Jul 16, 2012

NI MANJI BOSI MPYA JANGWANI


Manji kulia akiteta na Sanga kushoto

Zoezi la uchaguzi wa Yanga, limekamilika na Yussuf Mehboob Manjia meshinda Uenyekiti wa klabu hiyo, wakati Clement Sanga amechaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti na nafasi za Ujumbe Abdallah Bin Kleb, Aaron Nyanda, Mussa Katabaro na George Manyama.

Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi wa Klabu ya Yanga, Jaji John Mkwawa kushoto akiwa na Mjumbe wa kamati hiyo Mzee Mzimba













Akitangaza matokeo hayo, majira ya saa 10:30 alfajiri katika ukumbi wa Diamond Jubilee, Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi wa klabu ya Yanga Jaji John Mkwawa amemtangza Manji kama mishindi wa nafasi ya uenyekiti kufuatia kupata asilimia 97% ya kura zote zilizopigwa katika nafasi hiyo.
Mwenyekti mpya wa Yanga, Yusuf Manji akiwa na Makamu wake Clement Sanga 
Nafasi ya Makamu Mwenyekiti imekwenda kwa Clement Sanga aliyejipatia asilimia 62% ya kura zote zilizopigwa katika nafasi ya u makamu mwenyekiti.
Abdallah Bin Kleb, Moses Katabaro, Aaron Nyanda na George Manyama  wamechaguliwa katika nafasi ya ujumbe wa kamati ya  Utendaji.
Jaji Mkwawa amewashukuru wana Yanga kwa kuwa wastaarabu na watulivu, kitu kilicholekea kufanyika uchaguzi kwa amani na zoezi hilo kumalizika salama pasipo kuwa na rabsha yoyote.
Matokeo kamili ya wagombea ni:

Nafasi ya Mwenyekiti:
Yusuf Manji (kura 1876)  97.0%,  John Jembele (kura 40) 2.6%,  Edgar Chibura (kura 4) 0.24%

Nafasi ya Makamu Mwenyekiti:
Clement Sanga (kura 1948) 62.6%, Yono S Kevela (kura 475) 23%, Ayoub Nyenzi (kura 288) 14%

Nafasi ya Ujumbe: 
Abdallah Bin Kleb (kura 1942), Moses Katabaro (kura 1068), Aaron Nyanda (kura 922), Geroge Manyama (kura 682), Beda Tindwa (kura 391), Edgar Fongo (kura 295),  Graticius Ishengoma (kura 247),  Jumanne Mwamenywa (kura 251),  Justine Baruti (610),  Lameck Nyambaya (kura 425),  Omary Ndula (kura 170),  Peter Haule (441),  Ramadhan Said (249),  Yono Kivela (123)

kutokana na matokeo yalivyo hapo juu safu ya viongozi waliochaguliwa ni
Mwenyekiti: Yusuf Manji,
Makamu Mwenyekiti: Clement Sanga
Wajumbe: Abdallah Bin Kleb, Moses Katabaro, Aaaron Nyanda, Geroge Manyama
CHANZO NA  BIN ZUBEIRY  wa http://bongostaz.blogspot.com
 

Jul 6, 2012

15 Wateuliwa Kuchezesha Kombe La Kagame

 
Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) limeteua waamuzi 15 kuchezesha michuano ya Kombe la Kagame itakayofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Julai 14-28 mwaka huu.

Waamuzi hao wanatakiwa kuwasili Dar es Salaam, Julai 11 mwaka huu kwa ajili ya vipimo vya afya na mtihani wa utimamu wa viungo utakaofanyika Julai 12 na 13 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam chini ya wakufunzi wa CECAFA.

Kwa upande wa waamuzi wa kati (centre referees) walioteuliwa ni Anthony Ogwayo (Kenya), Dennis Batte (Uganda), Israel Mujuni (Tanzania Bara), Issa Kagabo (Rwanda), Thierry Nkurunziza (Burundi), Farah Aden Ali (Djibouti) na Waziri Sheha (Zanzibar).

Waamuzi wasaidizi (assistant referees) ni Elias Kuloba (Kenya), Peter Sabatia (Kenya), Musa Balikoowa (Uganda), Hamis Changwalu (Tanzania Bara), Jesse Erasmo (Tanzania Bara), Simba Honore (Rwanda), Abdulahi Mahamoud (Djibouti) na Josephat Bulali (Zanzibar).

Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
 

Jul 4, 2012

KOCHA MBELGIJI YANGA TAYARI AMEWASILI DAR, TAZAMA ALIVYOPOKEWA KIFALME


Kocha mpya wa Yanga, Mbelgiji Thom Saintfiet amewasili mida hii Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere, Dar es Salaam na kulakiwa na mamia ya wapenzi wa klabu hiyo. Tazama mapokezi yake tangu anatokea ndani ya Uwanja wa Ndege, hadi akiwa ndani ya gari tayari kwa safari ya Jangwani.











                                                                                                                                












 Picha na habari kwaniaba ya http://bongostaz.blogspot.com ya BIN ZUBEIRY





p

Timu 10 Tanzania Kucheza ROLLINGSTONE Burundi

Timu 10 za Tanzania Bara zitashiriki kwenye michuano ya Rollingstone kwa vijana wenye umri chini ya miaka 20 ambayo mwaka huu itafanyika Makamba nchini Burundi kuanzia Julai 7 mwaka huu.

Jumla ya timu 24 zinashiriki mashindano hayo na zimepangwa katika makundi sita tofauti. Timu nyingine zinatoka Burundi, Kenya, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC), Uganda na Zanzibar.

Timu za Tanzania zilizoingia katika mashindano hayo ni Azam, Bishop High School, Chakyi Academy, Coastal Union, Rollingstone, Ruvu Shooting, Simba, TAYFA Academy, Yanga na Young Life.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Rollingstone, Issa Karata timu zote zinatakiwa kwenda vyeti vya kuzaliwa vya wachezaji wake ili kuthibitisha umri wao. Kamati ya Mashindano itakuwa na uamuzi wa mwisho kuhusu umri wa mchezaji yeyote.

Kila timu inatakiwa kuwa na wachezaji 20 na viongozi watano ambao watagharamiwa na waandaaji kwa huduma za malazi na chakula kwa muda wote wa mashindano hayo yaliyoanzishwa miaka 13 iliyopita.

Wakenya Kuchezesha Ngorongoro Heroes Nyumbani

Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limeteua waamuzi kutoka Kenya kuchezesha mechi ya raundi ya pili kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 20 kati ya Tanzania (Ngorongoro Heroes) na Nigeria.

Mwamuzi atakayechezesha mechi hiyo ya kwanza ya raundi ya pili itakayofanyika Julai 29 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam atakuwa Moses Ojwang Osano.

Waamuzi wasaidizi watakuwa Peter Keireini na Elias Kuloba Wamalwa wakati mwamuzi wa mezani (fourth official) ni Thomas Onyango. Kamishna wa mechi hiyo atakuwa Charles Masembe kutoka Uganda.

Pia CAF imemteua Alfred Kishongole Rwiza wa Tanzania kuwa Kamishna wa mechi ya michuano hiyo kati ya Misri na Kenya itakayochezwa jijini Cairo kati ya Julai 27, 28 na 29 mwaka huu.

TBL YAKABIDHI 'MPUNGA' WA UCHAGUZI YANGA

Mkurugenzi wa Mawasiliano na Mahusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steven Kilindo (kulia) akimkabidhi mfano wa Hundi ya Sh. Milioni 20, Katibu Mkuu wa Yanga, Celestine Mwesigwa (kushoto) katika hafla fupi ya kukabidhi hundi hiyo iliyofanyika makao makuu ya TBL, Ilala Dar es Salaam asubuhi ya leo.
TBL imetoa fedha hizo kwa ajili ya uchaguzi Mkuu wa klabu hiyo, uliopangwa kufanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam, Julai 15, mwaka huu, ikiwa ni sehemu ya mkataba wa udhamini baina ya Yanga na Kilimanjro Premium Lager Beer, inayozalishwa na TB L.  
Wengine nyuma yao, kutoka kulia ni Katibu wa Kamati ya Uchaguzi ya Yanga, Francis Kaswahili, Katibu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Angetile Osiah, Meneja wa Bia ya Safari Lager aliyemuwakilisha George Kavishe, Meneja wa Bia ya Kilimanjaro aliye safarini na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Yanga, Jaji John Mkwawa.  

Angetile akielezea jambo, kulia kwake ni Kaswahili

Ofisa Habari wa Yanga, Louis Sendeu katikati akiwa na 'vimwana' Dina Ismail kulia na Elizabeth Mayemba kushoto

Mwesigwa akiondoka TBL na begi lake dogo likiwa na 'mahela', kulia ni Clara Alphonce wa Mwananchi

Mkurugenzi wa Executive Solutions, Aggrey Marealle aliyekuwa mwongoza shughuli hiyo


Oscar Shelukindo katikati akimuwakilisha George Kavishe. Kulia ni Kilindo na kushoto Mwesigwa

Jaji Mkwawa akitafakri jambo

Mwesigwa akizungumza   picha na habari kwa niaba ya   BIN ZUBEIRY  kwa habari zaidi tembelea www.http://bongostaz.blogspot.com      











                           




Yanga yaanza kwa kupoteza


Kikosi cha pili cha mabingwa wa Kombe la Afrika Mashariki na Kati, Dar Young Africans kinachojiandaa na michuano ya Rollingstone kimekubali kufungwa goli 3-2 na Jamhuri ya Pemba, katika mchezo wa kombe la urafiki uliokwisha hivi punde.

Katika mchezo huo Yanga walikuwa wa mwanza kupata goli katika dakika ya 18 mfungaji akiwa Shaban Hamisi.

Jamhuri walifanikiwa kusawazisha goli hilo katika dakika ya 34, na kuongeza jingine katika dakika ya 45. Hivyo kupelekea Yanga kwenda mapumzika wakiwa nyuma kwa goli 2-1.

Katika dakika ya 69 Jamhuri walifanikiwa kuandika goli la tatu huku Yanga wakifunga goli lao la pili katika dakika ya 77 kupitia kwa Notekelly Masasi, na kupelekea mpira kumalizika kwa Yanga kufungwa goli 3-2.

Habari kwa niaba ya  http://aboodmsuni.blogspot.com/ wa   SPORTS IN BONGO

Jul 3, 2012

MISRI Yaahirisha Mechi Dhidi Ya Ngorongoro HEROES

Mechi mbili za kirafiki kati ya timu ya Taifa ya Tanzania kwa vijana wenye umri chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heroes) na Misri zilizokuwa zichezwe mwezi huu zimefutwa.

Chama cha Mpira wa Miguu Misri (EFA) kimetuma taarifa jana (Julai 1 mwaka huu) kikiomba kusogezwa mbele hadi mwishoni mwa Agosti baada ya kushindwa kupata usafiri wa ndege kuwahi tarehe ambazo ilikubaliana na TFF kwa ajili ya mechi hizo.

Ngorongoro Heroes ambayo tayari iko kambini ilikuwa icheze mechi hizo Julai 3 na 5 mwaka huu jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya maandalizi kabla ya kuikabili Nigeria katika mechi ya michuano ya Afrika, Julai 29 mwaka huu.

Mechi nyingine za kirafiki kwa Ngorongoro Heroes inayofundishwa na Jakob Michelsen zitachezwa Julai 14 na 16 mwaka huu dhidi ya Rwanda.

Jul 2, 2012

SPAIN NDIO MABINGWA WAPYA WA ULAYA 2012


Timu ya Spain jana usiku ilidhihilisha kuwa wao ndio mabingwa wa soka wa dunia baada ya jana kuibuka mabingwa wa soka wa Ulaya baada ya kuifunga timu ya Itali kwa mabao 4-0.

 David Silva of Spain scores the opening goal
Mfungaji wa goli la kwanza Silva

We are the champions: Skipper Iker Casillas lifts the trophy as the team celebrate 
Iker Casillas akiwa amenyanyua juu kombe baada ya kukabidhiwa huku wachezaji wa Spain wakishangilia kwa nguvu.

 Spain celebrate after their 4-0 victory 
Wachezaji wa Spain wakishangilia baada ya kuibuka na ushindi wa goli 4-0 dhidi ya Itali

Mario Balotelli of Italy shows his dejection as the the Spanish team celebrate 
Mario Balotelli akiwa amini kilichotokea baada ya mpira kwisha

 
Cassanoakijaribu kuipenya ngome ya ngumu ya Spain

Fernando Torres of Spain scores his side's third goal 
Fernando Torresnae hakuwa nyuma katika kuiadhibu Itali

Juan Mata of Spain scores his team's fourth goal 
Juan Mata alifunga ukurasa wa magoli kwa Spain hapo jana ni goli la 4

Spain wao walitumia mtindo wao wa (4-3-1-2) na iliwakilishwa na  Casillas 7; Arbeloa 7, Pique 8, Ramos 8, Jordi Alba 8; Xavi 8, Busquets 7, Xabi Alonso 7; Fabregas 8 (Torres, 75, 7); Silva 8 (Pedro, 58, 7), Iniesta 9 (Mata, 87, 6)

Itali wao walitumia mtindo wao wa  (4-1-3-2)  na iliwakilishwa na  Buffon 7; Abate 6, Barzagli 6, Bonucci 5, Chiellini 4 (Balzaretti, 21, 7); Pirlo 7; Marchisio 6, Montolivo 6 (Motta, 56, 6), De Rossi 7; Balotelli 5, Cassano 5 (Di Natale, 46, 6)

 Referee: Pedro Proenca (Portugal)

Jun 19, 2012

Nicklas Bendtner anatakiwa Benfica


Benfica imeonesha nia ya kumtaka mchezaji wa Asernal raia wa Denmark Nicklas Bendtner 24.
Imeripotiwa kudai kwamba Benfica wamekuwa katika kuwasiliana na Arsenal kuanza mazungumzo juu ya uhamisho.Kilichobaki ni Asernal wao kukubali ofa yao



Je, hamjui mimi ni nani?  Pele Denmark, Nicklas Bendtner, anapata knickers yake katika twist
Je, hamjui mimi ni nani? Pele wa Denmark, Nicklas Bendtner, ameandika ujumbe huo kwenye twitter yake 



Je, kuangalia, Arsene?  Pengine si - Arsenal Bendtner wa 'kazi' inaonekana juu, pamoja na malengo ya Euro
Je, kuangalia, Arsene? Pengine si - Arsenal Bendtner wa 'kazi' inaonekana juu, pamoja na malengo ya Euro  



 

Jun 18, 2012

ratiba ya ligi uingereza yatolewa rasmi

Saturday, 18 August 2012
Arsenal v Sunderland
Everton v Man Utd
Fulham v Norwich
Man City v Southampton
Newcastle v Tottenham
QPR v Swansea
Reading v Stoke
West Brom v Liverpool
West Ham v Aston Villa
Wigan v Chelsea
Saturday, 25 August 2012
Aston Villa v Everton
Chelsea v Newcastle
Liverpool v Man City
Man Utd v Fulham
Norwich v QPR
Southampton v Wigan
Stoke v Arsenal
Sunderland v Reading
Swansea v West Ham
Tottenham v West Brom
Saturday, 1 September 2012
Chelsea v Reading
Liverpool v Arsenal
Man City v QPR
Newcastle v Aston Villa
Southampton v Man Utd
Swansea v Sunderland
Tottenham v Norwich
West Brom v Everton
West Ham v Fulham
Wigan v Stoke
Saturday, 15 September 2012
Arsenal v Southampton
Aston Villa v Swansea
Everton v Newcastle
Fulham v West Brom
Man Utd v Wigan
Norwich v West Ham
QPR v Chelsea
Reading v Tottenham
Stoke v Man City
Sunderland v Liverpool
Saturday, 22 September 2012
Chelsea v Stoke
Liverpool v Man Utd
Man City v Arsenal
Newcastle v Norwich
Southampton v Aston Villa
Swansea v Everton
Tottenham v QPR
West Brom v Reading
West Ham v Sunderland
Wigan v Fulham
Saturday, 29 September 2012
Arsenal v Chelsea
Aston Villa v West Brom
Everton v Southampton
Fulham v Man City
Man Utd v Tottenham
Norwich v Liverpool
QPR v West Ham
Reading v Newcastle
Stoke v Swansea
Sunderland v Wigan
Saturday, 6 October 2012
Chelsea v Norwich
Liverpool v Stoke
Man City v Sunderland
Newcastle v Man Utd
Southampton v Fulham
Swansea v Reading
Tottenham v Aston Villa
West Brom v QPR
West Ham v Arsenal
Wigan v Everton
Saturday, 20 October 2012
Fulham v Aston Villa
Liverpool v Reading
Man Utd v Stoke
Norwich v Arsenal
QPR v Everton
Sunderland v Newcastle
Swansea v Wigan
Tottenham v Chelsea
West Brom v Man City
West Ham v Southampton
Saturday, 27 October 2012
Arsenal v QPR
Aston Villa v Norwich
Chelsea v Man Utd
Everton v Liverpool
Man City v Swansea
Newcastle v West Brom
Reading v Fulham
Southampton v Tottenham
Stoke v Sunderland
Wigan v West Ham
Saturday, 3 November 2012
Fulham v Everton
Liverpool v Newcastle
Man Utd v Arsenal
Norwich v Stoke
QPR v Reading
Sunderland v Aston Villa
Swansea v Chelsea
Tottenham v Wigan
West Brom v Southampton
West Ham v Man City
Saturday, 10 November 2012
Arsenal v Fulham
Aston Villa v Man Utd
Chelsea v Liverpool
Everton v Sunderland
Man City v Tottenham
Newcastle v West Ham
Reading v Norwich
Southampton v Swansea
Stoke v QPR
Wigan v West Brom
Saturday, 17 November 2012
Arsenal v Tottenham
Fulham v Sunderland
Liverpool v Wigan
Man City v Aston Villa
Newcastle v Swansea
Norwich v Man Utd
QPR v Southampton
Reading v Everton
West Brom v Chelsea
West Ham v Stoke
Saturday, 24 November 2012
Aston Villa v Arsenal
Chelsea v Man City
Everton v Norwich
Man Utd v QPR
Southampton v Newcastle
Stoke v Fulham
Sunderland v West Brom
Swansea v Liverpool
Tottenham v West Ham
Wigan v Reading
Tuesday, 27 November 2012
Aston Villa v Reading
Man Utd v West Ham
Southampton v Norwich
Stoke v Newcastle
Sunderland v QPR
Swansea v West Brom
Tottenham v Liverpool
Wigan v Man City
Wednesday, 28 November 2012
Chelsea v Fulham
Everton v Arsenal
Saturday, 1 December 2012
Arsenal v Swansea
Fulham v Tottenham
Liverpool v Southampton
Man City v Everton
Newcastle v Wigan
Norwich v Sunderland
QPR v Aston Villa
Reading v Man Utd
West Brom v Stoke
West Ham v Chelsea
Saturday, 8 December 2012
Arsenal v West Brom
Aston Villa v Stoke
Everton v Tottenham
Fulham v Newcastle
Man City v Man Utd
Southampton v Reading
Sunderland v Chelsea
Swansea v Norwich
West Ham v Liverpool
Wigan v QPR
Saturday, 15 December 2012
Chelsea v Southampton
Liverpool v Aston Villa
Man Utd v Sunderland
Newcastle v Man City
Norwich v Wigan
QPR v Fulham
Reading v Arsenal
Stoke v Everton
Tottenham v Swansea
West Brom v West Ham
Saturday, 22 December 2012
Chelsea v Aston Villa
Liverpool v Fulham
Man City v Reading
Newcastle v QPR
Southampton v Sunderland
Swansea v Man Utd
Tottenham v Stoke
West Brom v Norwich
West Ham v Everton
Wigan v Arsenal
Wednesday, 26 December 2012
Arsenal v West Ham
Aston Villa v Tottenham
Everton v Wigan
Fulham v Southampton
Man Utd v Newcastle
Norwich v Chelsea
QPR v West Brom
Reading v Swansea
Stoke v Liverpool
Sunderland v Man City
Saturday, 29 December 2012
Arsenal v Newcastle
Aston Villa v Wigan
Everton v Chelsea
Fulham v Swansea
Man Utd v West Brom
Norwich v Man City
QPR v Liverpool
Reading v West Ham
Stoke v Southampton
Sunderland v Tottenham
Tuesday, 1 January 2013
Chelsea v QPR
Liverpool v Sunderland
Man City v Stoke
Newcastle v Everton
Southampton v Arsenal
Swansea v Aston Villa
Tottenham v Reading
West Brom v Fulham
West Ham v Norwich
Wigan v Man Utd
Saturday, 12 January 2013
Arsenal v Man City
Aston Villa v Southampton
Everton v Swansea
Fulham v Wigan
Man Utd v Liverpool
Norwich v Newcastle
QPR v Tottenham
Reading v West Brom
Stoke v Chelsea
Sunderland v West Ham
Saturday, 19 January 2013
Chelsea v Arsenal
Liverpool v Norwich
Man City v Fulham
Newcastle v Reading
Southampton v Everton
Swansea v Stoke
Tottenham v Man Utd
West Brom v Aston Villa
West Ham v QPR
Wigan v Sunderland
Tuesday, 29 January 2013
Arsenal v Liverpool
Aston Villa v Newcastle
Man Utd v Southampton
Norwich v Tottenham
QPR v Man City
Reading v Chelsea
Stoke v Wigan
Sunderland v Swansea
Wednesday, 30 January 2013
Everton v West Brom
Fulham v West Ham
Saturday, 2 February 2013
Arsenal v Stoke
Everton v Aston Villa
Fulham v Man Utd
Man City v Liverpool
Newcastle v Chelsea
QPR v Norwich
Reading v Sunderland
West Brom v Tottenham
West Ham v Swansea
Wigan v Southampton
Saturday, 9 February 2013
Aston Villa v West Ham
Chelsea v Wigan
Liverpool v West Brom
Man Utd v Everton
Norwich v Fulham
Southampton v Man City
Stoke v Reading
Sunderland v Arsenal
Swansea v QPR
Tottenham v Newcastle
Saturday, 23 February 2013
Arsenal v Aston Villa
Fulham v Stoke
Liverpool v Swansea
Man City v Chelsea
Newcastle v Southampton
Norwich v Everton
QPR v Man Utd
Reading v Wigan
West Brom v Sunderland
West Ham v Tottenham
Saturday, 2 March 2013
Aston Villa v Man City
Chelsea v West Brom
Everton v Reading
Man Utd v Norwich
Southampton v QPR
Stoke v West Ham
Sunderland v Fulham
Swansea v Newcastle
Tottenham v Arsenal
Wigan v Liverpool
Saturday, 9 March 2013
Arsenal v Everton
Fulham v Chelsea
Liverpool v Tottenham
Man City v Wigan
Newcastle v Stoke
Norwich v Southampton
QPR v Sunderland
Reading v Aston Villa
West Brom v Swansea
West Ham v Man Utd
Saturday, 16 March 2013
Aston Villa v QPR
Chelsea v West Ham
Everton v Man City
Man Utd v Reading
Southampton v Liverpool
Stoke v West Brom
Sunderland v Norwich
Swansea v Arsenal
Tottenham v Fulham
Wigan v Newcastle
Saturday, 30 March 2013
Arsenal v Reading
Aston Villa v Liverpool
Everton v Stoke
Fulham v QPR
Man City v Newcastle
Southampton v Chelsea
Sunderland v Man Utd  
Swansea v Tottenham
West Ham v West Brom
Wigan v Norwich
Saturday, 6 April 2013
Chelsea v Sunderland
Liverpool v West Ham
Man Utd v Man City
Newcastle v Fulham
Norwich v Swansea
QPR v Wigan
Reading v Southampton
Stoke v Aston Villa
Tottenham v Everton
West Brom v Arsenal
Saturday, 13 April 2013
Arsenal v Norwich
Aston Villa v Fulham
Chelsea v Tottenham
Everton v QPR
Man City v West Brom
Newcastle v Sunderland
Reading v Liverpool
Southampton v West Ham
Stoke v Man Utd
Wigan v Swansea

Michuano Ya KAGAME Kuanza Julai 14

Mashindano ya Klabu bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kombe la Kagame) yanayoandaliwa na Baraza la Vyama ya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) yatafanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Julai 14-29 mwaka huu ambapo timu zinatakiwa kuthibitisha ushiriki wao kabla ya Juni 25 mwaka huu.

Yanga itashiriki mashindano hayo ikiwa bingwa mtetezi, wakati Tanzania Bara itawakilishwa na mabingwa wake Simba na Makamu bingwa Azam. Mashindano hayo yatafanyika jijini Dar es Salaam kwenye Uwanja wa Taifa na Uwanja wa Chamazi pekee kwa sababu ya kupunguza gharama za uendeshaji.

Ratiba ya mashindano hayo yanayoshirikisha mabingwa kutoka nchi kumi na moja ambao ni wanachama wa CECAFA itapangwa Juni 29 mwaka huu.

Mashindano haya ni muhimu kwa CECAFA na Tanzania Bara ambayo ndiyo mwenyeji kwa maendeleo ya mpira wa miguu na pia kukuza kiwango cha mchezo huo kwa ukanda huu ambao kwa Afrika unaoongoza kwa kufanya mashindano mengi ya timu za Taifa pamoja na klabu.

Mwenyekiti wa CECAFA ambaye pia ni Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodegar Tenga amewaomba wadau kujitokeza kudhamini michuano hiyo ambayo itaoneshwa na kituo cha televisheni cha SuperSport. Pia amewataka washabiki kujitokeza kwa wingi viwanjani kuunga mkono michuano hiyo.

CECAFA inawashukuru wadau wote kwa kuwezesha michuano hiyo kufanikiwa akiwemo Rais wa Rwanda, Paul Kagame kwa kutoa zawadi za fedha kwa washindi, Serikali ya Tanzania kwa kutoa Uwanja wa Taifa na Kamati ya Utendaji ya TFF kwa kukubali kuwa mwenyeji wa mashindano hayo.

Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
Mjumbe, Kamati ya Habari CECAFA

Uchaguzi Wa Viongozi Wa Yanga Kujaza Nafasi Zilizo Wazi



Kamati ya Uchaguzi ya TFF inawataarifu wadau na wapenzi wa soka kuwa mchakato wa uchaguzi wa viongozi wa YANGA kujaza nafasi zilizowazi za Kamati ya Utendaji unaendelea vizuri chini ya Kamati ya Uchaguzi ya YANGA.

Kamati ya Uchaguzi ya TFF imepokea kutoka Kamati ya Uchaguzi ya YANGA nakala za fomu za maombi ya uongozi wa YANGA pamoja na nakala za vyeti vya elimu vya waombaji uongozi kama sehemu ya taarifa ya awali ya mchakato wa uchaguzi huo wa YANGA. 

Kamati ya Uchaguzi ya TFF imebaini kuwa baadhi ya waombaji uongozi wamewasilisha nakala za vyeti vya kuhudhuria masomo ya sekondari (Secondary School Leaving Certificate) badala ya nakala za vyeti vya kuhitimu masomo ya elimu ya sekondari (Certificate of Secondary Education).

Kamati ya Uchaguzi ya TFF imekwisha ielekeza Kamati ya Uchaguzi ya YANGA kuwataka wagombea wote kuzingatia Kanuni za Uchaguzi za wanachama wa TFF Ibara ya 10(4) na (5) inayowataka wagombea wote kujaza Fomu Na.1 ya maombi ya uongozi na kuambatanisha nakala ya cheti cha Elimu ya Sekondari (Certificate of Secondary Education) kama ilivyoainishwa kwenye 

Fomu Na.1 kipengere Na.9. Kamati ya Uchaguzi ya TFF imeiagiza Kamati ya Uchaguzi ya YANGA iwashauri wagombea ambao vyeti vyao vimepotea wawasiliane na Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) kwa maandishi ili kupata ‘Statement of Examination Results’ itakayotumwa kwa Kamati ya Uchaguzi ya YANGA kupitia TFF kuthibitisha kuwa wamehitimu elimu ya kidato cha nne.

Uhakiki wa vyeti vya elimu ya sekondari vya waombaji uongozi hufanywa na NECTA na vyuo husika kwa elimu ya juu kwa chaguzi za wanachama wa TFF. Wanachama wote wa TFF wanatakiwa kuzingatia kikamilifu matakwa ya Kanuni za Uchaguzi.

Imetolewa na:
IDARA YA HABARI
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

Jun 15, 2012

Matukio mbalimbali Tuzo za TASWA.2011-2012

 
Kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars Kim Paulsen akikabidhi tuzo ya mwanamichezo bora wa Olimpiki Maalum Heri Suleiman

  
Mchezaji wa zamani wa timu ya Coast Union ya Tanga na Timu ya taifa Salim Amir akikabidhi tuzo kwa mchezaji Shomari Kapombe

  
Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji la Zanzibar ZBC Omar Said Ameir akikabidhi tuzo ya mchezaji bora wa Tanzania katika soka Agrey Morris katika hafla hiyo.

  
 Baba mwenye uzao wa mabondia Mzee Matumla kulia  akikabidhi tuzo ya mwanamchezo bora wa kigeni katika soka Emmanuel Okwi kwa Makamu Mwenyekiti wa klabu ya Simba Geofrey Nyange aliyepokea tuzo hiyo kwa niaba ya mchezaji huyo, katika tuzo  zinazoandaliwa na chama cha waandishi wa habari za michezo Tanzania TASWA na kudhaminiwa na kampuni ya bia ya Serengeti zilizofanyika usiku huu kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam

  
Mzee Ali Hassan Mwinyi akifurahia jambo wakati alipokuwa akimsikiliza mwenyekiti wa kamati ya Tuzo za TASWA Masoud Saanane katikati ni mwenyekiti wa TASWA Juma Pinto

  
 Mwenyekiti wa TASWA akimkabidhi tuzo yake mchezaji bora wa  mchezo wa Netiboli Lilian Sylidion kutoka kutoka Shule ya Filbert Bayi.

  
 Mkurugenzi wa kampuni ya bia ya Serengeti  Bw. Richard Wells akijadili jambo na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa KampunihiyoTeddy Mapunda  katika hafla hiyo

  
 Makamu Mwenyekiti wa Simba na Geofrey Nyange katikati akiwa katizo hafla hiyo kulia ni Jamal Rwambo mdau mkubwa wa michezo na kushoto ni Maulid Kitenge Makamu Mwenyekiti wa TASWA

  
Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Baraza la Michezo nchini BMT Bw. Dioniz Malinzi, Mwenyekiti wa kampuni ya bia ya Serengeti, Mark Bomani, aliyekuwa mkurugenzi wa kampuni ya bia ya Serengeti SBL Richard Wells na Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni hiyo Ephraim Mafuru


  Rais wa TFF, Leodegar Tenga wa pili kulia akiwa na Jellah Mtagwa kushoto kwake


Kaburu akimsaidia Kapombe kupokea tuzo ya Mwanamichezo Bora wa mwaka 2011 

Jun 14, 2012

Kuona Twiga Stars, Ethiopia 2,000/-

Kiingilio cha chini kwa mechi ya kufuzu kwa fainali za Afrika kwa Wanawake (AWC) kati ya Tanzania (Twiga Stars) na Ethiopia itakayochezwa Jumamosi (Juni 17 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ni sh. 2,000.
Kiwango hicho ni kwa washabiki kwa viti vya bluu, kijani na rangi ya chungwa. Viti hivyo kwa pamoja vinachukua jumla ya watazamaji 48,590 kwenye uwanja huo wenye uwezo wa kuchukua washabiki 60,000.
Viingilio vingine kwa mechi hiyo itakayoanza saa 10 kamili jioni ni sh. 5,000 kwa VIP B na C wakati VIP A itakuwa sh. 10,000. Tiketi zitauzwa uwanjani siku ya mechi kuanzia saa 3 asubuhi.
Mechi hiyo itachezeshwa na waamuzi Grace Msiska atakayepuliza filimbi wakati wasaidizi wake ni Bernadettar Kwimbira, Happiness Mbandambanda na Linda Chikuni, wote kutoka Malawi. Kamishna ambaye anatoka Kenya ni Maqulate Atieno. Waamuzi hao wamewasili jana.
blog yenu ya Bongo Yetu inawahimiza wapenda soka wote kujitokeza kwa wingi kuisapoti na kuipa nguvu timu yetu ya taifa ya wanawake aka twiga stars

Taifa Stars Yajipanga Kuikabili Msumbiji





kikosi cha timu ya Taifa
Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen amesema ili kuitoa Msumbiji ‘Mambas’ kwenye michuano ya Afrika ni lazima timu yake ishinde mechi ya marudiano itakayochezwa Juni 17 mwaka huu jijini Maputo.

Mechi ya marudiano kusaka tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 
zitakazofanyika mwakani nchini Afrika Kusini itachezwa kwenye Uwanja wa Taifa ulioko Zampeto nje kidogo ya Jiji la Maputo kuanzia saa 9 mchana kwa saa za huko.

Kim amewaambia Waandishi wa Habari leo (Juni 13 mwaka huu) kuwa maandalizi ya kikosi chake yanakwenda vizuri ingawa ana wachezaji watatu ambao ni majeruhi; kipa Mwadini Ali, na mabeki Nassoro Masoud Cholo na Waziri Salum.
Amesema wachezaji hao hawatakuwemo kwenye msafara wa timu hiyo utakaoondoka Juni 15 mwaka huu saa 11 alfajiri kwa ndege ya Kenya Airways kupitia Nairobi.

Kocha huyo amesema baada ya mechi tatu maendeleo kiuchezaji kwa timu yake inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager ni mazuri ingawa bado anafanyia kazi kwa nguvu safu ya ushambuliaji. Mechi iliyopita Taifa Stars iliifunga Gambia 2-1 huku mabao yote yakifungwa na mabeki.

Iwapo Taifa Stars itaitoa Msumbiji katika raundi ya mwisho itapangiwa moja kati ya timu 16 zilizocheza Fainali za AFCON zilizofanyika Januari mwaka huu katika nchi za Gabon na Equatorial Guinea. Katika mechi ya kwanza dhidi ya Msumbiji iliyochezwa Dar es Salaam, Februari 29 mwaka huu timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1.

Taifa Stars ambayo msafara wake utakuwa na wachezaji 20 itaagwa kesho (Juni 14 mwaka huu) saa 6 mchana kambini kwao- hoteli ya Accommondia (Tansoma) jijini Dar es Salaam.  Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) kwa ajili ya kujenga afya kupitia mpira wa miguu.

Jun 12, 2012

TFF: Yondani atacheza Yanga 100%




LAMPS COLLIN
UTATA wa usajili wa Kelvin Yondani unaelekea kupata majibu mapema baada ya kuthibitika kuwa ataichezea Yanga msimu ujao.

Mmoja wa wajumbe wa kamati mmojawapo ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) aliithibitishia Mwanaspoti jana Jumatatu kuwa Yondani atacheza Yanga msimu ujao baada ya kugundua udanganyifu uliofanyika Simba.

"Hapa tuwe wa kweli. Simba wanasema walimsainisha Yondani Desemba mwaka jana, tunajua kuwa Yondani alikuwa na matatizo na Simba wakati huo angesaini vipi mkataba mpya?" Alihoji mjumbe huyo wa TFF.

Mjumbe huyo alisema Simba wanaonekana kushindwa mapema katika kesi hiyo kwa sababu kama wangekuwa wanamtaka Yondani wangemsainisha kabla hajaingia miezi sita ya mwisho na mkataba wake ungesajiliwa TFF.

"Hivi unadhani Simba wangekuwa wanamtaka Yondani wangesubiri mpaka mkataba wake uishe?" Alihoji.

"Huyu sisi tuna taarifa kuwa alisaini Simba baada ya timu kurejea kutoka Algeria katika Kombe la Shirikisho. Ila walichokifanya ni kurudisha nyuma tarehe ya usajili ili ionekane amesajili Desemba.

"Hata kama amesajili Desemba bado walichelewa kwa sababu wakati huo tayari Yondani alikuwa amebakiza mkataba wa miezi sita, hivyo alikuwa huru kusaini klabu yoyote. "

Mwanaspoti ilipomuuliza Yondani atacheza timu gani msimu ujao alisema: "Kwa mazingira yote hayo ni dhahiri atacheza Yanga kwa asilimia mia."

Familia ya Yondani
Kaka mkubwa wa Kelvin Yondani ambaye pia ni wakala wa mchezaji huyo, Sunday Patrick ameridhia beki huyo kwenda Jangwani.

Sunday aliiambia Mwanaspoti wiki iliyopita kuwa: "Sisi kama familia kwa moyo mmoja tupo na Yondani katika uamuzi wake, cha msingi yeye amefuata sheria na hana mkataba wowote na Simba ndio maana hata sisi tumempa baraka za kwenda Yanga, pia viongozi wa Simba wanapaswa kufahamu kuwa mchezaji huyu bado ni mdogo na anatafuta maisha hivyo wamuache afanye uamuzi wake."

Kauli ya Yondani
Yondani ambaye awali alidai kusaini Simba, Alhamisi iliyopita aliikana kauli hiyo na kusema amesaini Yanga.
"Nimesaini Yanga, nawatakia kila la kheri Simba."

Yondani amelamba Sh.30 milioni kutoka Yanga na atakuwa akilipwa mshahara wa Sh 800,000 ingawa kuna taarifa kuwa ameongezewa na atakuwa akilipwa Sh milioni moja kwa mwezi huku ikidaiwa Simba ilipanga kumpa Sh 25 milioni na angelipwa mshahara wa Sh 800,000.

Kanuni ya TFF
Kanuni ya 43 ya TFF ya masharti ya mikataba kati ya wachezaji na klabu kifungu cha 3 kinasema; " Klabu inayotarajia kuingia mkataba na mchezaji wa kulipwa haina budi kuiarifu klabu yake ya sasa kwa maandishi kabla ya kufanya makubaliano na mchezaji huyo wa kulipwa.

Mchezaji wa kulipwa atakuwa huru tu kuingia mkataba na klabu nyingine iwapo mkataba wake na klabu yake ya sasa umekwisha au utakwisha baada ya miezi sita. Uvunjaji wowote wa sharti hili utastahili vikwazo vinavyofaa."

Tafsiri ya kanuni
Kutokana na kanuni hiyo, Yondani alikuwa huru kufanya mazungumzo au hata kusaini mkataba na klabu yoyote tangu Desemba mwaka jana kwa sababu mkataba wake ulikuwa umebakiza miezi sita kwani umekwisha Mei 31 mwaka huu.


chanzo na http://www.mwanaspoti.co.tz                                                                 

Jun 9, 2012

Yanga waipiga Simba bao la tatu




MICHAEL MOMBURI
USAJILI wa Ligi Kuu ndio kwanza umeanza kunoga lakini matajiri wa Yanga wameshaipiga Simba mabao matatu ya haraka haraka na yamebaki mawili tu kuchomoa kipigo cha mabao 5-0 ilichokipata uwanjani kwenye mechi ya Ligi Kuu Bara msimu uliopita.

Bao la kwanza ambalo Yanga walilifunga ni usajili wa kiungo Nizar Khalfan. Simba ilitangaza kumsajili mchezaji huyo, lakini Yanga ikafanya umafia ikamuwekea noti mezani akamwaga wino na kumtaka rasmi kwamba yeye ni mali ya Yanga. Hilo likapita kila mtu akauchuna.

Kama masihara, Mwanaspoti ikafichua kwa mara ya kwanza kuwa beki Kelvin Yondani amesaini Yanga na Simba.

Simba walikanusha habari hizo kwa nguvu zote, lakini Yanga wakatoa uthibitisho wa picha na maandishi bado Simba wakasisitiza wana mkataba naye. Yondani akaibuka Alhamisi usiku na kutamka kwa mdomo wake; "Nimesaini Yanga na naomba ushirikiano wa kila hali, naishukuru Simba kwa kunifikisha hapo nilipo nawataki kila la kheri."

Kabla hilo halijapoa hapa kuna jingine kali ambalo ni bao la tatu. Yanga imethibitisha kumsajili kipa wa Simba, Ally Mustapha 'Barthez' kwa thamani ya Sh 18 milioni lengo ikiwa ni kuikimbia nafasi yake maalum aliyowekea kwenye benchi la Simba kuanzia dakika ya kwanza mpaka ya mwisho wa mechi zote kila msimu.

Habari za kuaminika ambazo Mwanaspoti inazo ni kwamba Barthez alisainishwa na Seif Ahmed 'Magari' sambamba na Abdallah Bin Kleb ambaye anagombea nafasi ya ujumbe kwenye uchaguzi ujao wa Yanga. Matajiri hao wawili ndio wanaoongoza jopo la vibosile wengine wanaowezesha usajili wa Yanga kwa ajili ya msimu ujao.

"Barthez ameshasaini kila kitu wiki hii na fedha zake amechukua, ni kipa mzuri sana na atacheza sana akiwa na Yanga.

Tutakachofanya tutawapa Mtibwa Shabaan Kado na wao watupe mchezaji mmoja wa ndani kwavile Kado bado tuna mkataba naye,"mmoja wa viongozi wa usajili aliithibitishia Mwanaspoti.

"Tutabaki na Barthez na Said Mohammed, suala la Yaw Berko bado halijafikiwa muafaka wa moja kwa moja bado tunajadiliana lakini muda mfupi ujao kila kitu kitakuwa wazi, Berko tatizo lake la majeruhi ya mara kwa mara ndio inatupa wasiwasi,"aliongeza kiongozi huyo aliyekiri kwamba wamemkosa kiraka wa Uganda, Owen Kasule aliyesajiliwa El Merreikh.

"Tupo kwenye mazungumzo na Danny Mrwanda na Mussa Mgosi lakini kama tukifanikisha kumalizana na Mrwanda kwa wakati hatutamsajili Mgosi,"kilisema chanzo chetu.

Mwanaspoti linajua kwamba Bin Kleb aliyewezesha na kumsajili Haruna Niyonzima 'Fabregas' msimu uliopita, amepania kushusha wachezaji kadhaa wenye majina makubwa Yanga na jana Ijumaa jioni kulikuwa na kikao kizito jijini Dar es Salaam kukamilisha suala hilo.

Wachezaji wengine waliothibitishwa kusaini Yanga ni beki Juma Abdul wa Mtibwa, Barthez na Kelvin Yondani wote Simba, Nizar Khalfan(huru) na David Luhende wa Kagera.

Wachezaji walioko kwenye orodha ya kuachwa Yanga ni Shadrack Nsajigwa, Kiggi Makassi, Godfrey Bonny, Abuu na Zubeir Ubwa, Bakar Mbegu, Chacha Marwa, Davies Mwape wa Zambia na Kenneth Asamoah wa Ghana.

chanzo na mwanaspoti