Apr 2, 2012

CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA) YASHINDA UBUNGE

CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA) kimeibuka kidedea katika uchaguzi mdogo wa Mbunge katika Jimbo la Arumeru Mashariki ambapo mgombea wake Bw. Joshua Nassari amembwaga vibaya mgombea wa chama tawala Bw. Siyoi Sumari. FikraPevu inaweza  kutangaza kwa uhakika baada ya kufuatilia kura zote za vituo kuwa CDM imeshinda kinyang’anyiro hicho kwa ushindi usio na utata.
Matokeo ya awali yasiyo rasmi yanaonesha kuwa mgombea wa CDM ameshinda kwa zaidi ya kura 6000.
Ushindi wa Bw. Nassari umekuja baada ya kinyang’anyiro kikali cha ushindani uliojaa kila aina ya vituko, vijembe, kejeli, na propaganda za kila aina kati ya vyama vikuu viwili vya kisiasa nchini yaani CCM na CHADEMA. Uchaguzi huu mdogo umefanyika kufuatia kifo cha aliyekuwa mbunge wa Arumeru Mashariki Bw. Jeremiah Sumari aliyefariki takribani miezi mitatu iliyopita.
Kampeni ya uchaguzi mdogo huo huko Arusha ulihusisha vigogo mbalimbali wa vyama hivi vikubwa. Wakati CDM iliwapeleka viongozi wake wa juu CCM nayo ilipeleka viongozi wote wa juu isipokuwa Mwenyekiti wake ambaye ni Rais Bw. Kikwete pamoja na kumtumia Rais Mstaafu Bw. Benjamin Mkapa ambaye alifungua na kufunga kampeni yake.
Kwenye matokeo ya Udiwani kwenye kata zilizopiga kura hadi hivi sasa taarifa zinaonesha kuwa

Kirumba, Mwanza imeenda CDM
Lizaboni, Songea  imeenda CDM
Msambweni, Tanga imeenda CUF
Bariadi, Shinyanga, imeenda CCM

0 Weka maoni yako hapa:

Post a Comment

COMMENT HAPA