Jul 23, 2014

Tiba ya Methadone kwa hisani ya Ray C yamuokoa Video Queen wa Ice Cream, Doreen

Ray C Foundation wameanza kuyaona matunda ya kazi yao ya kuwasaidia watu walioathirika na matumizi ya dawa za kulevya baada ya kumtibu video Queen wa Ice Cream ya Noorah, Doreen kwa kutumia Methadone.

Ray C amepost instagram  picha ya Doreen akionena kuwa na afya nzuri tofauti na awali walipomchukua, na kuandika ujumbe kuhusu hali ilivyo.

 
 Doreen akiwa na Ray C kabla ya kupata matibabu ya Methadone

“Video queen aliecheza kwenye video ya Noorah Ice cream Amerudi katika Hali yake ya kawaida baada ya kuanza Tiba ya Methadone......Nafurahi sana nikiona matunda ya Ray C Foundation..............Keep it up girl!!!Nafurahi kukuona ukiwa na afya njema!!!!!!!Say No to Drugs!”
 

0 Weka maoni yako hapa:

Post a Comment

COMMENT HAPA