May 20, 2014

MOTO WATEKETEZA NYUMBA JIJINI MBEYA

Wakazi wa eneo la Makunguru jijini Mbeya wakiwa wamesimama nje nyumba iliopo kwenye eneo hilo ambayo imepatwa na dhahma ya kuungua moto na kuteketea kwa mali zote zilizokuwemo ndani ya nyumba hiyo, kutokana na kinachosadikiwa kuwa ni hitilafu ya umeme. Bado haijadhibitika mpaka sasa kama kuna mtu yeyote aliedhurika kwenye tukio hilo lililotokea mchana wa jana jijini humo.

 
Sehemu ya mali zilizokuwemo kwenye nyumba hiyo zikiwa zimeteketea zote kwa moto huo.

Majirani wakichungulia  kupitia dirishani kuona namna moto ulivyoteketeza mali zilizomo kwenye nyumba hiyo.
 Wengine walikuwa wakihadhithiana  tukio hilo.


 
 

0 Weka maoni yako hapa:

Post a Comment

COMMENT HAPA