Zaidi ya mgambo wa manispaa ya
Kinondoni 30 pamoja na polisi jamii wa kata ya Makumbusho 32
wamenusurika kufa kwa kipigo na kulazimika kukimbia baada ya
kushambuliwa na wafanyabiashara wa soko la Mwananyamala wakati wakifanya
zoezi la kuwaondoa wafanyabiashara hao katika maeneo yasiyo rasmi
pembezoni mwa soko hilo.
ITV imefika katika hospitali ya Mwananyamala na kukuta mgabo hao
wakiwa na majeraha makubwa vichwani, huku wengine wakiwa katika chumba
maalum kwa ajili ya kushonwa majeraha yaliyotokana na kipigo kikali toka
kwa wafanyabiashara hao ambao kwa kiasi kikubwa inadaiwa wamekiuka
sheria kwa kufanya biashara katika maeneo yasiyo rasmi.
Akizungumza na waandsihi wa habari, afisa mtendaji kata ya
Makumbusho Bibi Husna Nondo amesema operesheni hiyo imeandaliwa ili
kuondoa wafanyabiashara hao wasio rasmi katika soko hilo kutokana na
kuwa karibu na barabara pamoja na shule za Mwananyamala B. na shule ya
Minazini na kuwafanya wanafunzi kushindwa kusoma kutokana na kelele
hali iliyochangia kuwa na matokeo mabaya katika mitihani iliyopita.
Mkurugenzi wa manispaa ya Kinondoni bwana Mussa Natty
amewataadharisha baadhi ya wafanyabiashara wanaojichukulia hatua
mikononi na kuwapiga mgambo wa manispaa kinyume cha sheria ambapo
amesema katika kukabiliana na matukio ya namna hiyo yanayoendelea
kujitokeza manispaa inaangalia uwezekano wa kutumia jeshi la polisi
katika operesheni mazingira ili kuweka mji safi.
habari kwaniaba ya I T V DAIMA
0 Weka maoni yako hapa:
Post a Comment
COMMENT HAPA