Jul 28, 2014

Mke wa Kingwendu Abakwa.

 Mke wa Kingwendu Abakwa.MKE  wa  Kingwendu  ambaye  ni  muigizaji  maarufu  wa  filamu  za  vichekesho  nchini  amefanyiwa  kitendo  kibaya  cha  ubakaji  na  mwanaume  aliyefahamika  kama  Upunguvuku  katika  pagala  moja  huko  Mbagala  Kingugi  kwa  Kisauti.

Mke  wa  Kingwendu  anayejulikana  zaidi  kwa  jina  la  mama  Maua, alikutwa  na  masahibu  hayo  Alhamisi  iliyopita  baada  ya  kuvamiwa  na  Upunguvuku  anayedaiwa  kuwa  alikuwa  amelewa  na  kuingizwa  kwenye  jumba  ambalo halijasha  kujengwa  lililopo  maeneo  ya  Kwa  Dunga    ambapo  wapita  njia  waliwafuma  na  kuanzisha  mtiti.....

Shuhuda  wa  tukio  hilo  ambaye  hakutaka  jina  lake  liandikwe  amesema  kuwa, wakati  tukio  hilo  linatokea, Kingwendu  mwenyewe  alikuwa  safarini  na  hivyo  majirani  zake  ndio  waliomuokoa  mkewe.

Hata  hivyo  baadhi  ya  majirani  walioongea  na  mwandishi  wamedai  kuwa  wawili  hao ( Upunguvuku  na  mama  Maua)  ni  wapenzi  wa  siku  nyingi  na  wamekuwa  wakionekana  mara  kadhaa  wakienda  kunywa  pombe  za  kienyeji.

"Huyu  Upunguvuku  ni  fundi  Mwashi, tunamfahamu  vizuri  kuwa  ni  hawara  wa  mama  Maua, mara  kadhaa  huwa  tunawaona  wakinywa  pombe  za  kienyeji  pamoja, sema  tu  leo  wamefumwa  wakijivinjari  ndo  mwanamke  anamsingizia  eti  kambaka," alisema  shuhuda  mmoja.

Juhudi  za  kumpata  Kingwendu  kuongelea  mkasa  huo  hazikuzaaa  matunda  kutokana  na  simu  yake  kutopatikana  kila  akipigiwa.

0 Weka maoni yako hapa:

Post a Comment

COMMENT HAPA