Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad akihutubia mkutano wa hadhara katika viwanja vya Muwanda Jimbo la Donge
Hatimaye Chama Cha Wananchi (CUF) kimeingia katika kijiji cha Donge
kufanya mkutano wa hadhara katika viwanja vya Muwanda na kuhutubiwa na
Katibu Mkuu wa Chama hicho Maalim Seif Sharif Hamad.
Maelfu ya wafuasi wa Chama hicho kutoka maeneo mbali mbali ya Mjini
na Vijijini walijitokeza katika mkutano huo ili kushuhudia kile
kilichokosekana kwa muda mrefu kuingia katika eneo hilo la Donge kwa
ajili ya Mkutano wa hadhara.
Akizungumza katika mkutano huo, Maalim Seif amesema anajisikia
fahari kuzungumza na wananchi wa Donge katika eneo la ndani la jimbo
hilo.
Amesema Donge ni kijiji chenye historia ndefu na mabacho kimejipatia
umaarufun mkubwa Zanzibar baada ya kutoa wanazuoni kadhaa, pamoja na
kutajwa kwao kushiriki kikamilifu katika Mapinduzi ya mwaka 1964.
Kuhusu mamlaka kamili amesema suala hilo limeanza kudaiwa tangu
wakati wa marehemu mzee Karume, na kwamba wanaobeza kudai mamlaka ya
Zanzibar wanabeza kauli za Mzee Karume ambapo katika mkutano huo pia
iliwekwa sauti ya Mzee Karume alipokuwa akitaja malengo ya Mapinduzi.
Maalim Seif aliingia Donge mapema asubuhi ambapo kabla ya mkutano huo
alifanya shughuli za kuimarisha chama ikiwa ni pamoja na kufungua
matawi ya Chama hicho, barza pamoja na kuweka jiwe la msingi katika tawi
la CUF Donge Muwanda.
Katika Mkutano huo Maalim Seif pia alikabidhi kadi kwa wanachama
wapya 234, baadhi yao wakiwa wanachama na viongozi waliokihama Chama cha
Mapinduzi kwa sababu tofauti, mmoja wao nd. Salim Khamis Nassor akiwa
mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Wilaya (CCM).
Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad akipandisha bendera katika moja ya matawi mapya ya chama hicho katika eneo la Donge
Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad akikabidhi kadi kwa mmoja wa
wanachama wapya waliojiunga na chama hicho katika Jimbo la Donge
Wafuasi wa CUF wakiwa tayari kumsikiliza Katibu Mkuu wa Chama hicho Maalim Seif Sharif Hamad
Wafuasi wa CUF wakiingia Donge na kubeba ujumbe wa kumkaribisha Katibu Mkuu wa Chama hicho Maalim Seif Sharif Hamad
Wafuasi wa CUF wakiwa wakibeba ujumbe mzito katika eneo la Donge
Wafuasi wa CUF wakiwa tayari kumsikiliza Katibu Mkuu wa Chama hicho Maalim Seif Sharif Hamad
Vijana wa CUF Donge, wakighani utenzi katika mkutano wa hadhara wa chama hicho uliofanyika viwanja vya Muwanda Donge.
0 Weka maoni yako hapa:
Post a Comment
COMMENT HAPA