliohusika na mkataba huo walilipwa kiasi fulani cha pesa ambacho hakikutangazwa.
0 Weka maoni yako hapa:
Post a Comment
COMMENT HAPA